KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari za muda huu waungwana wa hapa jamvini......
Kwenye ulimwengu wa sasa uliojaa changamoto za ulaghai na uaminifu imekuwa ni changamoto kubwa sana kukutana na mwenza mwenye moyo wa dhati wa kujenga maisha na wewe......
Limekuwa jambo la kubahatisha kwa kuwa wakati mwingine waongo na wa kweli wanaongea lugha zinazofanana kiasi kwamba unaweza ukamfuga KASA ukidhani KOBE.....
ingawa wasanii ni wengi bado tunaweza kuona viashiria kadha wa kadha vya kutupa mwanga wa kutuoneshea uhalisia wa wale tunaodhania kuwa ni wenza wetu wa maisha.....
Sina maana ya kuwa ufanye uchunguzi lakini ni vyema wakati mwingine kujua mapema ili kuokoa muda, uhai na uchumi......na tunakumbushana kibinadamu kwani tunajua kuwa wakati mwingine ulevi wa mapenzi unazidi wa pombe na kupofua macho......
Unaweza ukamjua mtu wa hivyo kupitia mambo kadhaa yafuatayo
1) Hana AFFECTION na wewe
Nimekosa neno la moja kwa moja la kiswahili kuliweka hili jambo Sawa au kulielezea lakini naamini kama mtu mzima ambaye alishawahi kuwa penzini atakuwa ananielewa vyema...... affection kwenye uwanja wa mapenzi huonekana kwenye kila jambo mnalofanya pamoja ingawa humo humo kuna waigizaji lakini yenyewe huja automatic na huanzia moyoni........kama ukijitoa kwenye box la mapenzi na kutazama kwa macho yako makavu utaona kuwa hapa hakuna affection......
Tofauti ya affection ya mlaghai na ya kweli ni kuwa ya mlaghai huonekana sana au kwa wingi pale ambapo unataka kumfanyia au umeshamfanyia jambo linalomnufaisha yeye...... lakini nje ya hapo hutaona......nk
2)Muda mwingi hataki au anafupisha story na mipango ya pamoja ya muda mrefu.......
Watu hivyo huwa hawataki kushirikiana au kuyaongelea mambo au mipango ya pamoja ya muda mrefu na kama ukiona anaongelea sana mipango hyo basi ujue ni ile ambayo kwa asilimia kubwa yeye ndio atakuwa mnufaika mkubwa wa mipango hiyo.....
Mambo kama kufunga ndoa( unless kama NDOA ndio njia pekee ya kufikia malengo yake kwako).... kuanzisha familia.....kuonana au kujuana na watu wake wa karibu......hutaona anayapa kipaumbele lakini huwa wanafanya hivyo kwa kutumia akili kubwa Sana kwa kuwa wao wapo hapo kiakili na sio kimapenzi kama wewe.....
3) Kujifanya wana wivu na kukasirika kwa vitu vidogo vidogo
Hii kwa kifupi ni njia ya kukulaghai au kuku manipulate ili uwaone na wao wamezama kumbe wanaelea..... wanatumia akili nyingi sana lakini na wewe kama utatanguliza akili utagundua ujanja wao.....
4)Ukaribu wao unaongezeka kwako kwa kadri unavyomnufaisha na hupungua na kupotea kabisa ikiwa kinyume chake.......
Watu hawa kama hutakuwa na akili ya akiba unaweza kusema Mungu Baba amesikia kilio changu....kumbe unacheza scene ya muvi za watu bila ya wewe kujua......
Ngoja niishie hapa......
Nawasilisha....
STAY SAFE, PLAY SAFE......