Angalia US Presidential Debate 2020

Angalia US Presidential Debate 2020

Angalia hapa



Kuwa na Trump kwenye debate ni upuuzi tupu; hana akili ya kujadili bali anajua kubishana na kuongopa tu. Halafu Moderator anamwachia sana kuingilia.

Kumbuka alishinda hivyo hivyo kimzamzaa
 
Mdahalo wa kwanza wa Urais wa Marekani ambao umefanyika alfajili ya leo umeonyesha ni jinsi gani wapiga kura wanaweza kupima sera na upeo ya kisiasa wa wagombea.

Ni mfano mzuri sana na unaopunguza gharama kwa wagombea, kwani wanapata wakati nzuri kuwafikia wapiga kura wengi zaidi na kiurahisi kupitia Televisheni.

Leo Wamarekani milioni 300 wamefuatilia Mdahalo huu. Huo ni mtaji mzuri kwa wapiga kura kwa Wagonbea.

Japo ulikuwa na vurugu za Trump kuingilia sana nafasi ya Biden lakini umewajenga kikampeni kila upande.

Hoza zilizotawala zilihusu Covid-19, Uchumi, Afya, Ubaguzi wa Rangi na mabadiliki ya hali ya hewa.

Duniani watu zaidi bilioni 2 wameshuhudia Mdahalo.

Tuko kwenye uchaguzi nini Watanzania tunachojifunza kwenye mdahalo kama, huo? Sasa tuone umuhimu wa wagombea wakubwa Tanzania kuchuana ili wapiga kura tuweze kuchambua pumba na mchele.

Magufuli Vs Lissu utawezesha watu kuchambua sera zao. Mhendesha Mdahalo ( Debate Moderator) awe Jaji mstaafu ambaye hana upande ili tupate chakula ya ubongo.
 
JPM hawezi mdahalo kamwe, ccm kwa Mara ya kwanza wana mgombea asiyejiweza sana kukabiliana na wagombea wengine kwa hoja
 
Wenzetu wako mbali Sana kiuchumi angalia ishu zilizojadiliwa Kwenye mdahalo wao ni vitu vitano muhimu Kwa nchi yao yaani UCHUMI,UBAGUZI WA RANGI,COVID-19,AFYA NA HALI YA HEWA...sasa ukirud huku kwetu ni aibu tupu miaka 50 ya UHURU bado tupo Kwenye siasa za Maji ya visima,umeme vijijini, barabara za Lami na majosho ya ng'ombe.

MUNGU atusamehe Tu Kwa kweli!!!
 
We need a debate, kama mtu hawezi ku debate hafai kungoza. Kuogopa debate ni kuwa una mapungufu ambayo hutaki watu wayaone.
 
Wenzetu wako mbali Sana kiuchumi angalia ishu zilizojadiliwa Kwenye mdahalo wao ni vitu vitano muhimu Kwa nchi yao yaani UCHUMI,UBAGUZI WA RANGI,COVID-19,AFYA NA HALI YA HEWA...sasa ukirud huku kwetu ni aibu tupu miaka 50 ya UHURU bado tupo Kwenye siasa za Maji ya visima,umeme vijijini, barabara za Lami na majosho ya ng'ombe.

MUNGU atusamehe Tu Kwa kweli!!!
Huku danganyika kuna lijamaa linapita kuhubiri maendeleo hayana chama wakati huo huo linaeneza chuki dhidi ya upinzani.
Sijui limebobwa lile lijamaa
 
Wenzetu wako mbali Sana kiuchumi angalia ishu zilizojadiliwa Kwenye mdahalo wao ni vitu vitano muhimu Kwa nchi yao yaani UCHUMI,UBAGUZI WA RANGI,COVID-19,AFYA NA HALI YA HEWA...sasa ukirud huku kwetu ni aibu tupu miaka 50 ya UHURU bado tupo Kwenye siasa za Maji ya visima,umeme vijijini, barabara za Lami na majosho ya ng'ombe.

MUNGU atusamehe Tu Kwa kweli!!!

Bwana yule asiyeweza mdahalo Wala kufahamu kiingereza vizuri anahutubia injili ya wanawake warembo na weupe na kumuoza mama yake kwa mahari ya jogoo. Tutafika kweli?!
 
Bwana yule asiyeweza mdahalo Wala kufahamu kiingereza vizuri anahutubia injili ya wanawake warembo na weupe na kumuoza mama yake kwa mahari ya jogoo. Tutafika kweli?!
Kwa kweli
 
kwa hiyo marekani wakifanya debate na sisi tufanye debate? Tanzania is not a copy cat of USA that is why we have different names they are called USA we are called Tanzania
 
Watu wanapimwa kutokana na kazi zao na misimamo yao wanavyo isimamia, watu hawapimwi kwa maneno maneno, na midaharo labda Kama hawajawahi kuhudumu popote.

Lisu amesha wahi kuwa, mbunge, rais wa wanasheria,kiongozi ndani ya Chadema mbaka Sasa. Akiwa mbunge aliwashawishi wananchi wa jimbo lake wasi changie madawati,maabara,na vyumba vya madarasa huku akifahamu watotowake hawasomi hapo wanasoma shule za kulipia.

Ana shawishi hivyo wakati karibu nchi nzima wananchi waliunga mkono juhudi za serikali kuchangia ujenzi uo.

Akiwa mjumbe wa kamati kuu Chadema Lisu anasema Yeye ndie aliye andaa waraka ulioitwa wa mafisadi na alizunguka nchi nzima kuunadi na katika waraka huo alimwandika Lowasa Kama fisadi kiongozi lakini chakushangaza Lowasa alipo kosa nafasi ya kugombea urais kupitia CCM yeye Lisu na Mbowe waka mkaribisha Chadema agombee nafasi hiyo ya Urais uku apo kabla wakiwa wame waaminisha wa Tanzania kwamba Lowasa ni Fisadi.

Akiwa mjumbe wa kamati kuu na mwanasheria wa chadema, walimfukuza Zitto Kabwe kwa tuhuma za kupanga njama za kumpindua Mwenyekiti bila kumpa nafasi ya kujitetea na zitto alipo kimbilia mahakamani Lisu akatamka Zitto atabaki kua mbunge wa mahakama

Lisu Kama kiongozi alishuhudia matumizi ya hovyo ya fedha za Chadema zilizo tolewa na wafadhili wa ndani na nje ya nchi, michango ya wabunge, rushwa za ngono katika kupata wabunge wa Viti maalumu kwa maslahi ya baadhi ya viongozi wanao muunga mkono Mwenyekiti DJ, bila kukemea au kupinga kwa namna yoyote na yeye kwa jinsi ya mazingira yalivyo inaonekana ni mnufaikaji mkubwa wa Mambo ya hovyo ndani ya Chadema.
Hizo ndizo rangi halisi za Lisu.

JPM yeye misimamo yake na uchapakazi wake tangua akiwa naibu waziri mbaka waziri anafahamika ni mtumishi asiye yumba katika kupigania Taifa la Tanzania. Katika kipindi chake akihudumu Kama waziri ndie alikua mmoja wa waziri Bora kutokea nchi hii Kati ya walio acha alama ya utendaji kazi ukimwacha sokoine na Agustino mrema.
JPM akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano kazizake zinaongea zenyewe. Uhitaji mjadala au kongamano kuwapima utendaji kazi wao au misimamo yao wakati kazi zao walizo wahi kuzifanya zinaongea.
JPM is far better than Lisu.

Lisu anamapungufu mengi sana kuweza kupewa nchi. Ana kiburi kisicho na faida na kumfanya asiweze kuyaona Mambo ki uhalisia wake, kitendo Cha kutuhumu watu tu akiwa kwenye kampeni zake bila ushahidi tena akiwa mwanasheria ni mapungufu ambayo hayaelezeki
 
Kuna Mambo yanafanywa kipindi Cha UCHAGUZI yanayofungua vichwa vya watu na kuondoa mawazo mgando.

Mtifuano wa Trump na Biden unatufunza kujenga hoja, kuomba ridhaa kwa kuwaaminisha wananchi kwamba unaweza, kujadili na mpinzani mwako na kumwonyesha kwanini wewe Ni Bora zaidi.

Jambo la mdahalo linapendwa na Watanzania wote bila kujali vyama, watu wanataka kuona tunateteaje kile tumekua tukiimba kila siku?

Lakini kwa wanasiasa wetu waliozoea kudanganya ukiwaambia mdahalo unaweza kupigwa pingu. Wanaamini katika ujanja ujanja wa hoja, wanaamini katika ndiyo Mzee.

CCM Kama chama kikubwa itisheni mdahalo wa wagombea urais kuondoa utata unaondelea juu ya Nani Ni mwongo na Nani Ni mkweli. Kama mnajiamini itisheni mdahalo acheni kusifia mdahalo wa Mabeberu.
 
Back
Top Bottom