Hao watalii wenyewe wamejifungia ndani watawezaje kuja nchini kutalii? tuhamasishane tu wapwa tukatalii wenyewe kwenye mbuga zetu
Mtego wa NotiHao watalii wenyewe wamejifungia ndani watawezaje kuja nchini kutalii? tuhamasishane tu wapwa tukatalii wenyewe kwenye mbuga zetu
TiticombWeka akiba ya maneno usije ukaumbuka siku chache zijazo.
Jana jioni nimekaa sehemu pembezoni mwa Morogoro Road nimeona Land Cruiser ya utalii imebeba watalii.
Ukienda kwenye ukurasa wa twitter wa Quartar Airways utaona tangazo kuanzia tarehe 16 June 2020 wanaanza safari za kuja Tanzania (jiji la Dar es Salaam).
Nenda pale airport ya JNIA kuna kampuni ya LSG Skychefs wameambiwa na kampuni flani kubwa ya ndege wataanza kuchukua huduma zao za inflight catering tarehe hizo nilizotaja hapo juu.
Nenda Zanzibar utaona pilikapilika zinazo endelea uwanja wao wa ndege wa kimataifa.
Siasa zisizidi uwezo wetu wa kuchanganua mambo, kutafakari na kutafuta ukweli.
Titicomb
Kama mtanzania nitashukuru kama nchi yetu itakuwa imeshukiwa na "Neema" kiasi kikubwa hivyo!
Ni jambo jema sana, kama hayo mashirika ya ndege ya kimataifa, ndiyo yanayotupigia debe kama Taifa, ili tuzidi kung'ara katika anga za kiutalii kimataifaTena Qatar kwenye tangazo lao la kuaja Dar tarehe 16 June wameipamba nchi yetu kama kitovu(hub) ya utalii Afrika. Wanatupigia debe utalii kimtindo.
Tena alitangaza kwamba ziko 'fully booked' hadi Oktoba!Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??
Hawa waliletwa na shirika gani la ndege, au walikodi ya kwao kuja kutalii?Jana jioni nimekaa sehemu pembezoni mwa Morogoro Road nimeona Land Cruiser ya utalii imebeba watalii.
Tatizo mnalala peke yenu mnakosa watu wa kuwaliwaza. Bawacha 96% nasikia hamjaolewa ndio maana mnaandika upuuzi. Kwa hiyo unadhani ndege huwa zina miminika kama chai kwenye kikombe?Tulimsikia Mheshimiwa Rais akiutangazia Ulimwengu kuwa ameifungua mipaka ya nchi na hivi sasa ni ruksa mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa kuzileta ndege zao nchini
Sasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.
Hata hivyo kimya kizito huko angani namna kulivyokuwa kweupe, ndiko kulikonifanya nilazimike kiandika "thread" hii.
Swali ninalojiulza sasa ni je hayo mashirika ya ndege, hayajamsikia Mheshimiwa Rais akizifungua anga za nchi yetu??
Ni jambo la wazi kuwa hayo mashirika ya ndege yamesikia tamko hilo la Rais, ila kama tujuavyo hayo mashirika ya ndege yanafanya biashara, huwezi kurusha ndege ya Boeing yenye kuchukua abiria zaidi ya 300, ukiwa umebeba abiria 5 kuja nchini, hakika safari hiyo hailipi, kwa maana nyingine utasitisha safari za namna hiyo.
Ukweli ni lazima tumwambie Mheshimiwa Rais kuwa zile propaganda zinazoiendesha nchi kwa hivi sasa haziwezi kufanya kazi huko kwenye anga ya kimataifa
Hivi unadhani mtalii gani toka kwenye nchi yoyote atakuja Tanzania kwa hivi sasa, nchi ambayo "imegoma" kutoa takwimu za ugonjwa wa corona kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu hivi sasa??
Hivi Rais wetu anadhani kuwa dunia anaweza kuihadaa kirahisi rahisi, kama ambavyo anaweza kutuhadaa watanzania??
Tumemsikia wenyewe Waziri wa Mali asili na utalii, Hamisi Kigwangala, akionyesha kukatishwa tamaa na sekta ya utalii inavyoenda kwa hivi sasa!
Nashauri kama Taifa tuwe wasema kweli kwa mambo mbalimbali, ndipo tutapoaminika huko duniani
Kwa mwenendo huu tunaokwenda nao hivi sasa ya kila kitu tunapenda kupiga "fix" ndiko huku tulikolifikisha Taifa letu kwa hivi sasa
Ndege sio sawa na gari mkuuSasa tulitegemea baada ya tamko hilo la Rais, tuzione ndege zikimiminika kuja nchini kuwaleta watalii na wafanyibiashara mbalimbali.
Za kuambiwa changanya na zako 😁 😛Rais Magufuli alituambia hadharani kuwa KLM imekuwa booked mpaka mwezi wa nane eti na imeshajaa abiria wa kuja Tanzania ila cha ajabu hii ni mara ya tatu kwa hiyo ndege kuahirisha safari ya kuja Tz kwa kukosa abiria. Yani watu ni waongo waongo wanawadanganya tu kina yakhe na yenyewe yanaitika.
Comedy indeed. Angeanza yeye na madege yake ya ATCL kuleta watalii wengine wafuate. Kwetu gonjwa limekwisha siku nyingi na madege tunayo na vivutio tunavyo kuliko nchi yoyote duniani na mitishamba ya kujifukiza iko tele. Tatizo liko wapi mpaka tutegemee mabeberu waje kwa ndege zao zetu zikiwa zimepark tu?Tena alitangaza kwamba ziko 'fully booked' hadi Oktoba!
Hizi ndege zenye wasafiri wengi kiasi hiki ziko wapi, mbona haziji?
Hizi komedi za siku hizi hata kucheka inashindikana kwa wanaozisikiliza.