Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

Baba, moja hata hilo gazeti la lete raha sikuwahi.kulisoma. hivyo silijui. Pili, simuliz hii inaendana na taarifa ya habari ya mambo yanayotokea kila siku ama kudhaniwa kutokea. Kama unasoma utakuwa unaelewa vema. Sasa ikawaje kufanana na matukio ya simulizi zilizopita? Moja, meli ya kichina, uwekezaji wa kichina nchini na vita baridi, yenye.moto ndani yake, kati ya bloku ya kijamaa na kibepari.

Yalikuwapo kweye lete raha? Enjoy simulizi mzee. Hata mm ninayeongea na kuituma hapa, sijui inaishije na wala huko mbele ipoje maana ninaandika na kuituma papo hapo.
Mkuu sio kwamba Na crash riwaya hii! Hapana!!! For sure nimewah kusoma ctor hizi hapo zamani kidogo! Ndo nashangaa huu mfanano!! Je!? Ni developing story au Ni mfanano wa mawazo ya watunzi? But all in all story inasisimua Na I appreciate the thought your share to us! My brother
 
Shime wasomaji wa riwaya tufanye harambee ili mambo yawe motooo
 
*ANGA LA WASHENZI II -- 54*

*Simulizi za series*


ILIPOISHIA

“Kuna haja ya kuhofia kuhusu hilo?” Jona akauliza.

“Ipo!” Miranda akajibu akimtazama. “Jona, watu hawa ni wachawi.”

“Wachawi? - Kivipi? Unamaanisha nini?”

ENDELEA

Miranda akanyamaza kwanza. Foleni likaruhusiwa kwendaze, basi akatia gari moto wakaendelea na safari. Baada ya kutembea kwa dakika tatu, bado akionekana mtu anayebughudhiwa na mawazo, akasema:

“Kuna kipindi Mr Brown alinieleza kidogo juu ya watu hawa. Tulikuwa tunaongelea mambo yetu tukiwa tumetoka kufanya kazi fulani hivi kubwa. Siku hiyo nilimfurahisha sana kwa utendaji wangu wa kazi, akaniambia kama nikiendelea hivyo hivyo, basi siku moja angalinipeleka Uingereza.

Huko nitapata mafunzo zaidi na kama nikifuzu basi nitakuwa HS, yaani Headquarter Servant. Nitapata kila ninachokitaka, na nitafanya kazi mataifa mbalimbali kutimiza adhma ya kundi.

Sikuweza kumuuliza sana kwani alikuwa amelewa, na hata yale maongezi yake kwa namna moja ama nyingine nilidhani yanachochewa na pombe, hivyo sikuzingatia sana. Lakini kwa sasa naona yalikuwa na mantiki ndani yake.

Na zile simulizi alizokuwa ananipa, hazikuwa za uongo wala kutiwa chumvi. Alikuwa anasema ukweli.”

“Ni simulizi gani hizo alikuwa anakupa?” Jona akataka kujua.

“Alikuwa anaongea kwa kujivuna na kucheka mara kwa mara. Ni wazi alikuwa anapendezwa na simulizi hizo. Alijipambanua akinieleza ni namna gani vijana hao wamekuwa wakifanya kazi kwa ufanisi, na hata akan’tolea mifano kedekede ya watu mashuhuri na maarufu waliouawa na hao watu mpaka sasa hakuna aliyekamatwa.

Anyways, sitamaliza kama tukiongelea haya. Ila yatupasa kuwa makini sana.”

Baada ya lisaa limoja na nusu, wakawa wamewasili kwenye nyumba fulani yenye ghorofa moja. Wakazama ndani na walipoketi wakajihudumia glasi glasi za juisi na maongezi yakaendelea.

“As long as hawa watu hawaonekani ku-pose threat, Inabidi tungoje kwanza ni kitu gani kundi la Sheng litafanya,” alisema Jona alipoweka glasi mezani. “Hatua yao ndiyo itatupa mwanga sisi tufanye nini.”

Marwa akaguna na kisha akatia neno, “Mimi kuna kitu nahisi. Kwa akili yangu yote na kwa moyo wangu wote, siamini kama watu hawa, kama Miranda alivyowaongelea, watahusika na Sheng pekee kisha wakajiondokea zao. Nahisi mbali na hili la Sheng, kuna la ziada.

Na hapo ndipo ndipo utata utakapotokea.”

Jona akabinua mdomo, “Inawezekana unalolinena ni kweli. Si la kulipuuza hata kidogo. Kama kuna uwezekano, inabidi kufuatilia nyendo zao hatua kwa hatua.”

**

Saa nane usiku …

“Tunaenda siku nyingine sasa, naona kuna haja ya kuchukua hatua,” alisema jamaa mmoja mweusi. Macho yake yalikuwa yanamtazama mwanaume wa kichina aliyekuwa ameketi kwenye kiti kirefui akinywa whiskey.

Mwanaume huyu wa kichina alikuwa ndiye yule aliyekuwa akiwasimamia wakina Marwa walipokuwa kwenye kitengo cha SPACE BUTTON. Sasa ndiye yeye amekuwa mkuu baada ya Sheng kutoonekana.

Alikunywa tena fundo moja la whiskey kisha akamtazama mwanaume huyo aliyempa taarifa, akamwambia kwa sauti yake nyembamba yenye lafudhi ya ki-mandarin,

“That’s none of your business. Najua cha kufanya na ni kwa muda gani nifanye. So can you please get away from my face?”

Mwanaume yule aliyemfikishia taarifa akageuka aende zake, ila huyu bwana wa kichina akamwita na kumwambia,

“Ole wako ufanye kitu ambacho sijakwambia,” alisema akiwa anarembua kilevi. “Nitakuambia nini cha kufanya. Usidhani mimi ni chizi, I am not crazy. I am not craaazy, ok?”

Mwanaume yule mweusi akaenda zake akimwacha huyu bwana wa kichina hapa anaendelea kunywa. Baada ya kama dakika tano, bwana huyu akamalizia kinywaji chake, akanyanyuka na kujikokota kwenda ndani.

Alipofika akajitupia kitandani akitabasamu. Akatazama simu yake. Akabofyabofya kutazama akaunti yake ya benki, mara punde ujumbe ukaingia kumwambia ana shilingi milioni mia nane taslimu. Akatabasamu na kukumbatia simu yake.

Alikuwa ana furaha sana. Huu ulikuwa ni muda wake. Na akiwa anaamini kabisa kuwa bwana Sheng hatarudi akiwa hai, basi aliazimia kujiweka sawa kabla mambo hayajarudi kwenye mstari.

Simu ikaita.

Akaitazama akikunja sura. Akajiuliza kwa sekunde kadhaa kisha akapokea na kuiweka sikioni. Alikuwa ni wakala toka makao makuu, Hong Kong, China.. Na alibashiri bwana huyo atakuwa amempigia kumuuliza kuhusu Sheng.

Maongezi yao yakadumu kwa muda wa dakika kumi. Na kama alivyobashiri, mada ilikuwa Sheng kwani hajatuma mrejesho wa maendeleo kwa muda wa ‘masiku’ sasa. Na bwana huyo akaenda mbele kwa kuuliza sababu zinazomfanya bwana Sheng kutokuwapo eneo la kazi kwa siku zote hizo.

Kumbe walishatazama kwenye ‘tracing’ zao wakabaini kwa siku zote hizo ambazo bwana Sheng hajawasilisha mrejesho wa kazi, hakuwapo eneo la kazi.

Basi kwa maswali hayo, huyu bwana wa kichina akashindwa kuficha. Ikabidi sasa aweke bayana kuwa Sheng hayupo eneo la kazi, na hawafahamu wapi alipo.

Basi haikuwa taabu, bwana yule aliyewapigia simu akasema anatuma taarifa za location aliyopo Sheng, na kufikia kesho majira kama hayo apewe ‘feedback’.

“https://jamii.app/JFUserGuide!” Bwana huyu wa kichina akalaani. Sasa mipango yake ilikuwa imeharibika. Usiku wake uligeuka kuwa wa maruwani ghafla na hata pombe zilizokuwa zimemwingia kichwani, zikapotea!

Akabaki akiwaza nini cha kufanya.


**

Saa nne na robo asubuhi …

“He is weak enough!” aliongea mwanaume wa kizungu, mmoja wa kundi la ‘intellect instinct’ akiwa ndani ya eneo lile la kiwanda kilichotelekezwa.

Mwanaume huyu alikuwa ametoka ndani ya chumba kile walichomhifadhi bwana Sheng. Na hapa akiwa anaongea alikuwa ametia mkono wake wa kuume mfukoni, yu ndani ya suti nyeusi matata.

“We have already done each and everything. It’s just a matter of time for us to interrogate and kill him … we need at least eight final hours ... ok. I’ll be in touch.”

Bwana huyo akakata simu, akageuka arejee kule chumbani, ila alipopiga hatua nne, akasikia kama sauti ya mlio wa gari. Haraka akasimama na kutulia tuli kuhakikisha kama alichokisikia ni kweli.

Hakusikia tena sauti yoyote, ila akawa tayari ana shaka. Badala ya kwenda kule chumbani akatembea kwa ustadi kwenda nje ya kiwanda. Alipofika mlangoni, akajibana mahali na kutazama nje.

Hakuona kitu.

Ila akiwa amejiweka kwenye mazingira ya utulivu mkubwa, masikio yake yakampa taarifa kuwa kuna jambo halipo sawa. Akanyanyua mkono wake wa kuume na kuongea kwenye saa yake kwa sauti ya chini,

“Alert.”

Kisha akachomoa bunduki yake ndogo na kuikamata vema mkononi. Baada ya kama dakika mbili za utulivu, akasikia sauti ya kitu cha chuma kikidondoka chini. Sauti ilitokea upande wake wa kushoto.


**

“Umeona kitu?” aliuliza mwanaume mmoja rangi maji ya kunde. Hawa walikuwa ni wafuasi wa bwana Sheng. Kwa idadi wanaume watano wakiwa wamekuja hapa kumkomboa mkuu wao.

“Hamna kitu,” mwenzake akamjibu.

Basi wakasonga tena wakiwa wananyata. Wakasonga na kusonga, na baada ya dakika kama sita, wakawa wamefika kwenye mlango wa chumba ambacho amehifadhiwa bwana Sheng.

Na kwa muda wote huo hawakuwa wamemwona mtu yeyote yule. Kitu pekee walichokiona ilikuwa ni gari aina ya cadillac nyeusi ikiwa imeegeshwa kwa nje ya kiwanda hiki.

Basi wakafungua mlango, haukuwa umebanwa na komeo wala loki, wakazama ndani na kumwona Sheng akiwa amejilaza chini hajielewi. Ni pumzi tu ndiyo huashiria kuwa yu hai.

Wakambeba na kuanza kujongea kwenda nje. Wanaume wawili walifanya hivyo, na wengine watatu wakiwa wanawalinda wenzao wakitazama huku na huko kwa tahadhari kubwa. Mikono yao iliyobebelea bunduki ikienda kushoto na kulia, juu na chini.

Wakafanikiwa kutoka nje pasipo mushkeli. Wakasonga zaidi kulifuata gari lao, ila ajabu hawakulikuta. Pale walipoliacha hakukuwa na alama yoyote ile ya gari.

Na hata lile cadillac nyeusi waliyoiona wakati wanakuja, nayo haikuwapo. Wakatazamana kwa bumbuwazi.

Wakatazama huku na kule, hakukuwa na kitu mbali na kiwanda kilichochoka na kufubaa. Mazingira yalikuwa kimya mno. Majani na matawi ya miti yaliyumbishwa na upepo, kisha yakatulia.


***
 
Back
Top Bottom