Angalia wenzetu walivyo mbali

Angalia wenzetu walivyo mbali

Mkuu laila hakushinda uchaguzi wewe acha kudanganya watu hizi ni politics tu

Uhuru ndo alishinda na atashinda tena 2017
Ni kweli kabisa kwamba UKenyatta alishinda kwa kura na wala hakuiba, ushindi huo ulikuja hivi!!!, kilichotokea ni kwamba upande wa anakotokea Raila (Nyanza Provience) ambako ndiyo wapiga kura wengi wa Raila zoezi la kupiga kula lilifungwa rasmi saa 5:00 jioni lakini upande anaotokea Kenyatta watu walipiga kura hadi 3:30 asubuhi maana misululu ya wapiga kula ilikuwa mrefu mno, siku hiyo kituo cha citizen kilikuwa kinarusha live maeneo yote ya kupigia kura nchi nzima. Mbinu iliyotumiwa na mashabiki wa jubilee ni kwamba walihakikisha kila mtu wao mejiandikisha na familia yake yote, hii pia ilichochewa na hali halisi ya siasa za Kenya kuwa asilimia kubwa huendeshwa kwa ukabila.
kwahiyo kabila lililokuwa linamuunga mkono Uhuru waliandikisha hadi vijana wao wa form II&III sasa sijui kama vijana wa kidato hicho walikuwa tayari na umri wa mpiga kura, hiyo ni kazi ya tume ya uchaguzi ya nchi husika. Kwahiyo Raila alishindwa kuwahamasisha waungaji mkono wake kuhakikisha kila mtu kwenye familia anajiandikisha na kupiga kula; nimeona nieleze kwa ufupi kuhusu Raila kuibiwa kura zake siyo kweli ila alizidiwa kete kwenye uandikishaji wapiga kura na ndo maana eneo lake walimaliza mapema kupiga kula wakati kwa mwenzake watu walipiga kura hadi asubuhi ya saa 3:30 (saa tisa na nusu usiku?
 
A
Mkuu, kwani ni lazima kucopy na kupaste toka Kenya? Kwa hiyo unataka Mapolisi wetu waue tu Raia hovyo kama wafanyavyo Polisi wa Kenya?

Acha upotoshaji, kama kuna sehemu polisi wanaonea na kuwanyanyasa raia basi ni TZ, yanayofanywa na polizi wa TZ, Kenya yaliisha baada ya utawala wa Moi Daniel.
An extra judicial killings kenya inashughuliwa haraka na askari anayehusika anawajibishwa kweli.
Wakenya wanajua haki zao, mfano: unakumbuka aliyekua naibu Jaji mkuu (Nancy) alifukuzwa kazi kwa kumtishia mlizi wa duka kwa pistol? Tanzania nani anaweza kumshtaki jaji achilia naibu jaji mkuu?? Kama watu wanaingizwa vidole na mgombo tu!!
 
Kenya yaliisha wapi wewe.. Je wale waouliwa na watu wasiojulikana nao vipi..!?
 
Hakuna ubaya wowote wa kuiga mazuri na kuachana na mabaya yao. Kwani Tanzania polisi hawaui hovyo raia? Waliotaka kumuua Ulimboka ni akina nani? Waliomuua Mwangosi ni akina nani? waliomuua Kombe ni akina nani? na vifo vingine chungu nzima vinavyofanywa na polisi nnchini. Acha kukurupuka!

Mkuu, kwani ni lazima kucopy na kupaste toka Kenya? Kwa hiyo unataka Mapolisi wetu waue tu Raia hovyo kama wafanyavyo Polisi wa Kenya?
 
Sio lazima tuige kila kitu but kama jambo ni zuri tunaiga mkuu
Lizaboni!!
Hata huzo kaxi sijui za mkurugenzi wa nini zingetangazwa watu waombe na wawe short listed. Sio kila kitu kuteua. Hata hao ma ras sijui nini sio nafadi za kusiasa ila gapa kwetu ni za watu wanaojipendekeza jwa mkubwa.$$$$$$it.
 
Katiba ya Kenya, iliyopatikana baada ya mgogoro mkubwa wa kisiasa, na katiba ya Afrika Kusini iliyopatikana baada ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, zinatajwa kuwa ndiyo katiba bora kabisa barani Afrika. Katiba yetu Tanzania ni kati ya katiba hovyo kabisa kwa sababu inategemea zaidi hekima ya Rais. Mkimpata Rais hovyo anaweza hata kuwaangamiza kwa kutumia katiba.

Katiba ya Tanzania imekaa kidikteta kwa sababu mamlaka makubwa yamerundikwa kwa mtu mmoja, Rais.
 
Katiba ya Tanzania inampa madaraka Rais kugawa vyeo na madaraka kama njugu, bila hata ya kumpa mwongozo. Ndiyo maana, hata leo, tunashuhudia Wenyeviti wengi wa bodi mbalimbali wanapewa nafasi hizo kama zawadi na wakati fulani kama msaada ili wasife njaa, bila ya kujali kuwa anayesaidiwa ni mtu mmoja na familia yake lakini kwa gharama ya mamilioni ya Watanzania ambao huyo aliyeteuliwa hataweza kutoa mchango wowote wa maana kwa Taifa.
 
Katiba ya Kenya, iliyopatikana baada ya mgogoro mkubwa wa kisiasa, na katiba ya Afrika Kusini iliyopatikana baada ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, zinatajwa kuwa ndiyo katiba bora kabisa barani Afrika. Katiba yetu Tanzania ni kati ya katiba hovyo kabisa kwa sababu inategemea zaidi hekima ya Rais. Mkimpata Rais hovyo anaweza hata kuwaangamiza kwa kutumia katiba.

Katiba ya Kenya na Afrika ya kusini ni kati ya katiba mbaya kabisa duniani kwa sababu zilipatikana baada ya mapambano ya kikabila (ubaguzi wa makabila).Wazungu wakiwabagua waafrika na waafrika wakibaguana wenyewe kwa wenyewe kikabila.Walipotwangana wenyewe kwa wenyewe wakaanzisha hizo katiba ambazo zinatambua serikali za majimbo ya kikabila.Kenya wanaserikali za majimbo ambayo yamegawanywa kikabila na Afrika kusini ni hivyo hivyo,India pia ni hivyo,Nigeria pia ni hivyo,marekani pia ni hivyo Kuna majimbo ya weusi na majimbo ya weupe.

Ukiwa na katiba inayotambua majimbo ya kikabila huwezi ita hiyo ni katiba bora.!!!
 
Usidanganye watu kuwa katiba ya Kenya na Afrika Kusini zinatambua majimbo ya kikabila. Huo ni uwongo mkubwa. Katiba zinatambua mamlaka ya majimbo japo ni kweli kuwa kama ilivyo Tanzania kila jimbo/mkoa kuna kabila fulani ndiyo ambalo lina wakazi wengi. Pia ni ukosefu wa uelewa kufikiria kuwa uwepo wa serikali za majimbo unaashiria upungufu. Mamlaka makubwa ya majimbo huonesha kiwango cha juu cha demokrasia, maana yake ni kuwa madaraka makubwa yapo kwa wananchi. Mwalimu wakati anafuta utawala wa majimbo, sababu kubwa aliyoitoa ni kwamba kwa sababu demokrasia ya Tanzania bado ni changa, utawala wa majimbo unaweza kupunguza umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo aliufuta kwa sababu Tanzania ilikuwa ni nchi yenye maendeleo madogo sana ya demokrasia.

Jambo la pili, nataka kukuelewesha, katiba kupatikana baada ya mapigano au baada ya migogoro haimaanishi kuwa haiwezi kuwa nzuri. Katiba ya Kenya na Afrika Kusini, inawezekana kabisa matukio mabaya ya kabla yaliwapa hekima na uelewa wa haja ya kuwa na katiba nzuri.
 
A

Acha upotoshaji, kama kuna sehemu polisi wanaonea na kuwanyanyasa raia basi ni TZ, yanayofanywa na polizi wa TZ, Kenya yaliisha baada ya utawala wa Moi Daniel.
An extra judicial killings kenya inashughuliwa haraka na askari anayehusika anawajibishwa kweli.
Wakenya wanajua haki zao, mfano: unakumbuka aliyekua naibu Jaji mkuu (Nancy) alifukuzwa kazi kwa kumtishia mlizi wa duka kwa pistol? Tanzania nani anaweza kumshtaki jaji achilia naibu jaji mkuu?? Kama watu wanaingizwa vidole na mgombo tu!!

Endelea kupotosha watu
 
Katiba ya Kenya na Afrika ya kusini ni kati ya katiba mbaya kabisa duniani kwa sababu zilipatikana baada ya mapambano ya kikabila (ubaguzi wa makabila).Wazungu wakiwabagua waafrika na waafrika wakibaguana wenyewe kwa wenyewe kikabila.Walipotwangana wenyewe kwa wenyewe wakaanzisha hizo katiba ambazo zinatambua serikali za majimbo ya kikabila.Kenya wanaserikali za majimbo ambayo yamegawanywa kikabila na Afrika kusini ni hivyo hivyo,India pia ni hivyo,Nigeria pia ni hivyo,marekani pia ni hivyo Kuna majimbo ya weusi na majimbo ya weupe.

Ukiwa na katiba inayotambua majimbo ya kikabila huwezi ita hiyo ni katiba bora.!!!

Huo ndio ukweli
Unakuta habari tena gazetini
Luo wapinga jubilee
Hahaha
 
Katiba ya Kenya, iliyopatikana baada ya mgogoro mkubwa wa kisiasa, na katiba ya Afrika Kusini iliyopatikana baada ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, zinatajwa kuwa ndiyo katiba bora kabisa barani Afrika. Katiba yetu Tanzania ni kati ya katiba hovyo kabisa kwa sababu inategemea zaidi hekima ya Rais. Mkimpata Rais hovyo anaweza hata kuwaangamiza kwa kutumia katiba.

Katiba ya Tanzania imekaa kidikteta kwa sababu mamlaka makubwa yamerundikwa kwa mtu mmoja, Rais.
Leo hii wakenya hao hao wameanza kuipinga na kuiona haifai
 
Mkuu, kwani ni lazima kucopy na kupaste toka Kenya? Kwa hiyo unataka Mapolisi wetu waue tu Raia hovyo kama wafanyavyo Polisi wa Kenya?
Hoja ya kuua imetoka wapi? Jadili hoja iliyopo mezani!. Lazima tujifunze kutoka mifumo ya wengine.
 
Back
Top Bottom