Andiko hii 1 Samweli 15 linatoa picha kinachoendelea huko Israel

Andiko hii 1 Samweli 15 linatoa picha kinachoendelea huko Israel

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Sitaki kujua sana kuhusu huyu Mungu wa namna hii ila maagizo yake kwa watu wake hayapaswi kuendelea kuchukuliwa kawaida kwani yanahamasisha na kuchochea mauaji makubwa yanayo tekelezwa na Netanyahu na genge lake.

Kwa nini nimemtaja Netanyau katika hili ? Kwa sababu yeye kama waziri mkuu wa Israel ndie aliyeleta mjadala wa wa amaleki mezani akiwakumbusha Waisrael kuhusu habari za waamaleki kwa yanayo endelea kati yake na Hamas na Wapalestina.

Nini anacho maanisha Netanyahu katika hili ? Ni kuto waonea huruma hata kidogo Wapalestina kama yalivyo tendeka kwa waamaleki kuanzia wao wake kwa waume,watoto mpaka wanyama na ndicho kinacho endelezwa na majeshi yake mpaka sasa pale Palestine.

Sina hakika kama Netanyau anatekeleza maagizo yote ya Mungu wao kama anavyotaka au ndio anachukua yale yafurahishayo nafsi yake pekee kwa sababu Mungu wao hakuwahi wachekea na kuwakumbatia mashoga na wasagaji labda kama kabadilishwa.

Sasa na Netanyahu kwa ile ardhi Netanyau aiitayo ardhi takatifu imegeuzwa kuwa ardhi ya wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake kuoneshana ufundi wa mahaba( tuachane na haya wenda Mungu wao Netanyahu hubadilika au hubadilishwa kwa sababu mbalimbali turudi kwenye mauaji ya kutisha ya jenerali huyu kamanda wa vita Netanyahu)

1 Samweli 15​

Bwana Anamkataa Sauli Asiwe Mfalme
1 Samweli akamwambia Sauli, “Mimi ndiye ambaye Bwana alinituma nikutie mafuta uwe mfalme juu ya watu wake Israeli, basi sasa sikiliza ujumbe kutoka kwa Bwana. 2 Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipanda kutoka Misri. 3 Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ngʼombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”

Hili andiko halina afya hata kidogo inanishangaza pamoja ya kwamba biblia imepokea maboresho kadhaa toka kuanzia Roma mpaka leo lakini bado andiko hili lina endelea kung'ang'aniwa kuwepo ndani yake sijui lengo lipi haswa ? Dunia nzima yote iteketezwe ?
 
Nani alifute?

Leo nani ni Muisrael halisi?
Linaweza futwa hata kwa jamii ya wakristu kwa sababu ukristu haufagilii mauaji ya hovyo ni upendo hivyo ndivyo ulivyo na unavyo jitambulisha.
 
Israel itaendelea kushinda na kushinda na kuendelea kushinda hadi ishinde sana

"Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe;
nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele". Ezekiel 37:20-21
 
Linaweza futwa hata kwa jamii ya wakristu kwa sababu ukristu haufagilii mauaji ya hovyo ni upendo hivyo ndivyo ulivyo na unavyo jitambulisha.
Maisha ya mashariki ya kati tangu enzi za Biblia hata Leo hayajawahi kutulia. Tunasoma vita,visasi na kuuwana tangu enzi na enzi.

Mimi nadhani ni asili tu ya watu wa mashabiki ya kati Wana asili ya ukatili na roho mbaya,kuanzia wayahudi hadi waarabu. Ustaarabu wa dini ulikuja kuwafanya wawe binadamu kidogo.

Nionavyo Mimi,Biblia na Quran zingeandikwa kwa watu wa Africa au america kusini Nina uhakika bingekuwa vitabu vya tofauti kabisa. Maana Africa na baadhi ya mataifa ya america ni watu wapole kiasili na wenye upendo.
 
Tatizo sio kushinda vita Israel haitakuwa taifa la kwanza kufanya hivyo.

Tatizo ni hilo andiko unakubaliana na maagizo hayo yakitendeka kwa jamii yako ?
 
Maisha ya mashariki ya kati tangu enzi za Biblia hata Leo hayajawahi kutulia. Tunasoma vita,visasi na kuuwana tangu enzi na enzi.
Hata maisha yetu sisi waafrika katika historia wamejaa matendo ya ajabu tuliyokuwa tukitendeana lakini mengi ya kale tumeyaacha tumebadilika ni kipi kinachoweka ugumu wao kubadilika ?
 
Mimi nadhani ni asili tu ya watu wa mashabiki ya kati Wana asili ya ukatili na roho mbaya,kuanzia wayahudi hadi waarabu. Ustaarabu wa dini ulikuja kuwafanya wawe binadamu kidogo.

Nionavyo Mimi,Biblia na Quran zingeandikwa kwa watu wa Africa au america kusini Nina uhakika bingekuwa vitabu vya tofauti kabisa. Maana Africa na baadhi ya mataifa ya america ni watu wapole kiasili na wenye upendo.
Sawa sawa
 
Linaweza futwa hata kwa jamii ya wakristu kwa sababu ukristu haufagilii mauaji ya hovyo ni upendo hivyo ndivyo ulivyo na unavyo jitambulisha.
Ufunuo wa Yohana 22:18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
 
Ufunuo wa Yohana 22:18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Haitakuwa mara ya kwanza Biblia kufanyiwa maboresho.
 
Back
Top Bottom