Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

Stive kweli unatuwekea burudani hii bila malipo yeyote,tunashukuru sana kwa hilo.
Ila kukaa kimya hivyo bila kutujulisha nini kinaendelea ni kutokujali hisia zetu. Hebu pita humu japo usalimie tu
 
Kama vp aseme kama kaisitisha sio kukaa kimya
Sjui anajiskia raha sana anavyoona tunateseka kwa ajili ya hadith yako
Hii sio poa
 
*ANGA LA WASHENZI II -- 51*

*Simulizi za series*


ILIPOISHIA

Akatazama, hola! Patupu!

Akahisi miguu imemwishia nguvu. Akahisi mwili umekuwa wa baridi kama barafu. Akahisi haja zote kwa mpigo!

Bam! Bam! Bam! Mlango ukabamizwa tena na tena.

ENDELEA

Akajikakamua na kuuendea. Alipofungua akakutana na mwanadada Miranda. Moyo wake ukapiga fundo kubwa, ila akajitahidi kubana hisia.

"Miranda!" akaigiza kutahamaki. "mbona bila taarifa mama?"

Miranda hakujibu. Akazama ndani na kwenda kuketi kitini. Akakunja nne.

"Habari yako?"

"Salama," akajibu Miranda na kisha akauliza, "vipi wewe?"

"Mimi niko poa tu," akasema Kinoo. Ila kiuhalisia hakuwa salama. Hata uso wake ulimsaliti. Alijawa na hofu. Na kwa namna fulani alikuwa anasutwa roho.

Akajichekesha.

"karibu bana. Naona Leo umeamua kun'tembelea!"

"Kinoo," Miranda akait kisha akamtazama mwanaum hiyo machoni na kumuuliza, "mkeo yupo wapi?"

Kinoo akatazama kando na kando kisha akasema, "sijui ameenda wapi. Ametoka kidogo."

"Una uhakika?"

"yah! Hayupo ndani. Vipi kwani kuna shida yoyote?"

"Hamna shida kwangu. Ila shida ipo kwako."

"shida gani?"

Miranda hakusema kitu. Akabaki akimtazama Kinoo kwa sekunde kadhaa. Akatazama chini na kisha akashusha pumzi ndefu.

"Kinoo," akauvunja ukimya kwa kuita. "Kama isingalikuwa wewe ni jamaa yangu niliyetoka nawe mbali, hata sasa ningekuwa nishakumaliza. Sijui ni nini kimekukalia kichwani mpaka ukadiriki kututoa sadaka kiasi hiki."

Kinoo akakunja sura kwa mkanganyiko.

"Sijakuelewa. Ni nini unamaanisha?"

"Unajua kila ninachokisema hapa, Kinoo. Wewe si mgeni hata kidogo. Unajua ulichokitenda na kama nakusingizia, nitazame unambie haujui."

Kinoo akatazama chini.

Kukawa kimya kwa sekunde kadhaa.

"Ni yule mwanamke, sio?" Miranda akauliza. Kabla hajapewa jibu, akaendelea kunena, "tangu alipoingia mwenye maisha yako nilijua vitu havitakuwa kama vilivyokuwa hapo awali. Nilifahamu fika, na ndiyo maana hata kukushirikisha tena kwenye mambo yangu nilisitisha."

Akanyamaza. Kinoo bado alikuwa anatazama chini.

"sasa yupo wapi hiyo mwanamke? unajua hata alipo hivi sasa? ila mimi nipo hapa. Nipo hapa kama nilivyokuwapo tangu nyuma. Je kama ningaliuawa, nani angalikuwa nawe hapa?"

Kinoo hakusema kitu. Ila macho yake yalianza kuwa mekundu.

"Hata pesa si hajakuachia?" Miranda akaendelea kunena. "Amekuacha kama alivyokukuta ... Nimeshangaa sana ni kwa namna gani alivyokufanya mjinga. Ulikuwaje mjinga kiasi hiki ndugu?"

Kimya. Miranda akasimama.

"Nakutakia maisha mema," akasema na kwendaze kuelekea mlango, ila Kinoo akamdaka mkono na kumsihi akae. Sasa macho yake yalikuwa mekundu zaidi.

"Miranda," akaita. "Nisamehe sana. Nastahili kuadhibiwa vikali. Siku zote umekuwa mkarimu na kama dada kwangu ila nikachagua kukuangamiza. Nimekabwa na hayà, hata uwepo wangu ni unafki mtupu.

Tafadhali, naomba uniangamize. Nami nimeridhia kwa hali zote."

"Sina haja ya kukuua, Kinoo," Miranda akajisemea. "Nina damu nyingi za kuziangamiza ila yako si mojawapo. Niliona tu tuachane kwa amani. Kila mtu akawa na maisha yake. Inatosha."

Ila Kinoo bado hakuwa radhi kumruhusu Miranda aende zake. Akiwa amemng'ang'ania mkono akamsisitiza amsamehe. Na yupo tayari kufanya lolote lile kama nauli ya msamaha wake."

Baada ya hiyo kauli, Miranda akaketi na kusema,

"Kuna kazi ya kufanya. Upo tayari?"

**

Saa nane mchana ...

"Kwahiyo una mpango gani na hiyo mimba?" Aliuliza Sasha kisha akapooza koo lake na kinywaji kikali.

Walikuwa wameketi sebuleni. Nyumba hii ni kubwa na ya kupendeza. Samani zake pia ni za gharama kubwa.

"Sijui nafanyaje!" Akasema Sarah. Alikuwa amejilaza kiuchovu kochini. "Siwezi kusema niitoe. Ni kubwa sasa. Ni hatari!"

Sasha akanyamaza kwanza. Akajinywea mafundo mawili kisha akasema, "kwahiyo utaubeba huo mzigo mpaka lini?"

Sarah akabinua mdomo. "Mpaka pale nitakapoutua. Hamna namna."

"You are not serious!" Sasha akang'aka. "Alafu huyo mtoto unakuja kumwambia baba yake nani?"

"Amekufa."

Sasha akacheka.

"Anyway, inabidi ufanye namna. Mimi sijaona haja ya kubeba mzigo huo. Na kuhusu ukubwa wa mimba, sio shida. Madaktari wapo, wazuri tu ninaowaamini. Nakupa muda wa kufikiri, utanambia. Sawa?"

Sarah hakujibu. Alitazama zake kando. Sasha akanywa mafundo kadhaa na kumaliza chupa yake, ndipo Sarah akanena, "kwahiyo itakuwaje kuhusu Kinoo?"

"Itakuwaje?" Sasha akatahamaki. "Itakuwaje nini? Haitakuwa kitu."

"Kwahiyo atabaki hai?"

"Aaahm yah! Atabaki hai ndio. Ila kwa muda."

"Unamaanisha nini kwa muda?"

Sasha akanyamaza kana kwamba hakusikia. Sarah akarudia kuuliza, "una maanisha nini? Mtamuua?"

"Bado unampenda? Mbona unajali sana?"

Sarah hakujibu. Macho yaliyomtazama dada yake yalionyesha anataka majibu na si maswali.

"Ana nafasi moja tu ya kujitetea. Kama asipotoa taarifa yenye kuzaa matunda hivi sasa, nadhani Sheng atamuangamiza."

"Ila taarifa anazotoa ni sahihi!" Sarah akang'aka.

"Sijakataa. Ila hazizai matunda. Na Sheng anawaza kuwa huenda akitoa taarifa huwapasha pia na wenzake!"

"Hapana. Hafanyi hivyo!"

"Sijabisha, Sarah. Ila ndivyo ambavyo nimekwambia kuhusu Sheng."

Kukawa kimya kidogo.


"Ole wako umwambie Kinoo haya n'lokwambia," Sasha akatahadhari.

**

Saa nne usiku ...

"Una uhakika?" Aliuliza Sheng akiongea na simu.

"Ndio, nina uhakika. Na mara hii sitataka pesa yako mpaka pale utakapohakikisha maneno yangu."


"Sawa. Tutawasiliana." Sheng akakata simu.

Baada ya kama lisaa limoja akawa na wajakazi wake kumi na mbili. Wakajiweka kwenye chombo cha usafiri na kwenda zao.

Wakanyookea eneo fulani mbele ya hoteli. Tutaita eneo hili hoteli ila haikuwa na hadhi hiyo, ila ilizidi hadhi ya guest house au lodge.

Hapo baada ya kukaa ndani ya gari kwa muda kidogo, wakatoka wanaume wanne na kuzama ndani ya hoteli.

Punde kidogo sauti za bunduki zikavuma! Wanaume wengine watatu wakatoka garini na kuzama ndani. Milio mingine ikavuma. Kisha kukawa kimya.

Sasa kwenye gari wakawa wamebakia wajakazi watatu tu pamoja na Sheng. Hawakuwa wanaelewa nini kinaendelea ndani. Na Sheng, kwa kuhisi kuna jambo halipo sawa, akawazuia watumishi wake wasiende tena ndani.

Wakangoja hapo kwa muda kidogo. Lakini katika hali ya ajabu, mara hoteli nzima ikazima taa na kuwa kiza!

Na mwanga uliporejea, Sheng akashuhudia watu wakiwa wamesimama mbele ya gari! Na watu hao walikuwa wamebebelea bunduki kubwa mikononi mwao, wakiwanyooshea!

"Shuka upesi garini!" Amri ikasikika. Sheng akatazamana na watumishi wake. Hakuwa tayari kutii amri ya yeyote. Basi wale wafanyakazi, katika namna ya kipekee, wakamziba Sheng, kisha mwanaume huyo wa kichina, akasukuma gia na kukanyaga mafuta kwa pupa!

Gari likamchupa kuwafuata wale watu waliowanyooshea bunduki. Na kabla watu wale hawajanusuru roho zao, wakagongwa na kusinywa!

Sheng akaangua kicheko. Na kama haitoshi, akarudisha tena gari na kuwasinya tena aliowagonga.

Kisha akashuka na kuwatazama. Usoni mwake alikuwa na tabasamu.

"Hakuna mtu wa kupambana na ..." kabla hajamalizia kauli yake hiyo, akakaukiwa na maneno ghafla baada ya kugundua aliowaua ni miongoni mwa wafanyakazi wake.

Lakini iliwezekanaje hili?

Hakujua kumbe wafanyakazi wake hao walikuwa wametolewa mhanga. Viunoni walikuwa wamefungiwa mabomu na hata bunduki walizokuwa wamebebelea hazikuwa na risasi hata moja.

Kabla hajafanya jambo, akashangaa kuona alama ya kitaa chekundu cha bunduki kikiwa kifuani mwake. Na kisha akaamriwa na mtu ambaye hakumwona,

"Weka mikono yako juu!"

***
 
*ANGA LA WASHENZI II -- 52*

*Simulizi za series*



ILIPOISHIA

Kabla hajafanya jambo, akashangaa kuona alama ya kitaa chekundu cha bunduki kikiwa kifuani mwake. Na kisha akaamriwa na mtu ambaye hakumwona,

"Weka mikono yako juu!"

ENDELEA

Haraka akaweka mikono yake juu kutii amri.

Dakika ... watu wakamveka kinyago cheusi akawa gizani. Akapakizwa ndani ya gari ambalo hakulifahamu, safari ikaanza kwenda mahali ambapo hapafahamu.

Kama mwendo wa lisaa limoja. Akashushwa ndani ya eneo fulani hivi, kiwanda ambacho kimetekelezwa. Akaingizwa ndani ya chumba fulani na kuvuliwa kinyago.

Hakuwa anaona kitu maana kulikuwa ni giza totoro. Dirisha moja lililo juu kabisa halikutosha kuingiza mwanga kabisa ndani kwahiyo watu hawaonani.

Baada ya kutupiwa humo, mlango ukafungwa na kukawa kimya kwa kama dakika tatu, hakuna kinachofanyika.

Baadae kidogo, Bwana Sheng anasikika akijikusanya na anajinyanyua. Anaangaza huku na kule kisha anapaza sauti kuita,

"Heeeey!" Kimya. Ni mwagwi tu wa sauti ndiyo ulimjibu. Akarudia kuita na kuita, ila ni bure. Hakukuwa na kitu. Na hata alidhani hakuna mtu anayemsikiliza.

Akanyamaza. Ila baada ya kama dakika mbili hivi, mlango ukafunguliwa. Vikasikika vitu fulani vikidondoka kang!-kang! Na kisha mlango ukafungwa.

Sheng akaita, hakuna aliyemjibu wala kuhangaika naye. Punde baada ya muda hewa ikaanza kuwa nzito. Akawa anahangaika kuhema.

Hakuchukua muda mrefu, akajihisi mdhaifu na hatimaye akapoteza fahamu.

Kama vile watu wale waliotupia vile vitu ndani walikuwa wanahesabu muda kwani punde walikuja kufungua mlango na nyuso zao zilikuwa zimefunikwa na vinyago vya kuzuia gesi.

Wakamtazama bwana Sheng wakitumia kurunzi. Wakamwona amelala hajiwezi. Wakatazamana na kutikisiana vichwa. Wakamjongea, na kumnyanyua.

Wakatoka naye ndani wakielekea kusikojulikana.

**

Beijing, mishale ya saa tano asubuhi ...

Baada ya kufanya kazi yake vema, kumaliza wale wote waliopo orodhani, sasa Lee alikuwa ndani ya jiji la Beijing kwa dhumuni la kuonana na afisa fulani wa serikali kwa ajili ya kujadili vitu kadhaa.

Mezani alikuwa ameweka glasi yenye mvinyo. Ila hakuwa anahangaika nayo sana, bali simu yake ambayo alikuwa anaandika text na kutuma.

Anapokea na kutuma. Baada ya muda kidogo, simu yake ikazima charge. Akalaani. Akaiweka simu yake mezani na sasa akahamishia mawazo yake kwenye glasi yake ya mvinyo.

Akanywa mafundo matatu alafu akatazama nje ya kioo. Huko nje watu walikuwa bize kila mtu akihangaika na yake. Watu walikuwa wanapita huku na kule. Kila mmoja na yake.

Hapa bwana Lee akapata wazo. Alimwona mzee fulani akikatiza akiwa amebeba briefcase mkononi. Akaitazama briefcase yake na kuinyakua kuiweka mezani.

Akafungua na humo ndani akatoa diary fulani ambayo alilenga asome kusogezea muda. Diary hii ilikuwa ni ile ambayo aliitwaa toka kwa makamu wa raisi aliyemmaliza kule nchini Mongolia.

Aliperuzi diary hiyo kwa muda kidogo. Kuna kitu kikavutia macho yake. Akatazama kwa umakini, ila kabla hajakata kiu chake, akahisi kiganja begani mwake. Kugeuka akakutana uso kwa uso na afisa yule aliyekuwa anamngojea.

Afisa huyo akatabasamu pasipo kusema kitu. Akampatia Lee ishara ya kichwa kisha akatangulia kwenda zake. Lee akalipia kinywaji chake kisha akamfuata afisa huyo.

Mpaka nje kulikuwa kuna gari limesimama, Lee akajiweka na safari ikang'oa nanga.

Ila afisa yule alikuwa mtu mkimya sana. Gari lilitembea kwa takribani robo saa na hakutia neno lolote.

Alikuwa anatazama nje ya gari na alionekana mtu aliyetingwa na mawazo kiasi. Lee alimtazama afisa huyu, na hakuona kama kuna haja ya yeye kusumbuana naye.

Akatulia tuli akiangaza huko nje. Ila baada ya muda kidogo afisa huyo akamwongelesha akitaka kumjua Lee kwa undani.

Lee hakujiweka wazi sana. Hakuona sababu ya yeye kufanya hivyo, basi akawa anamjibu afisa huyu kwa ufupi tu.

Afisa huyu kama mtu aliyegundua hilo, akaacha kusumbuana na Lee. Akanyamaza kama alivyofanya hapo awali. Safari ikaendelea.

Baada ya kama dakika ishirini, wakiwa wameacha jiji la Beijing kwa kiasi kidogo, gari ikasimama na kujiegesha pembeni. Kisha dereva pasipo kupewa maelezo yoyote, akaizima gari na kutulia tuli.

Yule afisa akafungua briefcase yake na kutoa karatasi kadhaa. Akamkabidhi Lee pasipo kusema jambo.

Naye Lee akatoa karatasi kadhaa kwenye briefcase yake na kumpatia afisa huyo kisha wakapeana mkono.

Ila kabla Lee hajatoka ndani ya gari hilo, afisa huyu alipomaliza kukagua karatasi alizopewa kwa haraka, akamsihi Lee kwa maneno machache sana. Awe makini.

Kabla Lee hajatia neno, mlango wa upande wake ukafunguka. Akaenda nje na gari la afisa likatimka akilishuhudia.

Akatazama mwanzo na mwisho wa barabara. Kulikuwa kuna safari ndefu ya kuelekea jijini Beijing. Hakika alihitaji usafiri.

Ila kwanini afisa yule alimtupia mbali huko? Aliwaza. Alikokotoa kichwani akajikuta akiamini pengine ni sababu za kiusalama.

Angalau mawazo hayo yakampa unafuu. Ila akawaza tena, kama ni sababu za usalama, je ni sahihi kwake kutelekezwa eneo kama hilo akiwa na nyaraka muhimu na nyeti hivyo?

Aliendelea kuwaza akijongea. Alitembea kwa mwendo wa dakika kumi, na mara ghafla akasikia sauti ya breki kali! Akashtuka na kutazama kando yake. Akaona gari aina ya Ford ranger nyeusi. Ilikuwa imeshusha vioo na ndani yake walikuwa wanaume kadhaa.

Kabla hajawajua wanaume hao ni wakina nani, wapo wangapi, akastaajabu wakitoa mitutu ya bunduki na kumwonyeshea.

Wakamimina risasi kadhaa. Zikatoboa na kujeruhi mwili wa Lee vibaya! Akadondoka chini kama mzigo asiyeonyesha dalili za uhai.

Wanaume wawili wakashuka toka kwenye lile gari, wakampoka Lee briefcase yake na kisha wakatimka zao kwa kasi wakirudi kule walipotokea, yaani kule mbali na jiji.

Baada ya muda asioujua. Akiwa gizani, Lee anasikia sauti za watu. Anakakamaa na kufungua kope za macho yake. Anamwona mwanamke mmoja na wanaume wawili. Anataka kusimama, anashindwa.

Watu wale wakamtaka atulie kwani amejeruhiwa vibaya. Akajitazama, tumbo lake lilikuwa limejawa damu. Alihisi maumivu makali sana.

Hakudumu tena muda mrefu, akapoteza fahamu.

**


Saa nne usiku, nchini ...

Mlango ulifunguliwa, Bwana Sheng akaingizwa ndani ya chumba chake akiwa hajiwezi kwa lolote. Alibwagwa chini na kisha mlango ukafungwa.

Watu hawa waliomleta walikuwa ni wanaume wawili waliovalia suti nyeusi na vinyago usoni. Vinyago vya kuzuia gesi yenye sumu hivyo nyuso zao hazikuwa zinaonekana haswa ni wakina nani.

Walikuwa wanatembea kwa ukakamavu. Miili mirefu na yenye nguvu.

Baada ya kuufunga mlango waliondoka zao wakielekea upande wa kulia wa mahali alipohifadhiwa bwana Sheng. Baada ya mwendo wa dakika tano, wakavua vile vinyago vyao na punde wakawa wametoka ndani ya eneo hili.

Huko nje napo palikuwa kiza, hivyo hawakuonekana vema watu hawa. Walijipaki kwenye gari, cadillac nyeusi, wakatimka.

Kule chumbani, kizani, baada ya dakika tatu tangu gari lile litimke, Bwana Sheng alianza kugugumia. Na mara akakohoa kama mara sita kabla ya kunyamaza na eneo zima likawa kimya kana kwamba ni chini ya shimo.

Akataka kuita, ila akashindwa. Kifua kilikuwa kinambana haswa. Akaishia kuvuta kamasi.

***
 
Tangu mara ya kwanza naweka simulizi hapa nilifahamu fika ni kama vile nimejishtaki kwa kila kiumbe kutoa.maoni yake kwa namna ajisikiavyo. Na hata mara nyingine mtu asijali ama akisahau kwamba nawe ni binadamu na unapitia.matatizo vilevile kama wao.

Nilitoa tahadhari bayana kuwa simulizi hii huandikwa na kutumwa, si kwamba imerekodiwa tayari. Na pia hapa juzi nikaweka wazi ya kwamba nilipotewa na simu yangu niliyokuwa naitumia kuandikia. Hata hivyo, baada ya kupata hii simu mpya, ambayo kiuhalisia nilipewa tu na mmoja wa simulizi zangu, simu hii imekuwa ikinipa matatizo haswa.

Si tu kwamba sijaizoea, bali pia uwezo wake ni hafifu hivyo hunichukua muda sana kuandika na hata kuingia mitandaoni. Napata taabu.

Sikuwapo humu mtandaoni kwa muda, nadhani ni stara tukaangalia last seen ya mtu kabla hatujatoa hukumu. Niwatazame mkihangaika, au nifanye kusudi kwa mali yani? Kufaidika nani? Sina haja ya michezo hiyo ya kijita kujitia upumbavu.


Na sipati kirutubisho chochote kumtesa mja wa mtu. Tuulizane wajama na huo ndiyo utu.

Mbali na hapo, sitafuta kauli yangu, nitamaliza nilichokianzisha. Haijalishi.kwa kina gani cha bahari. Au.kwa ncha gani za milima.

Nashukuru maana hamjachoka.na mimi. Mungu akijaalia ntajisogeza tena kesho tuendelee. Samahani kuwakwaza ila sijadhamiria hata lepe.
 
Dah ngoja niiache hii story naona arosto had hamu inaishaa, jaman siku ikiisha mnitag plzz[emoji26]
 
Dah ngoja niiache hii story naona arosto had hamu inaishaa, jaman siku ikiisha mnitag plzz[emoji26]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…