Andrew Chenge achukua fomu ya kugombea Uspika. Fahamu kuhusu wasifu wake

Andrew Chenge achukua fomu ya kugombea Uspika. Fahamu kuhusu wasifu wake

KUZALIWA

- Mbobezi wa Sheria Barani Afrika na "Alumni" wa Chuo kikuu bora Duniani- Havard cha Nchini Marekani Mh.Andrew John Chenge alizaliwa mwaka 1947 nchini Tanzania (Tanganyika wakati huo).

ELIMU

- Nguli huyu wa Sheria alianza safari ya kitaaluma katika Shule ya msingi Sasago (Musoma) kati ya mwaka 1955- 1958

- Kisha akajiunga na St. Pius Seminary Makoko Musoma kati ya mwaka 1959-1962

- Kisha akajiunga na St.Mary's Seminary Nyegezi mwanza kati ya mwaka 1963-1966 kwaajili ya masomo ya Sekondari.

- Kati ya mwaka 1967 - 1968 alijiunga na Mkwawa High school.

- Mwaka 1969 alikuwa kati ya wanafunzi wachache waliojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwaajili ya masomo ya Sheria (LL.B) na kufanikiwa kuhitimu kwa ufaulu wa juu mwaka 1972.

- Mwaka 1974 - 1975 alibahatika kuwa kati ya wanasheria wachache Duniani kujiunga na Chuo Kikuu cha Havard kwaajili ya Shahada ya uzamili aliyohitimu kwa ufaulu mkubwa.

UTUMISHI NA UZOEFU SERIKALINI

- Kati ya mwaka 1972 - 1990 alihudumu kama mwanasheria wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Kati ya mwaka 1990- 1992 alihudumu kama Naibu Mwanasheria Mkuu (D/AG)

- Kati ya mwaka 1993 -2005 alihudumu kama Mwanasheria mkuu wa serikali.

- Mwaka 2006 alihudumu kama Waziri wa Kwanza wa Ushirikiano wa Afrika mashariki

- Kati ya 2006-2008 alihudumu kama Waziri wa miundombinu katika serikali ya awamu ya nne.

UZOEFU KATIKA BUNGE

- Kati ya mwaka 2005 - 2020 alihudumu kama Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi

- Kati ya mwaka 2008 - 2010 alihudumu kama mjumbe wa kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha.

- Kati ya mwaka 2012-2013 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha

- Kati ya mwaka 2013-2015 alihudumu kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti

-Kati ya mwaka 2015- 2020 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria na pia kama mmoja wa Wenyeviti 3 wa Bunge.

#Bunge linahitaji kiongozi wa makamo kama ChengeView attachment 2078281
Hafai full stop
 
Nyie hamuingizi mgombea? Mmeshaanza kuwaona wana ccm Bora? Simunaonaga hakua aliye Bora ccm ila chadema pekeyake?
 
Hahhaha.. Kinachonifurahisha ni kwamba, wanaomshabikia Chenge ni chadema wale wale!
Mkuu kuwa CHADEMA unahitaji akili za kuvukia barabara tu. Empty mind, LEMA, SUGU, MSIGWA, MBOWE hao wote ni wazito chamani na hawana ELIMU yoyote.
 
Mkuu kuwa CHADEMA unahitaji akili za kuvukia barabara tu. Empty mind, LEMA, SUGU, MSIGWA, MBOWE hao wote ni wazito chamani na hawana ELIMU yoyote.
Ungekuwa na angalau robo ya akili walizonazo hao jamaa ungekuwa umejikomboa kifikra! Lakini kwa jinsi ulivyo punguani kamwe huwezi kuwaelewa!
 
Bibi tozo hawezi kumudu kumburuza huyu Mzee!
Kumburuza hawezi ila tu wataungana kutuhujumu maana mzee vipengele vyote vya katika anavijua kama sala ya baba yetu😅!

Akiingia huyu mjengoni swala la katiba mpya msahau watanzania maana jamaa ndio mchora ramani wa michongo yote ya upigaji😅anajua pa kuingilia na pa kutokea bila kukamatwa wala kuwa suspected!
 
Hizi ni dalili za umasikini uliotopea. Hutaki mtu akuzidi, hutaki kusikia mafanikio ya wenzako. Chuki hizi mnazitumia hadi muwapo makazini na mwisho mnakuwa wafitini.
Mafanikio kwa wizi? Yani kuhujumu taifa we unaita mafanikio?

Hii tabia ya ubinafsi wa namna hii watanzania tumeitoa wapi jamani, yani wagonjwa wafe kwa kukosa madawa ili wewe utanue na malaya kwa hela ambayo ingewasaidia walioko hospitali?
 
Chenge ni fisadi mwenye uzoefu wa kiwango cha lami katika kuiba mali za uma😁😁😁
16418874249070.jpg
 
Kumburuza hawezi ila tu wataungana kutuhujumu maana mzee vipengele vyote vya katika anavijua kama sala ya baba yetu😅!

Akiingia huyu mjengoni swala la katiba mpya msahau watanzania maana jamaa ndio mchora ramani wa michongo yote ya upigaji😅anajua pa kuingilia na pa kutokea bila kukamatwa wala kuwa suspected!
Halafu ukute anauswahiba na kabudi, mayoweeeeeeeeeee ngachoka kabsa meku.
 
Back
Top Bottom