Andika kauli au msemo mmoja unaoukumbuka kutoka kwa hayati Magufuli


Nilichomuelewa Jpm, kama kuna watu aliwaumiza ni kwa ajili ya Tanzania.
Hakuamini kama siasa na demokrasia ingeleta maendeleo.
Aliona Tanzania ipo nje ya muda katika kila nyanja, hivyo alikua na mipango na mikakati yake binafsi kichwani kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Aliyempinga alimuona ni mpingaji wa maendeleo na hawatakii mema waTanzania.

Alikua yupo radhi kufanya maamuzi magumu na kukubali lawama lakini kikubwa nchi ipige hatua.

Jpm alikua na ideologies zake ambazo wengine walimuona dictator, lakini kwa nchi ilipokuwa imefika naungana na Jpm.

"Nimesacrifice maisha yangu kwa ajili ya waTanzania masikini"
 
Ila huyu mwamba alikuwa anapenda sana kutuita ndugu zake
Si huyu bi kizimkazi anatuona kama mang'ombe tunasumbua. Muda mwingi anatamani awe angani kuliko kukaa na wananchi
Samia ni mtoto wa kishua kwao mambo safi, magu amehaso
 
Kwamba, akifa akawe "kiongozi wa malaika". Tumuulize nani aliyekwenda huko na kurudi...😱😱😱😱
 
Wakina mama mnapenda kutanuliwa biashara zenu,
Ila Mama naye yupo safi tu
 
JPM akiwafundisha watu kukwepa ushuru wa mazao.Aliwaambia usibebe tani 1 kwa mkupuo watakudai tozo.Bebe kidogo kidogo .Ukikutana na hao wakusanya tozo wakikuomba tozo wajibu ' kichwa kama tozo' halafu chapa lapa.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Reactions: EEX
Alikua mzalendo wa kweli. Sio hawa wanaohubiri uzalendo kwa raia alaf wao sio wazalendo
 
"Ndugu zangu ipo siku mtanikumbuka, ipo siku mtanikumbuka na ninajua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya"

Rip Rais wa TAIFA takatifu la TANZANIA pengo lako halitazibika ndo kwanza linazidi kuzibuliwa
 
1.Mimi ni Raisi jiwe kweri kweri
2.Sitaki mtu anipende,nishapendwa na mke wangu inatosha.
3.Nitatumbua majipu kweri kweri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…