Anga la Ukraine Yumkini mikononi mwa NATO

Anga la Ukraine Yumkini mikononi mwa NATO

Hii ni vita ya kipuuzi katika dunia iliyostaarabika....
Sikutaka kujibu mfululizo hivi ndani ya mada hii, lakini nimejikuta nashindwa kucheka, na kujizuia nisiweke mchango mwingine hapa.

Wewe unaiita "vita ya kipuuzi", kwa vile hujui kinachopiganiwa.

Halafu unaiita "dunia iliyostaarabika...), sijui ni dunia gani hiyo uliyonayo akilini mwako.

Hao jamaa wanaochochea vita huko wanajiita wao ndio "walio staarabika"! Wengine wote duniani bado ni watu mashetanishetani vile! Wasiostaarabika!
 
Mbona ziara ya Johnson haikutangazwa mapema kabla hajafika huko! Wanakwenda kwa kuvizia kama wachawi.
Hahahahahah mkuu ilitangazwaa niliona live CNN tangazo la yeye kutinga Kyiv, European union pia ilikuwa wazi sana hata siku 2 kabla
 
Hahahahahah mkuu ilitangazwaa niliona live CNN tangazo la yeye kutinga Kyiv, European union pia ilikuwa wazi sana hata siku 2 kabla

Habari mbaya sana hiyo kwa warusi wa Kigoma na kote kwingine waliko nchini
 
Umeshudiwa ugeni mzito nzito Kyiv Ukraine, katika kipindi hiki cha mgogoro.

Rais wa umoja wa Ulaya amefika Kyiv. Mawaziri wakuu toka Czech, Slovenia, Poland na juzi UK nao wamefika pale wakajivinjari kwa raha zao.

Aungurumapo Simba mcheza nani?

Haitakuwa ajabu kusikia Marine Moja imetimba pale na wanaume wakivinjari mitaani Kyiv kama kwao.

Beberu hajawahi kufanya ajizi na usalama wake kama tulivyo sisi magwiji wa nyungu. Popote aendako yeye si habari mpya kumsikia akichukua jukumu lote la ulinzi likiwamo la anga ugenini.

Ilikuwa hivyo na Obama Dar es salaam. Ilikuwa nusu hivyo na Ghadafi ugenini.

View attachment 2185031

Aupate wapi utulivu wa kuhutubia mabunge duniani Zelensky, kwenye hatari ya mvua ya makombora asiyokuwa na udhibiti nayo?

Yumkini ndicho kilichomfurusha Mrusi hadi aliko sasa.

Kukiitwa, "kukiona cha mtema kuni!"
Mwambieni Zelensky, serikali ya Tanzania chini ya Samia ipo tayari kujitolea kulinda anga la Ukraine kwa gharama sifuri. Na mbwa yeyote atakayeleta fyoko fyoko atashikishwa adabu.
 
... anajisahaulisha kwamba hadi picha zimerushwa live wakiwa kikaoni. Putin ndicho kiumbe kinacholindwa kuliko kitu chochote kwa sasa; ndicho kiumbe chenye hofu kuliko kiumbe chochote chini ya Jua kwa nyakati hizi; hata digidigi wana amani kuliko Putin.
Ulinzi wa Magufuli ni mara 100 ya ulinzi wa Putin
 
Marekani aliua Afigastan, Libya nk nk mbona hatukuona mkileta ushabiki. Hao watoto wanauwawa kwa Kiburi cha Rais wao, Rais wao angeona Uhai wa hao watoto una faida angemuita Mrus Mezan akubali yaishe, lkn kwakuwa anaona Kutumika na Marekani ni heri kuliko Uhai wa hao watoto mimi ni Nani niwe na Uchungu. Rais wao abebe lawama
Nilitegemea swali la mdau litapata jibu la kipumbavu kama hili.
 
Mwambieni Zelensky, serikali ya Tanzania chini ya Samia ipo tayari kujitolea kulinda anga la Ukraine kwa gharama sifuri. Na mbwa yeyote atakayeleta fyoko fyoko atashikishwa adabu.

Kujimwambafy hakujawahi kumwacha mtu salama.

Kuna wenzetu kimasikhara wamebaki kutoa povu:

IMG_20220409_224024_834.jpg
 
Mrusi wa Buza usichokijua NATO wataingilia kati muda siyo mrefu kumfurusha Putin,walikuwa wanamchora kwa mbali kuona pumzi yake wameshamuona kumbe msukule mwanzo ilikuwa nguvu ya soda.

Wanaenda kuzaa nae believe me!
Ujinga wa aina hiii ndio utafanya WaUkraine wateketee, hao NATO wataweka Base yao wapi?? Watakapojibizana na Mrusi watoto wa wapi watakufa?? Ndio mbaya zaidi maaana Warusi watakufa, WaUkraine Watakufa Mrusi atapiga kwa Washirika wa NATO wote madhara yatakuwa mara 100 zaidi. So kushangilia kwamva NATO aningilia ni ujuha na Upuuuzi. Jambo la kupigiwa chapuo na kushinikiza MRUSI akae meza Moja na Ukraine wayamalize basi hata kama yanawakera hao Mafirauni wa Magharibi yeye akubali ili kuokoa Uhai wa watu wake na siyo kusikiliza Magharibi na Amerika wana mshinikiza vipi
 
Uzalendo ni pamoja na kuwa tayari kuifia nchi si kusalimu amri.

Aghalabu ujinga zaidi nikujidhania kuwa na mawazo bora kabisa kuliko Ukraine nzima kama nchi.

Ujinga uliopitiliza na kutopea ni kudhani nchi zote zinazolaani UN si mali kitu ila wewe.

Mamburula kwenye ubora wetu:

IMG_20220303_102530_977.jpg
 
Mbona ziara ya Johnson haikutangazwa mapema kabla hajafika huko! Wanakwenda kwa kuvizia kama wachawi.
Kwa hiyo Urusi hana uwezo wa kuona? Hana spies hapo Kyiv kujua nani yupo au kaja?

Mbona Marais wengine wa EU hutamgaza kabisa kuwa siku fulani twaenda Kyiv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom