Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mimi si msomaji mzuri sana wa Maandiko Matakatifu , lakini ninafahamu kidogo kwamba ndani ya Biblia kuna kisa kilichomhusu Yesu na Petro , inaelezwa kwamba Petro alijaribu kupita Juu ya Maji kama alivyokuwa anafanya Yesu , yaani Yesu alikuwa na kawaida ya kukatiza tu Juu ya Maji bila kuzama kama sisi tunavyokatiza barabarani , sasa Bwana Petro naye akaona ngoja apite juu ya Maji kama Yesu alivyokuwa anafanya .
Maandiko Matakatifu yanaeleza kwamba , baada ya kujaribu tu Petro akaanza kuzama , baada ya kuona hivyo haraka sana Petro akamwita Yesu na kumuambia Yesu amshike mkono kumuokoa ili asizame , inadaiwa kwamba Bwana Yesu akanyoosha mkono akamshika Petro na kumuokoa na hakuzama tena , Wanazuoni wanasema kwamba Iwapo Ndugu Petro angenyamaza kimya bila kuomba msaada wa Yesu basi bila shaka angezama na pengine angeliwa na Mamba .
Andiko hili linatufundisha kwamba tunapopatwa na matatizo , tusinyamaze , tufungue vinywa vyetu kuomba Msaada ili tuokolewe