Andiko la Thadei Ole Mushi lilivyonifikirisha

Mimi si msomaji mzuri sana wa Maandiko Matakatifu , lakini ninafahamu kidogo kwamba ndani ya Biblia kuna kisa kilichomhusu Yesu na Petro , inaelezwa kwamba Petro alijaribu kupita Juu ya Maji kama alivyokuwa anafanya Yesu , yaani Yesu alikuwa na kawaida ya kukatiza tu Juu ya Maji bila kuzama kama sisi tunavyokatiza barabarani , sasa Bwana Petro naye akaona ngoja apite juu ya Maji kama Yesu alivyokuwa anafanya .

Maandiko Matakatifu yanaeleza kwamba , baada ya kujaribu tu Petro akaanza kuzama , baada ya kuona hivyo haraka sana Petro akamwita Yesu na kumuambia Yesu amshike mkono kumuokoa ili asizame , inadaiwa kwamba Bwana Yesu akanyoosha mkono akamshika Petro na kumuokoa na hakuzama tena , Wanazuoni wanasema kwamba Iwapo Ndugu Petro angenyamaza kimya bila kuomba msaada wa Yesu basi bila shaka angezama na pengine angeliwa na Mamba .

Andiko hili linatufundisha kwamba tunapopatwa na matatizo , tusinyamaze , tufungue vinywa vyetu kuomba Msaada ili tuokolewe

View attachment 2894079
Ni somo muhimu sana kwenu, wenye vyama vya siasa na kwa wananchi wote.
Binafsi nilichonyanyua hapa ni "lugha iliyotumika kufikisha ujumbe muhimu kwa wananchi."

Lugha na mifano ya namna hiyo inaingia moja kwa moja vichwani mwa waTanzania. Kama chama kinalo jambo kinataka kuliwasilisha kwa wananchi kirahisi na kwa haraka, na liwaingie ipasavyo wananchi hao, tumia lugha wanayoielewa.

Huu ni mfano wa kidini ya Kikristo, ipo mifano mingi ya aina hiyo hata kwenye dini zingine; na hata nje ya imani yoyote; hata kwenye upagani mifano ipo.

Tatizo la vyama vya upinzani kuwafikia wananchi kwa sehemu kubwa ni lugha inayowashinda wananchi kuielewa.
 
Amina, kwa sasa hata mifano ya Wapagani tutaendelea kuitumia
 
Dah!
Nilikuwa sijasoma/sijamsoma Ole hayo maneno huko chini nilipo andika kujibu uliyo andika wewe kabla ya hayo ya Ole.

Sasa nabaki nkishangaa, na nadhani ninajishangaa mwenyewe kukosa uelewa wa kuunganisha uhusiano kati ya mabandiko haya mawili.
Kama upo uhusiano, basi andiko la kwanza, ambalo ndilo nililojibu, litakuwa limekwenda shule sana. Ni fumbo zito, pamoja na kwamba ni lugha inayoeleweka kirahisi.

Sasa naomba ufafanuzi kama inawezekana. Kama haiwezekani, potelea mbali, nitaweka tafsiri yangu mwenyewe

N.B., Basi na isikupe taabu, kumbe jibu liko humu humu toka kwa wachangiaji wengine kwenye mada hii..
 
Sijaona jibu, kama Ole ni mzima, au alisha kwenda zake? Nimeona mahali humu humu R.I.P., mambo wakati mwingine yanakwenda haraka sana.
Niliandika hili baada ya Ole Mushi kufariki, Tuliojua kwamba kalishwa kitu tulipohoji afya yake ndio alijibu kama ulivyosoma pale juu, japo kuna wengine wanadai watu wa mfumo walidukua mawasiliano yake ili kupooza mambo baada ya maswali mengi kumuulizia (unganisha nukta)

Alifariki kwa matatizo ya Figo (wataalam wa afya wanajua uhusiano wa sumu na figo) Tanzia yake imo humu humu JF
 
Nilitaka niufunge huu ukurasa niondoke zangu, lakini fikra zikawa zinanikataza.

Huyo aliyeandika hayo yanayodaiwa yaliandikwa na Ole mwenyewe, baada ya( kupata nafuu?) - kumbe Ole mwenyewe akisha fariki...!
Hili jambo limesumbua sana akili.

Wewe umesema watu wa 'mfumo'. Watu wa mfumo ndiyo kazi zao hizi?

Acha tu niondoke.
 
Mwabukusi aliwahi kukana yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake akiwa selo na simu zake zikiwa zimeshikiliwa na Polisi, Yaani hata baada ya kunyang'anywa simu akaonekana anapost vitu Instagram, haraka sana alivyotoka akasema akaunti ni yake ila aliyeandika si yeye
 
Sielewi, mnasema Mungu anajua kila kitu, basi tatizo likinipata anajua, hakuna haja ya kumuomba. Kwani Yesu hakujua kwamba Petro angezama?
 
Mwabukusi aliwahi kukana yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake akiwa selo na simu zake zikiwa zimeshikiliwa na Polisi, Yaani hata baada ya kunyang'anywa simu akaonekana anapost vitu Instagram, haraka sana alivyotoka akasema akaunti ni yake ila aliyeandika si yeye
Ole alikuwa mtu wa CCM; halafu huyo mtu wa 'mfumo' kataka ionekane Ole wa CCM bado yupo kazini? Mbona hili linatatiza kueleweka! Au sahihi hiyo ya "Kidumu chama cha Mapinduzi" ilikuwa ni kupoteza lengo kulikotumiwa na hao watu wa mfumo.. Kwa nini?

Anyway, maana yangu ya kuuliza kama watu wa 'mfumo' wanafanya kazi hizi ni kwa sababu naona ni kazi isiyowahusu kabisa! Lakini najuwa, chini ya CCM kila jambo la hovyo linawezekana sana, kama polisi na walimu na wengine wanavyotumiwa hovyo hovyo tu.
 
Ohoooooo!!!
 
Back
Top Bottom