Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

Miranda kashajilengesha ,Marwa Fanya kweli dinner iwe dinner kweli
Hapana aisee. Wataharibu kazi. Halafu Marwa atapata wakati mgumu baadae kama Jona akizingua. Miranda akiwa upande wa BC unadhani Marwa atakuwa upande wa Jona au wa Beibe Miranda? Marufuku mapenzi kazini.[emoji6] [emoji6] [emoji6]
 
Shao akachinje bata mweusi
Katoboa daaah!
Mkuu Steve tunafukuza mwizi in silence mode ,good sana Mkuu wetu
 
Sijui ni mm nimeruka sehemu moja au vipii nakumbuka niliishia wakina Miranda wanafatiliwa na gari ya vijana wa sheng
Labda hukufika mwisho, walifuatiliwa na wakawekwa kwenye 18, yakafanyika makubaliano ya uhai wa kina Miranda au kumtoa jona...walivyokubaliana safari ikaanza ya kwenda kumchukua jona, waliyofika getini ndio ilipoanzia......hakuna kilichorukwa shunie
 
Stive sakata la Mariam VP, Au wale Jamaa wa Chugga kule wameona hawana cha kupoteza kwake, Ama tusubilie Jona apone ndo atukumbushe ya mariam ?
 
Labda hukufika mwisho, walifuatiliwa na wakawekwa kwenye 18, yakafanyika makubaliano ya uhai wa kina Miranda au kumtoa jona...walivyokubaliana safari ikaanza ya kwenda kumchukua jona, waliyofika getini ndio ilipoanzia......hakuna kilichorukwa shunie
Niliruka mama hiyo episode
 
*ANGA LA WASHENZI II -- 36*

*Simulizi za series*


ILIPOISHIA

Sheng akamuuliza ni kipi ambacho hana na hali jeshi zima alimkabidhi? Shao akasema bado havitoshi, anahitaji 'access' ya maabara kwa muda wowote ule.

Hapa kidogo Sheng akasita.

ENDELEA

Akamtazama Shao kwa jicho la shaka na kumuuliza kwanini anataka hilo aliloomba. Shao akamjibu kwa ufupi, amwamini. Sheng akafikiri kidogo kisha akapandisha kichwa chake juu kama ishara ya kuafiki, basi Shao akatia sahihi katika hati ile na kisha akamrudishia Sheng kisha akaaga na kwenda zake.

Sheng akabaki akifikiri. Hata naye Shao akaenda akifikiri. Alikwazwa na kile kitu. Alifika kwenye makazi yake na kuketi akiwaza haswa. Baada ya muda kidogo akaita vijana wake kumi na kuwaeleza kile kilichotukia.

Akawaonya na kuwasisitiza ya kwamba sasa misheni ya kumkamata na kumuua Jona si tu ni kazi bali utetezi wa uhai wao. Wafanye kila wakijuacho kuhakikisha wanamtia mkononi.

Na zaidi akawaambia ana mpango. Ila atawashirikisha muda si mrefu baada ya kukutana na mtu mmoja nyeti kabla siku hiyo haijaisha. Kwa hivyo, akawaambia wale vijakazi wakutane nae majira ya saa nne usiku palepale walipokutania.

Agizo hilo likapita, watu wakatawanyika. Kwenye majira ya saa mbili usiku, mwanamke mmoja aliyevalia baibui, akaja kwenye makazi ya Shao. Aligonga mlango mara mbili, Shao aliyekuwepo ndani akatazama saa yake ya mkononi, akagundua ndiye mgeni anayemngojea, akatabasamu akinyanyuka. Akauendea mlango na kufungua.

Alikuwa ni Sasha! Mwanamke huyo akazama ndani na muda si mrefu maongezi ya kiini yakachukua nafasi. Lengo kuu la Shao kumwita hapo mwanamke huyo ni kuwa anaamini kwa namna moja ama nyingine, wakina BC wanaweza wakawa wanahusika na tukio la kukombolewa kwa Jona.

Japo hakuwa na uhakika, aliona jambo hilo sio la kulipuuzia. Na sasa alikuwa anataka mrejesho wa Sasha amefikia wapi kuomba 'access' ya kuzama ndani ya kundi hilo akitumia mgongo wa dada yake, Sarah.

Sasha akanywa maji kwanza kupoza koo kisha akamwambia Shao kuwa kazi haikuwa nyepesi hata kidogo. Na kwa namna moja, wakuu wa kitengo hicho wanaonekana kutingwa na kazi kiasi kwamba maombi hayo yamewekwa kwenye mangojeo.

Hapa Shao akazidi kuamini aidha 'kazi' hizo ambazo zimewatinga zinaweza zikawa zinamhusu Jona. Akang'ata lips zake akitafakari.

Akanyanyua glasi yake ya kinywaji akanywa mafundo mawili alafu akakuna kidevu chake cheupe.

Akamwambia Sasha hawana muda wa kupoteza. Inabidi jambo lifanyike kuhakikisha makazi ya watu hao wanaowashuku yanapelelezwa kama yamemuhifadhi Jona. Na kazi hiyo ataifanya yeye, Sasha, kwani atakuwa ana ufahamu wa maeneo hayo.

Hata alipojitetea hayafahamu, Shao hakumwelewa. Akamsisitizia amtumie dada yake, Sarah, kuyafahamu na kisha afanye kazi hiyo ndani ya siku mbili tu!

Punde atakapofahamu kuwa Jona amelazwa miongoni mwa majengo hayo, atoe taarifa na wao watalifanyia kazi mara moja!

Sasha hakukaa, akaenda zake.

**

Usiku wa saa nne ...

Simu iliita, ila Sarah alihofia kuipokea. Alikuwa kitandani pamoja na Kinoo, na ni dada yake ndiye aliyekuwa anapiga.

Akamtazama Kinoo, hakuwa anatikisika. Alimpatia mgongo akitazama ukutani. Ila naye hakuwa amelala. Na alisikia simu hiyo ikiita. Lakini hakusema wala kufanya kitu.

Sarah akakata simu. Kisha akatulia kwanza asiseme jambo kwa kama dakika mbili akisikilizia pengine Kinoo atafanya jambo. Hakufanya!

Basi akafungua simu yake na kwenda moja kwa moja upande wa ujumbe. Akaandika kwa haraka akitumia vidole vyake vyepesi kumwonya Sasha asimpigie muda huo kwani yupo na Kinoo.

Kisha akatuma tena ujumbe wa pili kumuuliza anataka nini usiku wote huo?

Akangoja kwa sekunde tano ujumbe kuingia. Sasha akianzia mbali kwa kumuuliza nini kinakawiza zoezi lao la kuungwa kundini. Je watu wao wametingwa na kazi gani?

Sarah akasonya, kisha kwa pupa akabofya kioo cha simu kumwambia dadaye mbona hilo alishamwambia kuwa hajui, na Kinoo amekuwa mgumu kujipambanua?

Sasa Sasha akaenda kwenye lengo lake, akamwomba dada yake amweleze makazi ya watu wanaohusika na Kinoo. Sarah akamwambia kuhusu Miranda tu, maana ndipo anapopafahamu. Kisha asipoteze muda akamuaga dada yake na kuzima simu kabisa.

Akalala baada ya kuchoma dakika kadhaa akiwaza nini Sasha amepanga kufanya. Akapotelea kabisa usingizini.

Ila Kinoo bado alikuwa macho! Alivuta tena dakika kadhaa alafu akavuta simu ya Sarah na kuiwasha. Akatia nywila na kubonyeza OK. Simu ikakataa kufunguka.

Akajaribu tena kuweka nywila, akabonyeza OK, majibu yaleyale, simu imegoma! Kumbe Sarah alibadilisha nywila ya simu yake. Kinoo akalalama. Akairejesha simu alipoikuta kisha akaendelea kuwaza.

Ni nini mwanamke huyu alikuwa anafanya nyuma ya mgongo wake? Tena yeye na dada yake?

Haki alipata shaka. Na aliona alichukulie hatua hilo.

Ila atawahi kabla ya madhara kutokea? Hili ni la mimi na wewe kujiuliza.

**

Saa moja kasoro asubuhi...

Baada ya kupata kifungua kinywa, Lee alienda kukutana na Nieng, Shifoo Nieng, aliyekuwa ametulia ndani ya bustani aki-meditate kama afanyavyo kila siku kuanzia majira ya saa kumi na moja alfajiri.

Alipofika hapo, akatulia na kungoja. Alishaambiwa zoezi hilo la Nieng huwa linakoma saa moja kamili hivyo alijua hatakaa hapo kwa muda mrefu kungoja.

Hakukosea, muda si mrefu akaungana na Nieng ambaye alimtaka waende kufanyia maongezi yao ndani. Ofisi yake ilikuwa imekaa mbele ya dojo, ndani hakukuwa na kiti wala meza, bali mito midogo chini ambayo ndiyo hutumika kama kiti.

Wakaketi humo katika mtindo wakaao wanafunzi wa sanaa ya mapambano ndani ya dojo kisha maongezi yakachukua nafasi. Nieng akaanza kwa kumuuliza Lee kwanini alimuua Chong Pyong.

Lee akaeleza kila kitu. Hakuhusika na kumuua Chong Pyong. Amesingiziwa tu akiwa katika harakati za kumtafuta Chen Zi.

Nieng akastaajabu kusikia Chen Zi. Akamuuliza Lee ana mahusiano gani na Chen Zi? Lee akalaghai kuwa ni rafiki. Alihofia kusema kuhusu nyaraka ile aliyokuja kuitafuta.

Basi Nieng akamwambia Lee kuwa Chen Zi aliuawa na familia ya Li. Wala hakuwa amezidisha madawa kama inavyosemekana. Na sababu kubwa iliyopelekea Chen Zi kuuawa ni kuhisiwa ana mahusiano na Wu family.

Nieng akaenda mbali akamwambia Lee kuwa kuna mengi sana yanatukia ndani ya China, watu kuuawa na wengine kupotea. Familia ya Li imekuwa yenye nguvu mno hapa karibuni, na kama wasipofanya jitihada basi wataifutilia mbali kabisa familia ya Wu.

Mpaka hivyo wanapoongea, tayari wameshapokonywa jiji la Hongkong. Na hata Shanghai imekuwa matatani. Haitachukua pia muda mrefu kuwa chini ya Li, kama vile Beijing.

Ajabu ni kwamba, japo familia ya Wu inaungwa mkono na serikali, bado tu Li wanawasumbua. Inasadikika kuna baadhi ya vibaraka ndani ya serikali, na wao wamekuwa wakitoa taarifa zote kwa Li family.

Sasa kuwadhibiti inabidi liwe kipaumbele chao kikubwa. Kuna baadhi ya viongozi inabidi wauawe, kuna baadhi ya watu inabidi wapotezwe.

Japo wanawajua watu hao, bado kazi imekuwa ngumu! Ila Nieng akaendelea kwa kusema sasa amepata matumaini. Anaamini Lee atakuwa mwarobaini wa tatizo hilo.

Anaamini kwenye uwezo wake, atamkabidhi jeshi na orodha ya watu wa kuwamaliza.

Kwa Lee halikuwa gumu hilo. Akaliafiki. Ila shida kidogo ilikuja pale alipoambiwa mtu wa kwanza wa kummaliza.

Alikuwa ni makamu wa raisi!

***
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…