Andika neno lolote chungu, zito, lenye maumivu ambalo hautakujaa kusahau mtu alikutamkia

Andika neno lolote chungu, zito, lenye maumivu ambalo hautakujaa kusahau mtu alikutamkia

Tarehe 17,March ya mwaka ule.'Poleni sana,baba yenu aliwadekeza sasa ameondoka,sijui mtaishije'.Muda huo machozi yananibubujika,nipo mimi,mdogo wangu,na kaka yetu,tunabadilisha nguo,tusafiri twende kijiji ambacho mwili wa mzee utazikwa.Kwakweli nilihuzunika sana,hadi kesho naamini mimi kuwa hivi ni kwasababu ya mzee,kutuacha tukiwa wadogo.Pumzika kwa amani baba yangu,hapa naandika ila machozi yananilengalenga japo ni zaidi ya miaka 20 toka mzee aondoke.He was a real man.R.I.P once again.
 
Dear eX aliwahi niambia nanukuu "bora ufe tu sijui uliniloga hivi nilikupendea nini? Mtu akishakuombea kifo n dhahiri hajali chochote nilikasirika nikamjibu vibaya ukawa ndio mwsho wetu.

Baba mkubwa aliwahi niambia "utazunguka sana lakini hutokaa uyaone mafanikio, utashika 100 haitokaa wala kuongezeka, utalima na hautavuna hata kama ni mchicha wa wiki mbili, na sijawahi hata kumkosea chochote. Huyo huyo nikienda mkoani nyumbani ndio wakwanza kuomba hela. Hawa ndugu hawa basi tu Mungu azidi kunilinda na kupambana na watesi wangu.

Tuchunge sana vinywa vyetu kuna maneno si busara kumtamkia mtu, binafsi ndugu zangu wananisema sana kwa kunyamazia baadhi ya mambo ila baadae wanaona ni afadhali ya mimi nilieyakalia kimya. Tuwe na chembe za utu kwenye maneno yetu.
 
Tarehe 17,March ya mwaka ule.'Poleni sana,baba yenu aliwadekeza sasa ameondoka,sijui mtaishije'.Muda huo machozi yananibubujika,nipo mimi,mdogo wangu,na kaka yetu,tunabadilisha nguo,tusafiri twende kijiji ambacho mwili wa mzee utazikwa.Kwakweli nilihuzunika sana,hadi kesho naamini mimi kuwa hivi ni kwasababu ya mzee,kutuacha tukiwa wadogo.Pumzika kwa amani baba yangu,hapa naandika ila machozi yananilengalenga japo ni zaidi ya miaka 20 toka mzee aondoke.He was a real man.R.I.P once again.
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom