Andika tabia usiyoipenda ya baadhi ya member wa JF

Andika tabia usiyoipenda ya baadhi ya member wa JF

Wakuu nimeanzisha huu kwa lengo la kuonyana kuhusu tabia mbovu zinazoonekana kwa baadhi ya member wa jamiiforums.

Naanza mimi.
1. Sipendi kabisa tabia ya baadhi ya members kuingilia na kuvuraga mada za wenzao kwa kuanzisha majibizano yasiohusika na mada iliyopo. mfano unakuta mtu kaanzisha mada yake ya kutafuta mteja wa bidhaa yake au kutafuta kazi au kuomba ushauri juu ya suala fulani, sasa unakuta kuna member wanaanza kuleta mazungumzo ya ajabu yasiyohusika kabisa. Tabia hii ya hovyo.

2. Tabia nyingine inayokera ni kukuta watu wanapoteza muda kudharau miji au mikoa mingine ndani ya nchi kana kwamba dharau zao zinawasaidia chochote.

Je wewe umeona tabia ipi inayokukera jamvini?
Sipendi tabia ya watu kusimamia kitu ambacho hawajakieleza vizuri kama wewe.

Mipaka ya kusema huyu anajadili ndani ya mada, na huyu anavuruga, unaiwekaje?

Na kwa nini uone anayevuruga mada ni mtu mbaya badala ya kumchukulia kama changamoto ya wewe kuonesha ukomavu wa kifikra kwa kuweza kuendelea na mada bila "kutoka relini" hata baada ya mtu kutaka kukuvuruga?

Na kwa nini ujione una ulazima wa kumsoma mtu wakati ushaona anavuruga mada? Unajua kumblock mtu usione posts zake tena? Mimi kuna watu wengi nimewaona hawana mada za kujadili zaidi ya vurugu, ama nawachukulia kama "chuo cha ukomavu wa uvumilivu wa kitabia" ama nawa block nisione mada zao kabisa. Sijawahi kulalamikia hawa, kwa sababu teknolojia na kujielewa kwangu kiakili haviniruhusu kulalamika juu ya hawa.

Kwenye kudharau miji, kwangu hapo, kitu muhimu ni, wanachosema ni kweli au uongo?

Maana kama mji unastahili kudharauliwa, kwa ujinga fulani uliomo katika mji huo, ukisema uuheshimu mji huo na kuacha kuudharau unakuwa si tu hujitendei haki wewe mwenyewe kwa kuheshimu kitu kisichostahili heshima, bali pia unakuwa hujautendea haki mji huo kwa kuudharau mpaka ubadili ujinga huo.

Mathalan, mji una watu wanazibua vyoo na kumwaga maji ya mavi barabarani, hii ni tabia ya uchafu.

Nikisema watu wa mjii huu wana tabia ya uchafu, wenyewe wakisoma na kuona kweli huu ni uchafu, na ni ukweli, kwanza kabisa kauli yangu inakuwa si dharau, ni ukweli. Wengine wanaweza hata kusema ni kauli ya upendo. Mtu asiyejali hili hana upendo, anayejali kiasi cha kuliongelea anaweza kuwa kaongea kwa sababu hapendi kuona mji huu una uchafu.

Sasa unachoweza kuona kwamba ni dharau wewe, mwingine anaweza kukisema kwa nia safi kabisa na upendo.

Unajuaje hii ni dharau bila kuangalia ukweli uko wapi?

Mtu akikwambia ukweli mchungu ambao hupendi kuusikia, utasema kakudharau?

Mimi naona kakuheshimu sana mpaka kukuambia ukweli, angekudharau angejifanya hauoni ukweli.
 
Sipendi wanaoponda juhudi na kuichafua Serikali sema basi tu inabidi tuvumiliane.
Habari yako umeiandika kifupi sana, wakati inahitaji maelezo zaidi.

Juuhudi zote za serikali ni nzuri? Unajuaje hawa wanaponda kuichafua serikali, na si kwamba serikali ina uchafu na hawa wanausema tu uchafu ambao upo serikalini?
 
Binafsi hakuna kinachonikera hapa. Naamini kila binadamu yuko tofauti na mwenzake na katika utofauti huu ndimo mna ukamilifu wetu. Hakuna anachoweza kufanya kiumbe huyu aliyejipachika cheo cha uHomo Sapiens kikanishangaza wala kunikera hasa humu mitandaoni !!!
Hii hali ni ngumu sana kuifikia kiuhalisia.

Ila hata kama hujaifikia bado, unaelewa hii kanuni tu, unakuwa na kujielewa kwa hali ya juu sana.

Mimi kuna watu wamejaribu kunikera nikawaambia "ubongo wako haujaweza kufikia uwezo wa kunikera unavyotaka".
 
Habari yako umeiandika kifupi sana, wakati inahitaji maelezo zaidi.

Juuhudi zote za serikali ni nzuri? Unajuaje hawa wanaponda kuichafua serikali, na si kwamba serikali ina uchafu na hawa wanausema tu uchafu ambao upo serikalini?
Mada imesema nitaje tabia nisiyopenda na sina sababu yakukuelewesha zaidi hapo,tuvumiliane.
 
Back
Top Bottom