Angalia US Presidential Debate 2020

Angalia US Presidential Debate 2020

Punguza presha mjomba redio. Hii ni mada ya mdahalo kati ya Trump na Biden, umeufuatilia lakini? Au umetoka usingizini ukimuota Lissu ukaishia kuangukia humu na lipost lako refu lisiloendana na mada husika?
 
Watu wanapimwa kutokana na kazi zao na misimamo yao wanavyo isimamia, watu hawapimwi kwa maneno maneno, na midaharo labda Kama hawajawahi kuhudumu popote.

Lisu amesha wahi kuwa, mbunge, rais wa wanasheria,kiongozi ndani ya Chadema mbaka Sasa. Akiwa mbunge aliwashawishi wananchi wa jimbo lake wasi changie madawati,maabara,na vyumba vya madarasa huku akifahamu watotowake hawasomi hapo wanasoma shule za kulipia.
Ana shawishi hivyo wakati karibu nchi nzima wananchi waliunga mkono juhudi za serikali kuchangia ujenzi uo.
Akiwa mjumbe wa kamati kuu Chadema Lisu anasema Yeye ndie aliye andaa waraka ulioitwa wa mafisadi na alizunguka nchi nzima kuunadi na katika waraka huo alimwandika Lowasa Kama fisadi kiongozi lakini chakushangaza Lowasa alipo kosa nafasi ya kugombea urais kupitia CCM yeye Lisu na Mbowe waka mkaribisha Chadema agombee nafasi hiyo ya Urais uku apo kabla wakiwa wame waaminisha wa Tanzania kwamba Lowasa ni Fisadi.

Akiwa mjumbe wa kamati kuu na mwanasheria wa chadema, walimfukuza Zitto Kabwe kwa tuhuma za kupanga njama za kumpindua Mwenyekiti bila kumpa nafasi ya kujitetea na zitto alipo kimbilia mahakamani Lisu akatamka Zitto atabaki kua mbunge wa mahakama

Lisu Kama kiongozi alishuhudia matumizi ya hovyo ya fedha za Chadema zilizo tolewa na wafadhili wa ndani na nje ya nchi, michango ya wabunge, rushwa za ngono katika kupata wabunge wa Viti maalumu kwa maslahi ya baadhi ya viongozi wanao muunga mkono Mwenyekiti DJ, bila kukemea au kupinga kwa namna yoyote na yeye kwa jinsi ya mazingira yalivyo inaonekana ni mnufaikaji mkubwa wa Mambo ya hovyo ndani ya Chadema.
Hizo ndizo rangi halisi za Lisu.

JPM yeye misimamo yake na uchapakazi wake tangua akiwa naibu waziri mbaka waziri anafahamika ni mtumishi asiye yumba katika kupigania Taifa la Tanzania. Katika kipindi chake akihudumu Kama waziri ndie alikua mmoja wa waziri Bora kutokea nchi hii Kati ya walio acha alama ya utendaji kazi ukimwacha sokoine na Agustino mrema.
JPM akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano kazizake zinaongea zenyewe. Uhitaji mjadala au kongamano kuwapima utendaji kazi wao au misimamo yao wakati kazi zao walizo wahi kuzifanya zinaongea.
JPM is far better than Lisu.

Lisu anamapungufu mengi sana kuweza kupewa nchi. Ana kiburi kisicho na faida na kumfanya asiweze kuyaona Mambo ki uhalisia wake, kitendo Cha kutuhumu watu tu akiwa kwenye kampeni zake bila ushahidi tena akiwa mwanasheria ni mapungufu ambayo hayaelezeki

Wewe unapiga propaganda za kisiasa tu hapa. Hakuna ukweli wala uhalisia ktk kila ulichosema/andika hapa unless uwe umeamua kujifyatua akili yako na ufahamu wako tu....

NIKUKUMBUSHE KITU HAPA 👇 👇👇

Kwamba, wewe "labda" umesahau ama hujui kitu kimoja muhimu sana hapa, kwamba;

"TENDO" lolote hutanguliwa na "FIKRA" ama "WAZO" kwanza...

Yaani UNAFIKIRI ama KUWAZA kwanza, kisha MAWAZO ama FIKRA hizo unaziweka katika MATENDO...

Wataalamu wanasema, UKIFIKIRI ama KUWAZA vibaya, obviously kutakupelekea KUAMUA vibaya na final end ni KUTENDA vibaya....

Kinyume chake ni KUFIKIRI ama KUWAZA vyema, hukuongoza KUAMUA vyema na final end yake ni KUTENDA vyema....

Kabla ya kumpa mtu kazi, kawaida anapewa some sort of debate altenatatively you can even call it "interview"....

Lengo la interview/debate ni kupima " mpangilio wa mawazo na ufikiri wa mtu" kwa sababu ZAO la TENDO lolote ni FIKRA/WAZO katika akili na ufahamu wa mtu...

Ndiyo kusema ukitaka kumtengeneza mtu utakavyo, Fanya kitu kimoja tu, INGIA KWENYE FIKRA ZAKE.......

Tunataka kuwapa watu kazi kubwa ya URAIS. Tunahitaji kabla ya kuwapa kazi hiyo kazi, wapitie kwenye VIPIMO VYA KITAALAMU mojawapo ni "mdahalo" a some sort of interview ili wapimwe mtiririko na mpangilio wa mawazo yao katika maeneo (nyanja) zote muhimu za kijamii, kidiplomasia, kisiasa, uchumi na maswala ya jumla ya ulimwengu (overall global current matters)...

Ujinga na upuuzi unaoendelea sasa ktk nchi yetu ni kwa sababu, kazi hii kubwa ya URAIS amepewa mtu ambaye hakupitia kwenye screening ya namna hii...

Aliokotwa tu huko from no where na kupewa jukumu hili zito linahitaji utimamu wa nafsi, akili na mwili. Matokeo yake everything is going astray....
 
Huku dunia ya tatu mdahalo mnajiamulia 2010 walitaka mdahalo,2015 wakakataaa kabisa mdahalo yaani ile KATAKATA,2020 wanataka tena mdahalo 😀😀 sijui 2025 napo watataka au watakataa,sometimes kuwa elewa hawa ndugu zetu kazi.

Hao waliokuwa madarakani ndio hawataki kabisa mdahalo.
 
Kuna mahali nimeona Biden 48% na Trump 41%
Opinion za wengi zinampa Joe nafasi ya kuongoza maana Trump alikuwa ana interrupt sana wakati jamaa anaongea.

Waliotaka kusikia hoja naona kama hawamkubali sana Trump.

Ila kwa kawaida kama wewe ni rais uliye madarakani, ni rahisi kuwa defensive kuliko mpinzani wako maana yeye hana mahali pa kuulizwa.

Naona Trump akaamua kuwa defensive as well as kumshambulia Joe.
 
Opinion za wengi zinampa Joe nafasi ya kuongoza maana Trump alikuwa ana interrupt sana wakati jamaa anaongea.

Waliotaka kusikia hoja naona kama hawamkubali sana Trump.

Ila kwa kawaida kama wewe ni rais uliye madarakani, ni rahisi kuwa defensive kuliko mpinzani wako maana yeye hana mahali pa kuulizwa.

Naona Trump akaamua kuwa defensive as well as kumshambulia Joe.
Uisahau kuwa Biden naye alikuwa VP serikali iliyopita, naye hawezi kujitenga na kuboronga au kufanikiwa kwa Obama.
Trump anajitahidi sana kuingilia uchaguzi, Tutaona mwisho wake.
 
Niko Macho nikifuatilia debate ya Mabeberu hapa.

Trump ni kama mtoto wa chokoraa,sio msikivu kabisa kwa moderator.
Debate ilikuwa trump vs Biden na moderator na kawachanachana vipande, Moderator yuko biased kwa biden ila trump kamchana chana
 
Hahaha
Adjustments.jpg
 
Wenzetu wako mbali Sana kiuchumi angalia ishu zilizojadiliwa Kwenye mdahalo wao ni vitu vitano muhimu Kwa nchi yao yaani UCHUMI,UBAGUZI WA RANGI,COVID-19,AFYA NA HALI YA HEWA...sasa ukirud huku kwetu ni aibu tupu miaka 50 ya UHURU bado tupo Kwenye siasa za Maji ya visima,umeme vijijini, barabara za Lami na majosho ya ng'ombe.

MUNGU atusamehe Tu Kwa kweli!!!

Ccm washatuona machizi
Ccm wanaudhi kweli
 
Back
Top Bottom