Anga zimefunguliwa, lakini wenye ndege zao wamegoma kuzileta nchini!

Anga zimefunguliwa, lakini wenye ndege zao wamegoma kuzileta nchini!

Punguzeni kuwadanganya watu sasa kwa kujitapa
hata ktka maisha yakawaida linapokuja suala la uchumi ni vita, yaani wewe kuupata mkate wako wa kila siku lazima upigane coz kuna watu hawatataka upate mkate wako, vivo hivo hata uchumi wa kitaifa na kimataifa hivo usiwe mjinga wakufikiria
 
Tulimsikia Mheshimiwa Rais akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini

Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.

Hata hivyo kimya kizito huko angani namna kulivyokuwa kweupe, ndiko kulikonifanya nilazimike kiandika "thread" hii.

Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??

Ni jambo la wazi kuwa hayo mashirika ya ndege yamesikia tamko hilo la Rais, ila kama tujuavyo hayo mashirika ya ndege yanafanya biashara, huwezi kurusha ndege ya Boeing yenye kuchukua abiria zaidi ya 300, ukiwa umebeba abiria 5 kuja nchini, hakika safari hiyo hailipi, kwa maana nyingine utasitisha safari za namna hiyo.

Ukweli ni lazima tumwambie Mheshimiwa Rais kuwa zile propaganda zinazoiendesha nchi kwa hivi sasa haziwezi kufanya kazi huko kwenye anga ya kimataifa

Hivi unadhani mtalii gani toka kwenye nchi yoyote atakuja Tanzania kwa hivi sasa, nchi ambayo "imegoma" kutoa takwimu za ugonjwa wa corona kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa??

Hivi Rais wetu anadhani kuwa dunia anaweza kuihadaa kirahisi rahisi, kama ambavyo anaweza kutuhadaa watanzania??

Tumemsikia wenyewe Waziri wa Mali asili na utalii, Dkt Hamisi Kigwangala, akionyesha kukatishwa tamaa na sekta ya utalii inavyoenda kwa hivi sasa!

Nashauri kama Taifa tuwe wasema kweli kwa mambo mbalimbali, ndipo tutapoaminika huko duniani

Kwa mwenendo huu tunaokwenda nao hivi sasa ya kila kitu tunapenda kupiga "fix" ndiko huku tulikolifikisha Taifa letu kwa hivi sasa
Ndege haziwezi kuja sababu hakuna abiria,Hali ya dunia itaanza kutengemaa angalau kuanzia January 2021 sababu wengi bado wanahofu.Na hii si Tz peker dunia nzima sekta ya usafiri wa anga bado
 
Ndege haziwezi kuja sababu hakuna abiria,Hali ya dunia itaanza kutengemaa angalau kuanzia January 2021 sababu wengi bado wanahofu.Na hii si Tz peker dunia nzima sekta ya usafiri wa anga bado
Bana likasi
Sasa ni kwanini Prezidaaa wetu katupiga "fix" kuwa ndege za kimataifa ziko fully booked hadi mwezi wa 8 kuwaleta watalii nchini kwetu??
 
Huko duniani nawashangaa hawajamsikia mukulu?? au sauti haitoshi tuongeze volume??

Baniani mbaya kiatu chake dawa, hapo hapo majukwaani tunawaponda, ooh beberu, hapo hapo tunawataka waje!

Everyday is Saturday.......................... 😎
Upungufu wa busara ndio tatizo.
 
Endeleeni kufurahia matatizo ya nchi yenu mlimo zaliwa.
Screenshot_20200608-094448_1.jpg


JamiiForums mobile app
 
Tena Qatar kwenye tangazo lao la kuaja Dar tarehe 16 June wameipamba nchi yetu kama kitovu(hub) ya utalii Afrika. Wanatupigia debe utalii kimtindo.
Qatar kuna baadhi ya siku ndani ya wiki uwa ana flight 3 kwa siku 1,kia,zenj na dar,ya dar nadhani ni daily,so anajua soko lake liko vipi kwa Tanzania
 
Hivi unajua KLM ilikuwa inakuja ila imeahirisha safari
Weka akiba ya maneno usije ukaumbuka siku chache zijazo.

Jana jioni nimekaa sehemu pembezoni mwa Morogoro Road nimeona Land Cruiser ya utalii imebeba watalii.

Ukienda kwenye ukurasa wa twitter wa Qartar Airways utaona tangazo kuanzia tarehe 16 June 2020 wanaanza safari za kuja Tanzania (jiji la Dar es Salaam).

Nenda pale airport ya JNIA kuna kampuni ya LSG Skychefs wameambiwa na kampuni flani kubwa ya ndege wataanza kuchukua huduma zao za inflight catering tarehe hizo nilizotaja hapo juu.

Nenda Zanzibar utaona pilikapilika zinazo endelea uwanja wao wa ndege wa kimataifa.
Qatar Airways announces resumption of flights to Tanzania
https://www.qatarairways.com/en-tz/homepage.html

Siasa zisizidi uwezo wetu wa kuchanganua mambo, kutafakari na kutafuta ukweli.
 
Tulimsikia Mheshimiwa Rais akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini

Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.

Hata hivyo kimya kizito huko angani namna kulivyokuwa kweupe, ndiko kulikonifanya nilazimike kiandika "thread" hii.

Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??

Ni jambo la wazi kuwa hayo mashirika ya ndege yamesikia tamko hilo la Rais, ila kama tujuavyo hayo mashirika ya ndege yanafanya biashara, huwezi kurusha ndege ya Boeing yenye kuchukua abiria zaidi ya 300, ukiwa umebeba abiria 5 kuja nchini, hakika safari hiyo hailipi, kwa maana nyingine utasitisha safari za namna hiyo.

Ukweli ni lazima tumwambie Mheshimiwa Rais kuwa zile propaganda zinazoiendesha nchi kwa hivi sasa haziwezi kufanya kazi huko kwenye anga ya kimataifa

Hivi unadhani mtalii gani toka kwenye nchi yoyote atakuja Tanzania kwa hivi sasa, nchi ambayo "imegoma" kutoa takwimu za ugonjwa wa Corona kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa??

Hivi Rais wetu anadhani kuwa dunia anaweza kuihadaa kirahisi rahisi, kama ambavyo anaweza kutuhadaa watanzania??

Tumemsikia wenyewe Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt Hamisi Kigwangala, akionyesha kukatishwa tamaa na sekta ya utalii inavyoenda kwa hivi sasa!

Nashauri kama Taifa tuwe wasema kweli kwa mambo mbalimbali, ndipo tutapoaminika huko duniani

Kwa mwenendo huu tunaokwenda nao hivi sasa ya kila kitu tunapenda kupiga "fix" ndiko huku tulikolifikisha Taifa letu kwa hivi sasa

Mkuu, anga likifunguliwa leo sio lazima ndege zianze kuingia kesho au hata ndani ya wiki tatu mbele. Safari za ndege zinapangwa kwa muda mrefu. Ilikuwa jambo jema kufungua anga mapema ili makampuni yapange safari za kuja wakati wowote wakipata abiria au mizigo. Kuhusu watalii, ni wazi kwamba itachukua muda mrefu kabla ya soko la utalii kurudi katika hali yake ya kawaida kutokana na uchumi kuyumba. Na hili si kwa Tanzania tu ni kwa dunia nzima. Si dhani kwamba kuna sababu ya kushangaa kuona watalii wachache wanaingia nchini kwa sasa.
 
Hivi unajua KLM ilikuwa inakuja ila imeahirisha safari
Watalii wao pia wana raha gani ya kula starehe na hali za uchumi zimetetereka jamani?
Mmh, hawahitaji kuona wanyama wengine, wanaye mnyama mpya CORONA, ngoja tuone kasi ya fully booked.....

Katika mazingira ya kawaida tunapaswa tutafute namna nyingine ya kujipromote na kupromote huu utalii, siyo kusimama majukwaani na kuwatusi hao hao watalii kuwa nchi zao beberu.

Onyesha wakishuka airport kuna kinga au hatua zipi za dhati zitazingatiwa kuhakikisha SOSHO DISTENSI, KONTAKT TRESING, HOSPITAL FACILITIES in case wakiugua, n.k.

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Back
Top Bottom