Watu wanapimwa kutokana na kazi zao na misimamo yao wanavyo isimamia, watu hawapimwi kwa maneno maneno, na midaharo labda Kama hawajawahi kuhudumu popote.
Lisu amesha wahi kuwa, mbunge, rais wa wanasheria,kiongozi ndani ya Chadema mbaka Sasa. Akiwa mbunge aliwashawishi wananchi wa jimbo lake wasi changie madawati,maabara,na vyumba vya madarasa huku akifahamu watotowake hawasomi hapo wanasoma shule za kulipia.
Ana shawishi hivyo wakati karibu nchi nzima wananchi waliunga mkono juhudi za serikali kuchangia ujenzi uo.
Akiwa mjumbe wa kamati kuu Chadema Lisu anasema Yeye ndie aliye andaa waraka ulioitwa wa mafisadi na alizunguka nchi nzima kuunadi na katika waraka huo alimwandika Lowasa Kama fisadi kiongozi lakini chakushangaza Lowasa alipo kosa nafasi ya kugombea urais kupitia CCM yeye Lisu na Mbowe waka mkaribisha Chadema agombee nafasi hiyo ya Urais uku apo kabla wakiwa wame waaminisha wa Tanzania kwamba Lowasa ni Fisadi.
Akiwa mjumbe wa kamati kuu na mwanasheria wa chadema, walimfukuza Zitto Kabwe kwa tuhuma za kupanga njama za kumpindua Mwenyekiti bila kumpa nafasi ya kujitetea na zitto alipo kimbilia mahakamani Lisu akatamka Zitto atabaki kua mbunge wa mahakama
Lisu Kama kiongozi alishuhudia matumizi ya hovyo ya fedha za Chadema zilizo tolewa na wafadhili wa ndani na nje ya nchi, michango ya wabunge, rushwa za ngono katika kupata wabunge wa Viti maalumu kwa maslahi ya baadhi ya viongozi wanao muunga mkono Mwenyekiti DJ, bila kukemea au kupinga kwa namna yoyote na yeye kwa jinsi ya mazingira yalivyo inaonekana ni mnufaikaji mkubwa wa Mambo ya hovyo ndani ya Chadema.
Hizo ndizo rangi halisi za Lisu.
JPM yeye misimamo yake na uchapakazi wake tangua akiwa naibu waziri mbaka waziri anafahamika ni mtumishi asiye yumba katika kupigania Taifa la Tanzania. Katika kipindi chake akihudumu Kama waziri ndie alikua mmoja wa waziri Bora kutokea nchi hii Kati ya walio acha alama ya utendaji kazi ukimwacha sokoine na Agustino mrema.
JPM akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano kazizake zinaongea zenyewe. Uhitaji mjadala au kongamano kuwapima utendaji kazi wao au misimamo yao wakati kazi zao walizo wahi kuzifanya zinaongea.
JPM is far better than Lisu.
Lisu anamapungufu mengi sana kuweza kupewa nchi. Ana kiburi kisicho na faida na kumfanya asiweze kuyaona Mambo ki uhalisia wake, kitendo Cha kutuhumu watu tu akiwa kwenye kampeni zake bila ushahidi tena akiwa mwanasheria ni mapungufu ambayo hayaelezeki