Umeshudiwa ugeni mzito nzito Kyiv Ukraine, katika kipindi hiki cha mgogoro.
Rais wa umoja wa Ulaya amefika Kyiv. Mawaziri wakuu toka Czech, Slovenia, Poland na juzi UK nao wamefika pale wakajivinjari kwa raha zao.
Aungurumapo Simba mcheza nani?
Haitakuwa ajabu kusikia Marine Moja imetimba pale na wanaume wakivinjari mitaani Kyiv kama kwao.
Beberu hajawahi kufanya ajizi na usalama wake kama tulivyo sisi magwiji wa nyungu. Popote aendako yeye si habari mpya kumsikia akichukua jukumu lote la ulinzi likiwamo la anga ugenini.
Ilikuwa hivyo na Obama Dar es salaam. Ilikuwa nusu hivyo na Ghadafi ugenini.
Aupate wapi utulivu wa kuhutubia mabunge duniani Zelensky, kwenye hatari ya mvua ya makombora asiyokuwa na udhibiti nayo?
Yumkini ndicho kilichomfurusha Mrusi hadi aliko sasa.
Kukiitwa, "kukiona cha mtema kuni!"