Ye Soya
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 237
- 249
Mimi nimeota niko kijijini kwetu nilikozaliwa. Nikawa nimekaa sehemu nikakutana na Hayati Magufuli akiwa amevaa Kofia ya Pama na shati la kitenge na suruali nyeusi. Tena wakati nakutana nae nilijua kabisa nimekutana na mtu ambye ameshafariki. Tukaongea nae mambo mengi ya miradi ya kusafirisha gesi nikawa namuambia kwamba yote baada ya yeye kuondoka imekwama. Alionekana kusononeka sana.
Pia baada ya mazungumzo nae akaniomba lift kwenye kigari changu lakini baadae alishuka baada ya kuona kigari hakiko sawa. Aliniomba hela kadhaa nikampa ingawa wengine ambo walimuona alipowaomba hela walikataa kwa woga kwamba wanampa hela mtu ambaye alishaondoma duniani. Niliachana nae tukaagana na mimi nikaenda kijiweni kwa washkaji zangu tukaendelea na stori tofauti kabisa. Sasa hii ndoto iko na maana gani kwangu? Folk Part II na wataalam wengine kama Mzizimkavu na Mshana Jr msaada please katika ndoto hii.