Andika kauli au msemo mmoja unaoukumbuka kutoka kwa hayati Magufuli

Andika kauli au msemo mmoja unaoukumbuka kutoka kwa hayati Magufuli

images

Nilichomuelewa Jpm, kama kuna watu aliwaumiza ni kwa ajili ya Tanzania.
Hakuamini kama siasa na demokrasia ingeleta maendeleo.
Aliona Tanzania ipo nje ya muda katika kila nyanja, hivyo alikua na mipango na mikakati yake binafsi kichwani kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Aliyempinga alimuona ni mpingaji wa maendeleo na hawatakii mema waTanzania.

Alikua yupo radhi kufanya maamuzi magumu na kukubali lawama lakini kikubwa nchi ipige hatua.

Jpm alikua na ideologies zake ambazo wengine walimuona dictator, lakini kwa nchi ilipokuwa imefika naungana na Jpm.

"Nimesacrifice maisha yangu kwa ajili ya waTanzania masikini"
 
Ila huyu mwamba alikuwa anapenda sana kutuita ndugu zake
Si huyu bi kizimkazi anatuona kama mang'ombe tunasumbua. Muda mwingi anatamani awe angani kuliko kukaa na wananchi
Samia ni mtoto wa kishua kwao mambo safi, magu amehaso
 
Kwamba, akifa akawe "kiongozi wa malaika". Tumuulize nani aliyekwenda huko na kurudi...😱😱😱😱
 
Wakina mama mnapenda kutanuliwa biashara zenu,
Ila Mama naye yupo safi tu
 
JPM akiwafundisha watu kukwepa ushuru wa mazao.Aliwaambia usibebe tani 1 kwa mkupuo watakudai tozo.Bebe kidogo kidogo .Ukikutana na hao wakusanya tozo wakikuomba tozo wajibu ' kichwa kama tozo' halafu chapa lapa.
😂😂😂
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
images

Nilichomuelewa Jpm, kama kuna watu aliwaumiza ni kwa ajili ya Tanzania.
Hakuamini kama siasa na demokrasia ingeleta maendeleo.
Aliona Tanzania ipo nje ya muda katika kila nyanja, hivyo alikua na mipango na mikakati yake binafsi kichwani kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Aliyempinga alimuona ni mpingaji wa maendeleo na hawatakii mema waTanzania.

Alikua yupo radhi kufanya maamuzi magumu na kukubali lawama lakini kikubwa nchi ipige hatua.

Jpm alikua na ideologies zake ambazo wengine walimuona dictator, lakini kwa nchi ilipokuwa imefika naungana na Jpm.

"Nimesacrifice maisha yangu kwa ajili ya waTanzania masikini"
Alikua mzalendo wa kweli. Sio hawa wanaohubiri uzalendo kwa raia alaf wao sio wazalendo
 
Andika msemo au kauli moja kutoka kwa raisi wetu kipenzi cha watanzania Pombe Magufuli ambao unaukumbuka. Andika msemo huo mpaka msomaji akisoma asisimke ausome msemo huo kwa sauti ya Magufuli.

Mie naanza " Mimi nataka kama ni kunipenda, mnipende kwa ajili ya kazi. Kama ni kunichukia mnichukie kwa ajili ya kazi. Lakini nataka niwaambie ndugu zangu wa ukerewe na watanzania kwa ujumla, kwa haya tunayoyafanya matokeo yake mtayaona. Siku moja mtakuja kuzungumza alikuwepo kamagufuli"

"Basi kama tumerogwa mtuombee nyinyi mapadri, wachungaji, mashehe kama ni mapepo basi yaondoke. Na ndo maana mtu ukizungumza kutetea maslai ya nchi unaonekana you are different. Mtu amechaguliwa na watu unakuta kwenye jimbo lake umasikini mkubwa lakini anatetea haya ya upumbavu ( ufisadi). Maslai ya nchi is not politics, ni watu tuonaowaongoza"

"Na nataka niwaeleze ndugu zangu mimi sipendi sana kusafiri kwa sababu ninapenda kubana matumizi, nimealikwa sehem nyingi nimealikwa Ulaya na sehem zingine bado sijaenda"

Wee unakumbuka msemo gani wa Mgufuli?
"Ndugu zangu ipo siku mtanikumbuka, ipo siku mtanikumbuka na ninajua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya"

Rip Rais wa TAIFA takatifu la TANZANIA pengo lako halitazibika ndo kwanza linazidi kuzibuliwa
 
1.Mimi ni Raisi jiwe kweri kweri
2.Sitaki mtu anipende,nishapendwa na mke wangu inatosha.
3.Nitatumbua majipu kweri kweri
 
Back
Top Bottom