Anga zimefunguliwa, lakini wenye ndege zao wamegoma kuzileta nchini!

kwahio mnafurahia kwamba ndege hazitui
yani wewe nchi yako ikipata shida ni furaha kwako ,

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
Siyo tunafurahia........

Ila tunashangazwa na "fix" anazotupiga Prezidaa wetu, kwa kuwa alituhakikishia kuwa ndege za kuja nchini za kuwaleta watalii zote ziko "fully booked" hadi mwezi August mwaka huu!

Imenenwa kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu..........

Sasa kuna sababu zipi za kutuongopea wakati ukweli wenyewe unajulikana??
 
Tulimsikia Mheshimiwa Rais akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini

Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.
Hii hatari, maana yake hata Tundu AL tusimtegemee, hana ndege ya kumleta😀😀
 
Profesa majaja yuko bize anawapigia simu kuwabembeleza wakimuuliza tupe takwimu za korona anajikanyagakanyaga tu eti dawa nilioenda kuchukua madagascar imewatibu watz
 
Aliyeleta Uzi huu anaongea kiumbea umbea anazunguka zunguka! Sijui ana lengo gani! Ushauri; pendeni nchi yenu.
 
Weka akiba ya maneno usije ukaumbuka siku chache zijazo.

Jana jioni nimekaa sehemu pembezoni mwa Morogoro Road nimeona Land Cruiser ya utalii imebeba watalii.

Ukienda kwenye ukurasa wa twitter wa Qartar Airways utaona tangazo kuanzia tarehe 16 June 2020 wanaanza safari za kuja Tanzania (jiji la Dar es Salaam).

Nenda pale airport ya JNIA kuna kampuni ya LSG Skychefs wameambiwa na kampuni flani kubwa ya ndege wataanza kuchukua huduma zao za inflight catering tarehe hizo nilizotaja hapo juu.

Nenda Zanzibar utaona pilikapilika zinazo endelea uwanja wao wa ndege wa kimataifa.
Qatar Airways announces resumption of flights to Tanzania
https://www.qatarairways.com/en-tz/homepage.html

Siasa zisizidi uwezo wetu wa kuchanganua mambo, kutafakari na kutafuta ukweli.
Kweli kabisa.Na istoshe utalii umeathirika dunia nzima sio Tanzania tuu. Na watalii wakianza kuja wataanza kidogokidogo. Tuwe wazalendo tusishadadie na kufurahia eti watalii hawatakuja. Watalii watakuja tuu. Mi Kuna wamarekani nawafahamu wanakuja huku October, na walishakuja tour huku January. Wanakuja sababu walipapenda. Kumbukeni Tz tuna vivutio special watalii watakuja tuuu.
 
Bana likasi
Sasa ni kwanini Prezidaaa wetu katupiga "fix" kuwa ndege za kimataifa ziko fully booked hadi mwezi wa 8 kuwaleta watalii nchini kwetu??
Rais anapata habari za kuja watalii kutoka wapi? Kwa waziri? Hembu waulize wenye mahoteli makubwa ambayo kabla ya corona yalikua booked na baada ya corona watalii wameondoa booking zote! Waulize watalii wanakuja? Usidhani wanakuja kama wanaenda karikoo. Hata wenye vikampunk vidogo connection zap zinawaambia ishu zitakwenda sawa 2021. Sasa tunaleta siasa kwenye jambo la msingi inashangaza sana.
 
Watalii wao pia wana raha gani ya kula starehe na hali za uchumi zimetetereka jamani?
Mmh, hawahitaji kuona wanyama wengine, wanaye mnyama mpya CORONA, ngoja tuone kasi ya fully booked.....

Katika mazingira ya kawaida tunapaswa tutafute namna nyingine ya kujipromote na kupromote huu utalii, siyo kusimama majukwaani na kuwatusi hao hao watalii kuwa nchi zao beberu.

Onyesha wakishuka airport kuna kinga au hatua zipi za dhati zitazingatiwa kuhakikisha SOSHO DISTENSI, KONTAKT TRESING, HOSPITAL FACILITIES in case wakiugua, n.k.

Everyday is Saturday.......................... 😎
Hii point ifanyiwe na kazi na wizara husika.
 
Aliyeleta Uzi huu anaongea kiumbea umbea anazunguka zunguka! Sijui ana lengo gani! Ushauri; pendeni nchi yenu.
Majulao
Siyo nimeleta habari kiumbeya umbeya.......

Bali ninacho-argue ni kwanini mnapenda kutupiga "fix" watanzania??

Kama dunia nzima inajua kuwa hili janga halijaisha, kulikuwa na haja gani kwa Prezidaa wetu, kutupa "higher expectations" kuwa ndege zimekuwa over booked??
 
Tulimsikia Mheshimiwa Rais akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini

Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.

Hata hivyo kimya kizito huko angani namna kulivyokuwa kweupe, ndiko kulikonifanya nilazimike kiandika "thread" hii.

Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??

Ni jambo la wazi kuwa hayo mashirika ya ndege yamesikia tamko hilo la Rais, ila kama tujuavyo hayo mashirika ya ndege yanafanya biashara, huwezi kurusha ndege ya Boeing yenye kuchukua abiria zaidi ya 300, ukiwa umebeba abiria 5 kuja nchini, hakika safari hiyo hailipi, kwa maana nyingine utasitisha safari za namna hiyo.

Ukweli ni lazima tumwambie Mheshimiwa Rais kuwa zile propaganda zinazoiendesha nchi kwa hivi sasa haziwezi kufanya kazi huko kwenye anga ya kimataifa

Hivi unadhani mtalii gani toka kwenye nchi yoyote atakuja Tanzania kwa hivi sasa, nchi ambayo "imegoma" kutoa takwimu za ugonjwa wa Corona kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa??

Hivi Rais wetu anadhani kuwa dunia anaweza kuihadaa kirahisi rahisi, kama ambavyo anaweza kutuhadaa watanzania??

Tumemsikia wenyewe Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt Hamisi Kigwangala, akionyesha kukatishwa tamaa na sekta ya utalii inavyoenda kwa hivi sasa!

Nashauri kama Taifa tuwe wasema kweli kwa mambo mbalimbali, ndipo tutapoaminika huko duniani

Kwa mwenendo huu tunaokwenda nao hivi sasa ya kila kitu tunapenda kupiga "fix" ndiko huku tulikolifikisha Taifa letu kwa hivi sasa

Kwa nini isiwe kwamba ndege zimeshindwa kumiminika kwa sababu sehemu nyingi bado ziko kwenye lock-down? Kumbuka kuwa dunia nzima bado iko kwenye lockdown isipokuwa nchi nne tu ambazo ni THAILAND, SWEDEN, SOUTH KOREA na ya nne nimeisahau jina lake. Wenye mashirika yao wakishatoka kwenye lockdown, ndege zitamiminika
 
Mkuu ni ngumu kwa watalii kuja kwa sababu nchi nyingi raia zao wakitoka wanaporudi lazima wakae karantini kwanza ndo waendelee na mambo yao
Tulimsikia Mheshimiwa Rais akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini

Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.

Hata hivyo kimya kizito huko angani namna kulivyokuwa kweupe, ndiko kulikonifanya nilazimike kiandika "thread" hii.

Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??

Ni jambo la wazi kuwa hayo mashirika ya ndege yamesikia tamko hilo la Rais, ila kama tujuavyo hayo mashirika ya ndege yanafanya biashara, huwezi kurusha ndege ya Boeing yenye kuchukua abiria zaidi ya 300, ukiwa umebeba abiria 5 kuja nchini, hakika safari hiyo hailipi, kwa maana nyingine utasitisha safari za namna hiyo.

Ukweli ni lazima tumwambie Mheshimiwa Rais kuwa zile propaganda zinazoiendesha nchi kwa hivi sasa haziwezi kufanya kazi huko kwenye anga ya kimataifa

Hivi unadhani mtalii gani toka kwenye nchi yoyote atakuja Tanzania kwa hivi sasa, nchi ambayo "imegoma" kutoa takwimu za ugonjwa wa Corona kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa??

Hivi Rais wetu anadhani kuwa dunia anaweza kuihadaa kirahisi rahisi, kama ambavyo anaweza kutuhadaa watanzania??

Tumemsikia wenyewe Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt Hamisi Kigwangala, akionyesha kukatishwa tamaa na sekta ya utalii inavyoenda kwa hivi sasa!

Nashauri kama Taifa tuwe wasema kweli kwa mambo mbalimbali, ndipo tutapoaminika huko duniani

Kwa mwenendo huu tunaokwenda nao hivi sasa ya kila kitu tunapenda kupiga "fix" ndiko huku tulikolifikisha Taifa letu kwa hivi sasa
 
Hawa waliletwa na shirika gani la ndege, au walikodi ya kwao kuja kutalii?

Mnapofanya kampeni hizi zisizokuwa na uhalisi wa mambo, msidhani kwamba nyinyi peke yenu ndio mnaoitakia Tanzania mema, na hao wengine wanaoangalia mambo kwa uhalisia wake kuwa hawana mapenzi na nchi yao.

Kuweni wakweli, msitafute kuhadaa watu kwa mambo ambayo hayapo.
Unaongea mambo usiyoyajua kama vile una uhakika unayajua sababu unaendeshwa na hisia (emotions).

Mimi siyo mtumishi wa umma, siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa na sina chochote ninachopata kuipigia kampeni CCM, au chama chochote cha kisiasa.
Mh. Magufuli hanijui na wala jina langu halipo katika orodha ya wanaotegemewa majina yao kufikishwa mezani pake kwa uteuzi. Polepole, Makonda, Dr. Bashiru na CCM hawanijui labda kama wamenidukua tu.

Sina hasira za ukabila au mahaba ya ukabila, infact kiuhalisia sina kabila zaidi ya jina tu nikiulizwa ktk ofisi za umma kabila langu ndio nakumbuka mimi kabila gani. Sijui lugha yeyote ya asili, najuwa kiswahili, kiingereza, kifaransa kidogo na kispaniola kidogo sana.

Sijawahi kutumbuliwa wala kufilisiwa na serikali ya awamu yeyote hivyo sina chuki na yeyote, Sijawahi kufaidika moja kwa moja mimi binafsi na serikali ya awamu yeyote, sana sana nadaiwa mkopo wa elimu ya juu tu. Kwa namna hiyo nikichangia kitu akili yangu ipo huru sana sina upande zaidi ya upande wa ukweli na haki.

Dini najiita mkristo mkatoliki lakini sijaenda kanisani wala kutoa michango na zaka kwa miaka kadhaa. Na sasa nachukia sana mifumo ya kipigaji ya kimakanisa au uhuni wa makasisi. Sina mahaba ya udini au dhehebu la Mh. Magufuli kifupi nipo huru.

Back to the topic, hao watalii tusibishane kama upo Dar nenda mataa ya Kibo (Kibo Traffic lights) Morogoro road kuna kijiwe cha kahawa kwa Moud waulize hapo jana jioni tarehe 07 Juni 2020 mmeona gari yenye watalii inapita hapa?
 
Hawa waliletwa na shirika gani la ndege, au walikodi ya kwao kuja kutalii?

Mnapofanya kampeni hizi zisizokuwa na uhalisi wa mambo, msidhani kwamba nyinyi peke yenu ndio mnaoitakia Tanzania mema, na hao wengine wanaoangalia mambo kwa uhalisia wake kuwa hawana mapenzi na nchi yao.

Kuweni wakweli, msitafute kuhadaa watu kwa mambo ambayo hayapo.
Unaongea mambo usiyoyajua kama vile una uhakika unayajua sababu unaendeshwa na hisia (emotions).

Mimi siyo mtumishi wa umma, siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa na sina chochote ninachopata kuipigia kampeni CCM, au chama chochote cha kisiasa.
Mh. Magufuli hanijui na wala jina langu halipo katika orodha ya wanaotegemewa majina yao kufikishwa mezani pake kwa uteuzi. Polepole, Makonda, Dr. Bashiru na CCM hawanijui labda kama wamenidukua tu.

Sina hasira za ukabila au mahaba ya ukabila, infact kiuhalisia sina kabila zaidi ya jina tu nikiulizwa ktk ofisi za umma kabila langu ndio nakumbuka mimi kabila gani. Sijui lugha yeyote ya asili, najuwa kiswahili, kiingereza, kifaransa kidogo na kispaniola kidogo sana.

Sijawahi kutumbuliwa wala kufilisiwa na serikali ya awamu yeyote hivyo sina, sana sana nadaiwa mkopo wa elimu ya juu tu. Kwa namna hiyo nikichangia kitu akili yangu ipo huru sana sina upande zaidi ya upande wa ukweli na haki.

Hao wageni wameingiaje? mimi sijui hiyo siyo kazi yangu.

Jambo jingine lazima utambue kwamba kuna ndege za charter zimekuwa zikija na kutoka Tanzania siyo lazima wageni waje na schaduled flights. Mbona nimekutajia na kampuni zinazotoa huduma kwenye baadhi ya hizo ndege? Si ufanye kwenda kupeleleza kama kweli wamehudumia ndege yeyote hapo viwanjani.
 
Wacheni huo upuuzi
Kauli kali hii.
Sijapendezwa nayo, ongea hoja tu bila matusi tutaelimishana vizuri sana.
Hoja ikiwa nzito na ya kweli inaeleweka kirahisi mno, matusi na nguvu kubwa kupitia maneno makali ni dalil ya kukosa hoja.
 
Weka akiba ya maneno usije ukaumbuka siku chache zijazo.

Jana jioni nimekaa sehemu pembezoni mwa Morogoro Road nimeona Land Cruiser ya utalii imebeba watalii.

Ukienda kwenye ukurasa wa twitter wa Qartar Airways utaona tangazo kuanzia tarehe 16 June 2020 wanaanza safari za kuja Tanzania (jiji la Dar es Salaam).

Nenda pale airport ya JNIA kuna kampuni ya LSG Skychefs wameambiwa na kampuni flani kubwa ya ndege wataanza kuchukua huduma zao za inflight catering tarehe hizo nilizotaja hapo juu.

Nenda Zanzibar utaona pilikapilika zinazo endelea uwanja wao wa ndege wa kimataifa.
Qatar Airways announces resumption of flights to Tanzania
https://www.qatarairways.com/en-tz/homepage.html

Siasa zisizidi uwezo wetu wa kuchanganua mambo, kutafakari na kutafuta ukweli.
Hiyo Link ya Qatar Airways hakuna available flight to Tanzania tarehe 16 June
 
Tena alitangaza kwamba ziko 'fully booked' hadi Oktoba!

Hizi ndege zenye wasafiri wengi kiasi hiki ziko wapi, mbona haziji?

Hizi komedi za siku hizi hata kucheka inashindikana kwa wanaozisikiliza.
Watu wenye akili kama za Samaki Mfano wa Titicomb ndio hubebaga kila akisemacho Jiwe
 
Back
Top Bottom