Angalia umri wa afisa mpya wa mawasiliano/habari wa ikulu ya Marekani (White House) pamoja na elimu yake! Njoo bongo!

Angalia umri wa afisa mpya wa mawasiliano/habari wa ikulu ya Marekani (White House) pamoja na elimu yake! Njoo bongo!

Trump amemchagua afisa habari wa ikulu ya Marekani kwa muhula mpya unaokuja. Ni afisa kijana na siyo mara ya kwanza kwa nafasi yake!

Angalia umri wake pamoja na elimu yake, hatishi sana kielimu (mtazamo finyu wa watanzania). Unahisi nini kimembeba??

Pamoja na uzoefu wake akiwa ikulu plus 'connection',bila shaka uwezo wake ni mkubwa!

Chukua umri wake kwa kijana wa kitanzania plus hiyo elimu kisha lete mtazamo wako! Nafikiri wenzetu wanaangalia uwezo kwanza kisha connection!

Trump nominates youngest press secretary in US history​


At just 27 years old, Leavitt will make history as the youngest person to hold the position.

Trump nominates youngest press secretary in US history



Nb: Ni mtazamo tu!
Mazingira ni tofauti Huku kiaka 27 bado anaamka nyumbani kwa wazazi bado hajaanza kujitegemea kikamilifu.
 
Hapana, hayo ni mawazo yako tu, hunijui.

Na kama kawaida yenu Wabongo wengi ni mabingwa wa kutunga hadithi na kuziweka kama ukweli hata pale ambapo hamjui ukweli na mlitakiwa kuuliza tu kujuzwa.

Inawezekana kabisa mimi na wewe tusiweze kabisa kuelewana na jitihada za kuelewana zikawa sana na jitihada za kumfundisha guluguja asiye na ubongo wala uti wa mgongo hesabu za String Theory.
Poa poa mkuu big up...🤝
 
Mazingira ni tofauti Huku kiaka 27 bado anaamka nyumbani kwa wazazi bado hajaanza kujitegemea kikamilifu.
Cheo chenyewe kina deserve mtu ambae yupo active kulinga na dunia tuliyonayo yenye inaenda kasi balaa asa angemchagua babu/bibi ili iweje?
Ikulu saivi lazima pachangamke ukizingatia ni muhula wa mwisho alafu inabidi mambo mengi ya mageuzi ya tokee kwahiyo lazima damu ya moto iingie mzigoni .
 
  • Thanks
Reactions: apk
Gentleman,
kwani kuna ubaya wowote wajemeni?

tatizo liko wapi angali tunafanya kazi nzuri sana kwa weledi na maslahi mapana ya Taifa na waTanzania wote?🐒
Kwa sisi kuaminiwa vijana kuingia ikulu watatumia ile kauli ya mwasisi wa taifa hili
"IKULU NI MAHALI PATAKATIFU............"
 
Unajua nchi za wenzetu hawaangalie elimu uliyo nayo kama nchi za Africa Cha muhimu wanaangalia uwezo wako una kitu Gani ulichonazo talent yako ni nini unaweza kufanya nini elimu ya Africa kwanza hawaiamini Mimi Kuna ndugu yangu Yuko america alisoma bongo maswala ya udaktari alivyokwenda kule kuwaonyesha chet hawakukiamini ikabidi asome tena kule upya kwenye shule zao
Hivi hata wewe ungekuwa ni mmarekani ungeamini daktari mwenye elimu kutoka Bongo? Kna Samia wenyewe wanakimbia wanakwenda nje kutibiwa, mtu wa aina hii utamwamini atibu raia wako?
 
Tatizo wanaisikilizia Marekani redioni.

Marekani ukiisikia kutoka Buza na Marekani ukiishi Marekani ni nchi mbili tofauti ujue.
Pia wengi hawana uwezo wa kufuatilia mijadala fikirishi kwenye media za kimataifa kuhusu siasa za Marekani na mataifa mengine makubwa.

Wanafuatilia vitaarifa vya kishabiki vinavyosambazwa na bloggers hasa wale wenye kuhangaika na mielekeo ya conspiracies.
 
Pia wengi hawana uwezo wa kufuatilia mijadala fikirishi kwenye media za kimataifa kuhusu siasa za Marekani na mataifa mengine makubwa.

Wanafuatilia vitaarifa vya kishabiki vinavyosambazwa na bloggers hasa wale wenye kuhangaika na mielekeo ya conspiracies.
Ndiyo hivyo mkuu.

Halafu mtu anakuja hapa kujadiliana nami ambaye nimeichambua kutoka Alexis de Tocqueville mpaka Fareed Zakaria.

A to Z.
 
Kibongo bongo.. umri huo mi nawaza tuu connection ya mshangazi..

Kuhusu uwezo hapa bongo wengi waliopo kwenye system baadhi yao hawana kitu kabisa l.. amini kwamba.

Kuna watu hatulali kutwa tunafanya kazi za watu ambao wenyewe walifika pale kama professional wa hizo kazi..

Connection zonafanyika ila za kingese sana...
 
Kwahyo umpeleke kijana wa miaka 27 pale magogoni akawe afisa habari?🤣🤣🤣🤣 userious kidogo tafadhali. Bongo mtu wa umri huo bado anavuta bange kwanza,hotels na lodge ni yeye,sasa unadhani atfanya ipasavyo hyo kazi?
 
Back
Top Bottom