Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,076
Tulimsikia Mheshimiwa Rais Magufuli akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini
Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.
Hata hivyo kimya kizito huko angani namna kulivyokuwa kweupe, ndiko kulikonifanya nilazimike kuandika "thread" hii.
Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??
Ni jambo la wazi kuwa hayo mashirika ya ndege yamesikia tamko hilo la Rais, ila kama tujuavyo hayo mashirika ya ndege yanafanya biashara, huwezi kurusha ndege ya Boeing yenye kuchukua abiria zaidi ya 300, ukiwa umebeba abiria 5 kuja nchini, hakika safari hiyo hailipi, kwa maana nyingine utasitisha safari za namna hiyo.
Ukweli ni lazima tumwambie Mheshimiwa Rais kuwa zile propaganda zinazoiendesha nchi kwa hivi sasa haziwezi kufanya kazi huko kwenye anga ya kimataifa
Hivi unadhani mtalii gani toka kwenye nchi yoyote atakuja Tanzania kwa hivi sasa, nchi ambayo "imegoma" kutoa takwimu za ugonjwa wa Corona kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa??
Hivi Rais wetu anadhani kuwa dunia anaweza kuihadaa kirahisi rahisi, kama ambavyo anaweza kutuhadaa watanzania??
Tumemsikia wenyewe Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt Hamisi Kigwangala, akionyesha kukatishwa tamaa na sekta ya utalii inavyoenda kwa hivi sasa!
Nashauri kama Taifa tuwe wasema kweli kwa mambo mbalimbali, ndipo tutapoaminika huko duniani
Kwa mwenendo huu tunaokwenda nao hivi sasa ya kila kitu tunapenda kupiga "fix" ndiko huku tulikolifikisha Taifa letu kwa hivi sasa