Angalia George Weah baada ya kutoka kwenye kiti cha Urais jinsi anavyoishi maisha ya kawaida

Angalia George Weah baada ya kutoka kwenye kiti cha Urais jinsi anavyoishi maisha ya kawaida

Inapaswa hii clip imfikie mbowe ili ajue kustaafu pia unaweza kula bata,

Maana inaelekea anaogopa sana kupoteza ile heshima aliyokuwa nayo.

Hakuna kinachodumu milele , akubaliane na hali halisi tu
Ningekuwa na mipesa kiwango cha Mbowe, ningekuwa nacheza na watoto na wajukuu na kiangalia miradi tu. Stress za nini sixties
 
Waafrika wengi hung'ang'ania madaraka kwa hofu ya kurudia kuishi maisha yao ya kawaida ya zamani.

Lakini aliyekuwa Rais wa zamani wa Liberia, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2023 dhidi ya mpinzani wake Joseph Boakai, mambo yamekuwa tofauti.

Weah ambaye kabla ya kuwa Rais wa nchi yake alikuwa ni mchezaji Mpira maarufu duniani, amerudi kijijini kwao na anaishi maisha yake ya kawaida na marafiki zake wa zama za utotoni.

AMEJIKUBALI.

View attachment 3196574
Kwa hapa Tanganyika hili haliwezekani kwa kuwa marais wastaafu wanaogopa kulipizwa kisasi na ndugu za jamaa waliowapoteza na kuwaua wakati wa utawala wao.
 
Unaweza kuta nje ya uzio una kuna Wanajeshi wakutosha usiwaamini wanasiasa hata bahati mbaya
 
Unaweza kuta nje ya uzio una kuna Wanajeshi wakutosha usiwaamini wanasiasa hata bahati mbaya
Hiyo ni stahili yake.

Kuna watu wakipata madaraka hawakumbuki hata ndugu zao waliowachangia ada wakati wanasoma.

Unadhani leo hii unaweza kumkuta mwanasiasa mzaramo anacheza mkwaju Ngoma kijijini kwao?

Wanasiasa wengi wa Afrika wakishika madaraka hujibadili na kuanza kudhani ule uzamani wao ni uduni wa maisha ulioko kwenye historia ya maisha yao.
 
Lissu anavyowahadaa chadema.... anaahidi mambo mengi wakati hata mkewe kashindwa kumtunza, analishwa na wazungu
Malipo ya mwezi mmoja tu ulaya, kubeba tu ma-box au kuzibua vyoo, au kulea wazee ama kuosha vyombo, ni mshahara wa mwezi wa Mbunge wa Tanzania anayetembelea VX. Mkewe Lissu akitaka kurudi hahitaji mchango wa nauli ya mtu. Labda walikubaliana abaki na watoto kwa usalama wao.
 
Ningekuwa na mipesa kiwango cha Mbowe, ningekuwa nacheza na watoto na wajukuu na kiangalia miradi tu. Stress za nini sixties
Hili tatizo lipo kwa watu wengi sana mkuu.

Na ndio maana wastaafu wengi huwa hawakai sana mtaani.

Ipo haja ya kuwa na wanasaikolojia maalum kuhusiana na maswala kama haya.

Mtu kupoteza heshima yote hiyo ghafla tu sio kitu rahisi.
 
Una hoja... Usikilizwe.
 
Weah ambaye kabla ya kuwa Rais wa nchi yake alikuwa ni mchezaji Mpira maarufu duniani, amerudi kijijini kwao na anaishi maisha yake ya kawaida na marafiki zake wa zama za utotoni.
Alipokuwa Rais aliwaachaje hao rafiki zake
 
Mimi iyo nyimbo ya pili tu na ana play kupitia simu yake mwenyewe hahah.
 
Back
Top Bottom