Anga zimefunguliwa, lakini wenye ndege zao wamegoma kuzileta nchini!

Anga zimefunguliwa, lakini wenye ndege zao wamegoma kuzileta nchini!

Niko jirani na moja ya kampuni kubwa sana za utalii ambao wa system yao ilikua ni kupiga hela mwaka mzima wageni hawakati ila wanapunguaga tu na wengi wanakuja kwa ma group.

Mpaka leo hamna booking aina yeyote ile. Biashara hamna sasa hizo ndege sijui zmetua wapi ambako kakosekana hata mtalii mmoja wa kuja kupanda mlima na ile company!
 
Wangetakiwa waje na package imbayo inavutia watalii mfano Tunapackage ya kupunguza visingizio, hotel rates nk.Matangazo yatoke on how we will protect them hata tukiwambia Mungu anawalinda wanaweza kuja kufanya utalii wakuona hindi Mungu alivyotusaidia C19 ikaisha.
 
kwenye suala korona tuache mkuu.marekan wanaandamana hatujackia kifo cha korona hta kwa bahat mbaya..korona ni ugonjwa wa ku spread fear na ukiwa na fear ina attract ugonjwa galfa
 
Kwa jinsi ulivyo kuja na lugha za kashifa huku kukujibu tu nimekupendelea heshima kubwa mno ambayo hauku stahili.

Wewe mwenye akili nyingi unaelewa nini unaposikia 'kuanzia' au kiingereza 'starting from'?

Mimi nilifikiri wewe ni mtu wa kutumia mantiki (logic), sisi tuliosoma hisabati kuna hesabu za seti (set), hilo neno 'kuanzia' lina maana kubwa sana, limechukua eneo kubwa sana katika universal set. Nenda kajikumbushe hisabati za functions na mambo ya limits.

Kama ungekuwa unajua Hisabati, especially Logic uliyosema ungepitia kwanza hiyo link kabla ya ku share.
Hunijui, sikujui, ability ya Maths wanaijua wanaonifahamu, kwa akili yako hata hiyo user name hukupaswa kuitumia.
Kwa tunaojua Physics na Engineering Science tunaona aibu kuona such a user ID inaandika utumbo
 
kwenye suala korona tuache mkuu.marekan wanaandamana hatujackia kifo cha korona hta kwa bahat mbaya..korona ni ugonjwa wa ku spread fear na ukiwa na fear ina attract ugonjwa galfa
Marekani wanakufa kwa wingi ingawa sasa wewe unaangalia maandamano pekee
 
Back to the topic, hao watalii tusibishane kama upo Dar nenda mataa ya Kibo (Kibo Traffic lights) Morogoro road kuna kijiwe cha kahawa kwa Moud waulize hapo jana jioni tarehe 07 Juni 2020 mmeona gari yenye watalii inapita hapa?
Umejieleza vizuri kwa hayo uliyoandika huko juu, hata kama ukweli wenyewe ni wewe peke yako unayeujua.

Hii mistari ya mwisho ndio ukarudi kule kule nilikoku'quote', tena kwa kuvuruga zaidi.

Kwa hiyo tuchukulie huu ushuhuda ulioweka kwenye mistari hiyo kwamba ndio ushahidi wa mashirika kuleta ndege zao zikiwa zimejaa watalii Tanzania?
 
Watalii watajaa Tanzania wakiona kila Mtanzania anavaa barakoa kunawa mikono kupata vitakasa mikono
 
Balozi wa Marekani keshatia unoko kwa Matamko yake kila mara
 
Kila fursa inayopatikana tuitumie kutangaza utalii; mfano kama unao marafiki nje(mf ulaya,china,kwa Trump) tuwaeleze tuko njema. Ingawa hakuna takwimu za corona kwa muda,lakini hali haitishi kama inavyoripotiwa na mawakala wa mabeberu.
Tuipende taifa letu. Mwenyewe nimeanza kushawishi baadhi,ambao waliahirisha safari kati ya feb na March. Wamekubali kuja kuanzia june mwishoni.
Nashauri serikali iondoe tozo mbalimbali;watu wamepigika kiuchumi. Hata wenyewe wanshauri hivo
Haohao unaowashawishi welete fedha zao zikunufaishe ndio haohao unawaita mabeberu.
Yaleyale baniani mbaya..........
 
Usiongee usicho kijua.Airports nyingi ulimwenguni zinafunguliwa kwanzia katkat ya June mpaka August Aviation indusry itakuwa katka peak ulimwenguni.Nenda ICAO ukaone
 
Tulimsikia Mheshimiwa Rais Magufuli akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini

Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.

Hata hivyo kimya kizito huko angani namna kulivyokuwa kweupe, ndiko kulikonifanya nilazimike kiandika "thread" hii.

Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??

Ni jambo la wazi kuwa hayo mashirika ya ndege yamesikia tamko hilo la Rais, ila kama tujuavyo hayo mashirika ya ndege yanafanya biashara, huwezi kurusha ndege ya Boeing yenye kuchukua abiria zaidi ya 300, ukiwa umebeba abiria 5 kuja nchini, hakika safari hiyo hailipi, kwa maana nyingine utasitisha safari za namna hiyo.

Ukweli ni lazima tumwambie Mheshimiwa Rais kuwa zile propaganda zinazoiendesha nchi kwa hivi sasa haziwezi kufanya kazi huko kwenye anga ya kimataifa

Hivi unadhani mtalii gani toka kwenye nchi yoyote atakuja Tanzania kwa hivi sasa, nchi ambayo "imegoma" kutoa takwimu za ugonjwa wa Corona kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa??

Hivi Rais wetu anadhani kuwa dunia anaweza kuihadaa kirahisi rahisi, kama ambavyo anaweza kutuhadaa watanzania??

Tumemsikia wenyewe Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt Hamisi Kigwangala, akionyesha kukatishwa tamaa na sekta ya utalii inavyoenda kwa hivi sasa!

Nashauri kama Taifa tuwe wasema kweli kwa mambo mbalimbali, ndipo tutapoaminika huko duniani

Kwa mwenendo huu tunaokwenda nao hivi sasa ya kila kitu tunapenda kupiga "fix" ndiko huku tulikolifikisha Taifa letu kwa hivi sasa
Sasa wataanza kupangilia zile takwimu walizoficha na kuzitoa kidogo kidogo. Ukiwa na viongozi wasiofuata taratibu na kanuni ni shida sana.
 
Hao watalii wenyewe wamejifungia ndani watawezaje kuja nchini kutalii? tuhamasishane tu wapwa tukatalii wenyewe kwenye mbuga zetu
Hata fisi tu akionekana kwenye kichaka jirani hakuna mwenye interest ya kwenda kumuangalia sembuse kwenda huko kwenye mbuga za wanyama na ili iweje.
 
Mkuu, anga likifunguliwa leo sio lazima ndege zianze kuingia kesho au hata ndani ya wiki tatu mbele. Safari za ndege zinapangwa kwa muda mrefu. Ilikuwa jambo jema kufungua anga mapema ili makampuni yapange safari za kuja wakati wowote wakipata abiria au mizigo. Kuhusu watalii, ni wazi kwamba itachukua muda mrefu kabla ya soko la utalii kurudi katika hali yake ya kawaida kutokana na uchumi kuyumba. Na hili si kwa Tanzania tu ni kwa dunia nzima. Si dhani kwamba kuna sababu ya kushangaa kuona watalii wachache wanaingia nchini kwa sasa.

Inawezekana wewe ni mkweli kwa nafsi yako....

Lakini shida iko hapa;

Rais Joni Magufuli akiwa mafichoni Chato siku moja kabla ya kuanza safari kuja Dodoma kwa kauli kavu na macho mang'avu aliutangazia ulimwengu kuwa...

Mashirika mengi ya kimataifa ya ndege, yameshajaa "bookings" za abiria - watalii kuja Tanzania hadi mwezi August, 2020...!!

Kama ndivyo, shida iko wapi? Kwanini mambo yawe slow - slow wakati midege imeshajaa tayari? Yameshindwa kuruka kwa sbb mzigo wa abiria mzito sana?

Shida ni nini?.... Uongo tena kwa kiongozi mkubwa kama Rais, hauna tija na ni laana kabisa kwa taifa....!!
 
Unaongea mambo usiyoyajua kama vile una uhakika unayajua sababu unaendeshwa na hisia (emotions).

Mimi siyo mtumishi wa umma, siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa na sina chochote ninachopata kuipigia kampeni CCM, au chama chochote cha kisiasa.
Mh. Magufuli hanijui na wala jina langu halipo katika orodha ya wanaotegemewa majina yao kufikishwa mezani pake kwa uteuzi. Polepole, Makonda, Dr. Bashiru na CCM hawanijui labda kama wamenidukua tu.

Sina hasira za ukabila au mahaba ya ukabila, infact kiuhalisia sina kabila zaidi ya jina tu nikiulizwa ktk ofisi za umma kabila langu ndio nakumbuka mimi kabila gani. Sijui lugha yeyote ya asili, najuwa kiswahili, kiingereza, kifaransa kidogo na kispaniola kidogo sana.

Sijawahi kutumbuliwa wala kufilisiwa na serikali ya awamu yeyote hivyo sina chuki na yeyote, Sijawahi kufaidika moja kwa moja mimi binafsi na serikali ya awamu yeyote, sana sana nadaiwa mkopo wa elimu ya juu tu. Kwa namna hiyo nikichangia kitu akili yangu ipo huru sana sina upande zaidi ya upande wa ukweli na haki.

Dini najiita mkristo mkatoliki lakini sijaenda kanisani wala kutoa michango na zaka kwa miaka kadhaa. Na sasa nachukia sana mifumo ya kipigaji ya kimakanisa au uhuni wa makasisi. Sina mahaba ya udini au dhehebu la Mh. Magufuli kifupi nipo huru.

Back to the topic, hao watalii tusibishane kama upo Dar nenda mataa ya Kibo (Kibo Traffic lights) Morogoro road kuna kijiwe cha kahawa kwa Moud waulize hapo jana jioni tarehe 07 Juni 2020 mmeona gari yenye watalii inapita hapa?

Kwa hiyo kwa kuwa walikuwa kwenye " Land Cruiser" kama zile zinazobeba watalii na ni wazungu ukajua tayari ni wale mliopigwa "fix" na Mzee baba kuwa wamesha - book midege yote hadi mwezi August, 2020??

Umeulizwa swali simple sana, kuwa, hao walifika nchini na shirika gani la ndege maana anga ni tupu na JKNIA, KIA na Zanzibar Airports zote ni pakavu?

Cha ajabu badala ya kujibu maswali rahisi uliyoulizwa ukamua "off the road" na badala yake unaandika essay ndefu ku - display "ego" yako ya kujua kifaransa, kispanyola na sijui nini.....!!

Na eti ili mtu athibitishe kuwa ni watalii uliowaona, basi mtu huyo aende KIBO kwenye kijiwe cha Kahawa cha nani sijui.....!! Really? Really?

I am sorry. Pole sana....
 
Kitaturu
Hao watu wanajibaraguza tuu.......

Imenenwa kuwa ukweli utakuacha huru........

Sijui ni kwa manufaa ya nani kwa kiongozi mkuu wa nchi anapoamua kutupiga "fix" wananchi wake, kuwa ndege zote za kuja nchini ziko "fully booked" hadi mwezi wa 8 mwaka huu, wakati akijua wazi kuwa anatuongopea!
 
Kama ungekuwa unajua Hisabati, especially Logic uliyosema ungepitia kwanza hiyo link kabla ya ku share.
Hunijui, sikujui, ability ya Maths wanaijua wanaonifahamu, kwa akili yako hata hiyo user name hukupaswa kuitumia.
Kwa tunaojua Physics na Engineering Science tunaona aibu kuona such a user ID inaandika utumbo
Sawa umesikika maoni yako, kuna jingine?
Au bado unataka kuporomosha kashifa na matusi? Kama bado endelea hadi hasira zako ziishe uje tujadili vizuri.
 
Kama ungekuwa unajua Hisabati, especially Logic uliyosema ungepitia kwanza hiyo link kabla ya ku share.
Hunijui, sikujui, ability ya Maths wanaijua wanaonifahamu, kwa akili yako hata hiyo user name hukupaswa kuitumia.
Kwa tunaojua Physics na Engineering Science tunaona aibu kuona such a user ID inaandika utumbo
BTW, hii user name yangu kama unainasibisha na mtunzi wa kile kitabu cha Engineering Science basi umekosea. Yule anaitwa Titcomb siyo Titicomb kama ilivyo username yangu. Sijui huu umakini na akili unayojisifia vilikuwa wapi wakati unaandika hayo!!!

Mtaalamu wa hisababti anayeshindwa kuelewa maana ya 'kuanzia' unakaribishwa kwa mjadala wa hoja siyo matusi na mashambulizi binafsi.
 
Back
Top Bottom