Mkuu asante sana kwa kipaji hiki ulichokionyesha, wengi humu hatuwezi ni wasomaji tu, maana kukaa siku nzima unawaandika watu waje wasome kwa muda wa nusu saa tu then wanalalamika mbona cha leo "kifupi steve"? si mchezo! nami nina yangu machache
Utanisamehe najua watu wataanza "ooh! si uandike ya kwako"
Ni vizuri kuelimishana kwa uono wangu!
Sheng vs Lee na kampuni yao!
Hapa tangu awali ungemtengeneza sheng tu, ndio mbaya na anaingiza biashara haramu kwenye hiyo kampuni yao tofauti na malengo ya kampuni hiyo, ambayo ingekuwa ni kusimamia maslahi ya biashara za China
Na Lee yeye anapigania maslahi ya china tu, na alikuwa hapendi vile sheng alivyokuwa anawapelekesha watu na kuwaua ovyo
Sababu ya picha kuchorwa, na ufafanuzi wa codes
Miranda vs Kinoo
Miranda na kinoo walikuwa kundi la BC ambalo nalo lilikuwa na biashara chafu, ingawa alipokufa BC na kundi ndio likasarambatika, wakabaki wazungu wenzake tu. wakawa hawana chao, lakini walikuwa na siri nzito.
Kinoo hatujajua hata alipopotelea.
Jona vs Jeshi la polisi vs Makomandoo
Jona ndio sterling, lakini ajawahi kufikia cheo cha komandoo au labda ungemfanya yeye ni Jasusi, kwani inspekta wa polisi ni mtu mdogo hawezi kumzidi mbinu komandoo hata robo, sasa hata pale makomandoo wanaposhindwa maarifa na Jona inspekta wa polisi ni kulidhalilisha jeshi,
Wale makomandoo kumi walioenda kisiwani kuifuatilia ndege sikutegemea wao uwape hadhi ya chini kabisa kiteknolojia kiasi kwamba redio zao zile za "ovaa" "ovaaa" nimekupata ovaaaa, wakati wenzao wamevaa vya masikioni otherwise wasomaji wako wasiwe wajeda umewadhalilisha
Bahada ya kuwa tayari washaupata mwili wa rais, nilitegemea wao ndio wangetoa mawasiliano na huku makao makuu na kuaambia kilichojili, pia wanaenda kupambana na hao maharamia Uingereza, pasipo kufa kikondoo kwa kutegeshewa mvinyo hotelini.
Pia wangemsafisha Jona na wenzie, kuonyesha ni jinsi gani waliweza kupambana na maharamia wale na kuwaokoa hadi kulisambaratisha kundi ambalo hata waingereza walikuwa hawalitambui au kama walilitambua, basi liliwasumbua.
Jona heshima yake ingerudi ndani ya jeshi la polisi, sio kuishia kupewa pesa tu, zikiisha unakufa njaa vile vile.
Jeshi la polisi liliwekwa mfukoni mno! Pia halikuonyesha umuhimu uliomlazimisha Jona kurudi kazini.
Na vipi kuhusu tiba ya antidote? je! alipona au?
Sarah/Sasha
Hawa nao hatujajua wameishia wapi, licha ya kuwa Sarah alikuwa na ujauzito wa Kinoo, pamoja na kupata pesa nyingi pia, ingawa ndugu yake alimshauri aunyofoe
Mariam vs Nyoka na kundi lake
Mariam mpaka chezo linaisha bado ana siri kubwa juu ya biashara ya magendo ya marehemu mume wake, na pia maisha yake kwa jumla kwani ashakuwa teja!
Nyoka sidhani kama angeshindwa kumfuata mariam kwa shangazi yake kwenda kummaliza ilihali alikuwa anajua makazi ya shangazi yake huyo, kipande hiki pia mtunzi uliamua kukipotezea tu.
Yangu mawazo ni hayo tu, najua kuna mapungufu mengi lakini mtunzi anaweza kuyafanyia kazi next time
Hata hivyo natoa pongezi kubwa sana kwa mtunzi, kajitahidi mno akizingatia ushauri wa wadau wake atafika mbali kwakweli... kwani siku hadi siku amekuwa akiimprove zaidi na zaidi anzia Baradhuli mwenye mkono wa chuma, ile ya akina Amau Afrika magharibi ingawa hakuimalizia, na hii
Najua watu watakwazika kwa maoni yangu lakini si kwa nia mbaya nayaandika haya!
Haswa wale "Andika ya kwako na wewe tuone"