Angalia jinsi mlima Kilimanjaro unavyoonekana ukiwa nchi jirani

Angalia jinsi mlima Kilimanjaro unavyoonekana ukiwa nchi jirani

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
312
Reaction score
616
Zifuatazo ni picha zikionyesha muonekano wa mt Kilimanjaro ukiwa nchi ya Kenya mbuga inaitwa amboseli, hizi picha zinapatikana kwenye tovuti yao yao ya matangazo kwa uelewa wangu mdogo tumeshindwa hata kuweka haki miliki?

Kumbuka watalii wakiwa mbuga ya Amboseli wana uwezo wa kuangalia wanyama huku wanaangalia mlima kama inavyoonekana pichani.

Tanzania mbuga pekee ambayo unaweza kuangalia wanyama huku unaona mlima kwa uzuri ni mbuga ya Mkomazi ambayo hata haijulikani, haina wanyama wa kutosha na pia miundo Mbinu siyo rafiki sana, nilimsikia mzalendo namba moja akisema kuwa ataweka uzio kuzunguka mlima nadhani hii pia ingesaidia na pia kuwa na hakimiliki.
 

Attachments

  • 29DB1D6E-1F0B-423D-BD3D-EAF70572AA0E.jpeg
    29DB1D6E-1F0B-423D-BD3D-EAF70572AA0E.jpeg
    46.1 KB · Views: 25
  • 45219313-D25F-4EFA-B5C6-5F3D77E95544.jpeg
    45219313-D25F-4EFA-B5C6-5F3D77E95544.jpeg
    54.4 KB · Views: 16
  • 6B5222D4-3872-4C7A-821F-92250D2E17E8.jpeg
    6B5222D4-3872-4C7A-821F-92250D2E17E8.jpeg
    44.1 KB · Views: 22
  • D850EB4C-ADE4-4964-822A-D37479FD8990.jpeg
    D850EB4C-ADE4-4964-822A-D37479FD8990.jpeg
    42.2 KB · Views: 19
Sawa watalii wakiwa Kenya wanapata view nzuri sana na wanachukua picha nzuri za wanyama zenye background ya mlima lakini hawawezi kupanda huo mlima

Hakuna namna ya kuzuia hilo, kama una namna tuambie tufanyaje au mtumie Mh. Kigwangala ujumbe achukue hatua.
 
Labda uhamishiwe koromije, vinginevyo utaendelea kuonekana.
 
Una uhakika hili litafanya kazi?
Hili ni jukwaa huru na wewe unaruhusiwa kuchangia, kukosoa bila mbadala siyo sahihi tunajenga nyumba moja (Tz) kama unaona ni sawa kwenda Kenya ili uone mlima uliopo Tz basi kheri
 
Kuna resource ambazo ni trans boundary, ingawa nyingine ziko physically nchi nyingine lakini aliyeko jirani anaweza faida labda kwa macho kufurahia scenery au mfano uwepo wa msitu jirani ambao unasaidia kuregulate climate ya eneo husika.

Acha wenzetu wafaidi maana sote tu wa Mungu, na vyote ni vya Mungu.
 
Hii app itasaidia sana . Itakuwa nje ya mipaka ta Tz ukiangalia Mt Kilimanjaro kwa zaidi ya sekunde 30. Kwenye simu yako au akaunti yako ya benki, au mfumo wako wa fedha itakuja txt kuwa 0.5Usp inakatwa.

Kwa ndugu zetu, tuvumilieni tuko tunajenga nchi.

Developers wako kwa fainal touch
 
Hii app itasaidia sana . Itakuwa nje ya mipaka ta Tz ukiangalia Mt Kilimanjaro kwa zaidi ya sekunde 30. Kwenye simu yako au akaunti yako ya benki, au mfumo wako wa fedha itakuja txt kuwa 0.5Usp inakatwa.

Kwa ndugu zetu, tuvumilieni tuko tunajenga nchi.
Developers wako kwa fainal touch
Hope uko serious sio kejeli
 
Kuna mgombea WA kijani alidai ataweka pazia wakamcheka.😔😔😔
 
Back
Top Bottom