Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

Steve, hii story daah!! Fanya umalize hiko kitabu tununue, Maana hadi hasira ujue, unakatishwa Utamu alaf haujui Steve atatupia tena lini muendelezo!!! Hii ni inadhihirisha una uwezekano mkubwa Sana. Hadi wazee wa kimya kimya tunaanza kufunguka, hebu Tupe bei ya hiyo kitabu kama kipo, Hata kama ni ktk soft copy tutanunua tu.
 
Steve, hii story daah!! Fanya umalize hiko kitabu tununue, Maana hadi hasira ujue, unakatishwa Utamu alaf haujui Steve atatupia tena lini muendelezo!!! Hii ni inadhihirisha una uwezekano mkubwa Sana. Hadi wazee wa kimya kimya tunaanza kufunguka, hebu Tupe bei ya hiyo kitabu kama kipo, Hata kama ni ktk soft copy tutanunua tu.
 
Steve, hii story daah!! Fanya umalize hiko kitabu tununue, Maana hadi hasira ujue, unakatishwa Utamu alaf haujui Steve atatupia tena lini muendelezo!!! Hii ni inadhihirisha una uwezekano mkubwa Sana. Hadi wazee wa kimya kimya tunaanza kufunguka, hebu Tupe bei ya hiyo kitabu kama kipo, Hata kama ni ktk soft copy tutanunua tu.
naunga mkono hojaa
 
Duh!! Dadeki hii story nimeanza kuifuatilia mwezi wa 3 mwanzoni hadi saiv haijaisha tu,,,
Ifupishe bana iishe haraka maana inanifanya nimsahau hata wifi yenu.
Wifi yenu usiku ananigusagusa anataka mgegedo mi ananiona niko bize tu na simu angu nafuatilia hii story ***** hadi analia.
We steve wewe fanya kuimalizia bana wifi yako apate mgegedo.
 
Duh!! Dadeki hii story nimeanza kuifuatilia mwezi wa 3 mwanzoni hadi saiv haijaisha tu,,,
Ifupishe bana iishe haraka maana inanifanya nimsahau hata wifi yenu.
Wifi yenu usiku ananigusagusa anataka mgegedo mi ananiona niko bize tu na simu angu nafuatilia hii story ***** hadi analia.
We steve wewe fanya kuimalizia bana wifi yako apate mgegedo.
[emoji134] [emoji134] [emoji134] wifi yke shemeji yke
 
Steve, hii story daah!! Fanya umalize hiko kitabu tununue, Maana hadi hasira ujue, unakatishwa Utamu alaf haujui Steve atatupia tena lini muendelezo!!! Hii ni inadhihirisha una uwezekano mkubwa Sana. Hadi wazee wa kimya kimya tunaanza kufunguka, hebu Tupe bei ya hiyo kitabu kama kipo, Hata kama ni ktk soft copy tutanunua tu.
Naunga mkono hoja. Hata km ni soft copy tutanunua. Maana hata mimi nilikuwa nasoma kimya kimya lakini Duh!! Tunachoka kuisubiri
 
*ANGA LA WASHENZI II ---- 72*


*Simulizi za series*



ILIPOISHIA


Ila rubani huyu aliyejitambulisha kwa jina la Kassim Tolabora, alizungumza kutoa taarifa kwa lugha ya kiingereza pasipo kutia kiswahili kama ilivyozoeleka. Hili laweza likawa si tabu. Lakini lafudhi yake ilitia shaka. Ni wazi aliyekuwa anaongea hakuwa mswahili, alikuwa mzungu.


Hakukuwapo na hilo kwenye ratiba.


ENDELEA


Ndani ya ndege kulikuwa na Daktari na manesi kadhaa wa ziada kwa ajili ya kumhudumia Mheshimiwa akiwa anaenda kupata huduma zaidi. Lakini pia kulikuwa na maafisa usalama waliokuwa wanamsindikiza, wanaume nane kwa idadi. Walikuwa wamevalia kaunda suti rangi ya majivu.


Basi ndege ikaenda na kudumu kwa lisaa limoja hewani. Kasi yake ilikuwa kubwa ikikata pepo haswa. Watu waliokuwa ndani wakawa wanamtazama Raisi na taarifa yake ikitolewa kila muda, dakika na sekunde kuwa anaendeleaje. Huko aelekeapo pia wakapashwa taarifa kuwa anakuja mtu mkubwa kiasi hata maandalizi yalianza kufanyika.


Lakini pia wakati hayo yanaendelea, vyombo vya habari vya nje navyo vilianza kurusha habari juu ya kile kilichotokea Tanzania. Habari hii ilikuwa ya moto na ilivuta wasikilizaji na hata watazamaji wengi. Mpaka muda huo ambao Raisi alikuwa anasafirishwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, hakuna aliyekuwa amekamatwa kwa kuhusika na tukio hilo kubwa. Ilikuwa ni ajabu kwa namna yake.


Lakini pia swala hili likafukua makaburi, watu wa kawaida, wataalamu wa historia na hata wataalamu wa mambo ya siasa za Afrika wakaanza kulitafutia vyanzo kwa kutazama na kuchambua misimamo ya Raisi ambayo walikuwa wanadhani kwa namna moja ama nyingine ndiyo ambayo imemwadhibu.


BBC - Idhaa ya kiswahili majira ya saa nne usiku …


Mtangazaji, bwana Paul Chisanja, alikuwa beneti na Profesa Robert Waulaya wa chuo kikuu cha Mzumbe kuzungumzia jambo hilo. Kwa kujitanua na kutumia uhuru wao wa kujieleza, Profesa huyo akadadavua na kuhusisha jaribio hilo la kuuawa kwa Raisi na msimamo wake aliokuwa ameuweka kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika hivi karibuni kuwa ni muda sasa wa nchi za Afrika kuanza kukataa misaada toka nje kwani yawafanya watumwa.


Lakini akaenda mbele kwa kusema kuwa fukuto lililopo baina ya serikali ya saa na nchi za Magharibi huenda sasa ikawa sababu ya kutaka kumwondoa mwanaume huyo Ikulu.


Swala hili likapokelewa pia na vyombo kama vile CNN na Deutchvelle wakijaribu kuhoji na kuwahusisha watu kadhaa kwenye mahojiano hayo, ilimradi tu swala hili limetawala habari.


Basi ndivyo ilivyokuwa, wakati huo ndege ipo hewani kumsafirisha mkubwa wa nchi.


Ila huko Uingereza, Birmingham, kwenye ofisi kumi na mbili zilizopo nchi ya ardhi kulikuwa ni mahali ambapo pametingwa na shughuli nyomi. Ofisi hizi za siri ambazo zilikuwa zimewamudu watu takribani hamsini zilikuwa zimefumwa katika namna ya sayansi ya juu kabisa. Tarakilishi zilizokuwa zinatumika hapa zilikuwa ni nyepesi kwenye michakato lakini pia ziki-access hata mitandao ya kiza (dark web) ambazo hazikuwa zimezoeleka na watumiaji wa kawaida bali wahalifu.


Ndani ya ofisi hizi, mawasiliano yalikuwa kabambe na nadhifu. Huduma ndogondogo kama vile kuletewa chakula, maji, kahawa na hata ‘gluecose’ zilikuwa zinafanyika na roboti ndogo za matairi. Watu walikuwa ‘busy’ kuendesha na kusimamia mitambo.


Taarifa zilikuwa zinatolewa hapa kwenda pale katika vitengo tofauti tofauti ambavyo vyote vilikuwa vinasimamiwa na wanawake waliokuwa wamevalia suti na miguuni viatu vyeusi vya visigino virefu. Wanawake hawa vifuani mwao walikuwa na vibandiko vya vioo vilivyokuwa vimeandikwa majina yao.


Haya majina hayakuwa ya kawaida kama ujuavyo, lah! Yalikuwa yameandikwa kufuatia silaha. Mmoja, aliitwa Dagger, mwingine bullet, mwingine bomb, mwingine swords, mwingine arrow na kadhalika na kadhalika. Kwa idadi vitengo vilikuwa kumi, hivyo na wanawake kumi juu yao.


Juu ya wanawake hao kulikuwa kuna mwanaume mmoja, mkuu wa kila jambo, ama tumwite mkurugenzi mtendaji. Yeye ofisi yake ilikuwa pweke kwa juu kidogo ya hizi zingine. Ndani ya ofisi yake, kulikuwa na kiti kirefu na meza ya kioo basi. Kwa macho ya kawaida ungesema ofisi hii ina uhaba wa vitu ukilinganisha na ukubwa wake.


Ila ungekuwa umekosea haswa. Ndani ya ofisi hii kulikuwa na vitu lukuki ila vikiwa vimehifadhiwa kwa teknolojia ya juu. Kuta za ofisi hii zilikuwa zinabiduka na kuleta kinachoagizwa baada ya kubofya button ambazo zimejaa mezani.


Bwana huyu mkubwa aliyekuwepo hapa, hakuwa na jina kamili. Na kama vile wale wanawake ambao wapo kule chini wakisimamia vitengo mbalimbali, jina lake lilikuwa la ajabu kwenye kibandiko kinachoning’inia upande wake wa kuume wa kifua.


Kibandiko chake kilikuwa kirefu na maandishi yake rangi ya dhahabu kikisomeka ‘all of them’, kwa kifupi mabanoni A.OT. Kumaanisha kwamba yeye alikuwa ni mjumuiko wa vile vyote ambavyo wasimamizi wake walikuwa, yaani dagger, swords, bullet, arrow na kadhalika.


Mwanaume huyu wa kizungu ambaye amejawa na ndevu lukuki kwenye taya zake, alikuwa amevalia suti nyeusi, amejilaza kwenye kiti chake na miguu yake mifupi ameilaza mezani, nyayo zikifunikwa na viatu vya Italia (Italian shoes).


Alikuwa ‘amerelax’. uso wake haukuonyesha shaka. Masikioni alikuwa ana ‘earphone’ na kinywani ana ‘bubblegum’ anayoitafuna kwa kubadilisha pande za meno. Alikuwa mtulivu haswa.


Ila punde akanyanyua mkono wa kushoto na kutazama saa yake ya mkononi. Kuna kitu alikuwa anatarajia. Punde mlango wake ulifunguliwa akaingia mwanamke mwenye kibandiko kisomekacho ‘Sword’, alitembea kwa madaha na kukomea mbele ya mkuu wake. Akamwambia,


“They are on air with the President.”


Mwanaume yule akatulia kana kwamba hajasikia. Alitafuna bubblegum yake mara tatu alafu akauliza, “So?”


“They will finish their task,” akajibu mwanamke yule mleta habari. Mkuu akatafuna kwanza kama mara nne kisha akasema, “They better do that.”


Basi mwanamke yule aliyeleta habari akashika hatamu kwenda zake, ila kabla hajafika mlanggoni mkuu akasema, “Make sure you are on touch.”


“We are!” mwanamke akajibu na kwenda zake.



***



“Make sure he doesn’t survive. That’s your order,” sauti ya kike ilisikika kwenye earphone kubwa za rubani mkuu, mwanaume mzungu aliyevalia sare za rubani. Naye mwanaume huyo hakuwa mwingine bali Bwana Denmark, na kando yake, alikuwa rubani wa pili msaidizi, naye si mwingine bali bwana Wales.


Ilikuwa ni ajabu kwa wao kuwapo hapa. Hakuna aliyekuwa anadhania kuwa watuhumiwa wa jaribio la mauaji ya Raisi ndiyo haohao waliopewa dhamana ya kumpeleka mtu huyo nje ya nchi kwa matibabu.


Kiuhalisia hakuna aliyepanga wala kuyajua haya, hata wale waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hawakujua liendealo. Wanaume hawa, Denmark na Wales, walikuwa wamewavamia marubani na kuwamaliza muda mfupi kabla ya Raisi kupakiwa na safari kuanza.


Maiti za marubani halisia waliotakiwa kupaisha ndege hii zilikuwa zimeachwa kulekule kwenye uwanja wa ndege. Hakuna aliyekuwa amelijua hilo mpaka sasa.


“Let’s do it,” akasema Denmark akimtazama Wales. Wanaume hawa walikuwa wamekwishaandaa parachuti kwa ajili ya kutokomea wakishamaliza kazi yao. Basi walipoweka mitambo sawa, wakatoka ndani ya chumba cha marubani na kuelekea kule upande wa raia kukutana na wana usalama lakini pia Raisi wammalize kabisa.


Mikononi walikuwa wameshikilia bunduki ndogo kwa ajili ya kurahisha kazi. Hawakupanga kutoana jasho, ni tendo na kuhepa tu.


Basi baada ya kutoka kwenye eneo lao la kazi, tendo ambalo lilichukua sekunde nne tu, uso kwa uso wakakutana na kitu ambacho hawakukitarajia kabisa. Hii ilikuwa ni ‘surprise’ ambayo iliwaacha midomo wazi na kuwafanya watazamane.


Uso kwa uso walikutana na Jona, Lee na Miranda wakiwa wameketi. Watu hao walikuwa wamebebelea bunduki mikononi mwao. Na kwenye viti vingine, maafisa usalama wote, nane kwa idadi, walikuwa wamelala hawajielewi hata chembe.


Ilibidi Denmark na mwezake wapite kwenye bonde hilo la umauti kwenda kumkuta Raisi kwenye chumba chake maalumu. Humo alipofungiwa yeye na wahudumu.


Basi ghafla, risasi zikaanza kutupwa. Watu hawa wakarushiana risasi kwa fujo sana. Na kwa kuona kuwa ilikuwa ngumu kukabiliana na hali ya hapa, basi bwana Denmark na Wales wakarudi upesi kwenye chumba cha rubani na kujifungia humo.


Wakapasua mitambo yote mezani kwa rubani kwa kutumia risasi na sasa ndege ikaanza kwenda kombo. Wakati huo mlango wa chumba hicho ulikuwa unabamizwa kwanguvu, Jona na wenzake wakitaka kuzama humo.


Ilikuwa ni fujo kubwa! Jona na wenzake walishindwa kubomoa mlango kwa kukosa nafasi kwani ndege sasa ilikuwa inayumbayumba hovyo kana kwamba mtu aliyevamiwa na maruwani. Walitupiwa huku na kule, hata silaha zao hazikubakia mikononi!


Basi kwa wakati huo huo, wakina Denmark wakatumia mlango mdogo wa dharura uliokuwapo upande wa rubani, wakachoropoka toka kwenye ndege baada ya kupambana na pepo kali mno. Sasa wakawaacha wakina Jona wakipambana kwenye ndege inayoenda kuanguka.




***
 
Steve, hii story daah!! Fanya umalize hiko kitabu tununue, Maana hadi hasira ujue, unakatishwa Utamu alaf haujui Steve atatupia tena lini muendelezo!!! Hii ni inadhihirisha una uwezekano mkubwa Sana. Hadi wazee wa kimya kimya tunaanza kufunguka, hebu Tupe bei ya hiyo kitabu kama kipo, Hata kama ni ktk soft copy tutanunua tu.
Mkuu, shida ni kwamba hii simulizi naiandika na kuituma papo hapo, alafu kwa sasa nitawaibia pesa zenu kwasababu inaelekea mwishoni. Najitahidi kutuma kila siku, hata hapa kesho na keshokutwa nitajitahidi kuandika na kuituma mapema, kama pia ikiwezekana mara mbili.
 
Back
Top Bottom