ANGALIZO: Kutozingatia hivi vitu hutokuwa SHORTLISTED Ajira Portal

ANGALIZO: Kutozingatia hivi vitu hutokuwa SHORTLISTED Ajira Portal

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
Mama kaachia asali, mpaka July wengi mtakuwa mnasheherekea.

Nimekuwekea baadhi ya vidokezo vichache vinavyoweza kukunyima nafasi ya kuchaguliwa kwa ajili ya usaili (SHORTLISTED) kwa wanaopotia ajira portal.
  1. Kutosaini barua yako ya maombi, najua kabla ya kupakia barua yako ya maombi mfumo unakuambia hakikisha imesainiwa. Hii kuna wale wanaosaini pdf kwa kuinsert signature au online signature. Ukifanya hivi imekula kwako, print isaini kwa mwandiko wako na iscan tena.
  2. Scanning isiyo na viwango, wale wazee wa kumalizia kila kitu kwenye smartphone. Karatasi imejikunja na chafu Halafu unascan kwa simu yako inaacha water mark za "scanned by cam scanner". hauko serious mjuba.
  3. Vyeti vyako havijahakikiwa na advocate, na cha kuzaliwa hakijahakikiwa na rita. Hii najua kwenye maelekezo yao hawajasema ila nlikosa usaili kisa hiyo sababu. Nimeamabatanisha na screenshot ya ushahidi ili tomaso uamimi.
Wanaoomba ni wengi, kutakuwepo na vigezo vya ajabu vya kukutoa nje ya reli. Ni heri mkakutane Dodoma kwenye mnyukano ukose kuliko kuishia njiani.

Kama una vidokezo vingine ongezea hapa wadau wajue.
 
Screenshot_20220531-120127.png
 
Mama kaachia asali, mpk july wengi mtakuwa mnashrekea.

Nimekuwekea baadhi ya vidokezo vichache vinavyoweza kukunyima nafasi ya kuchaguliwa kwa ajili ya usaili (SHORTLISTED) kwa wanaopotia ajira portal.

1) kutosaini barua yako ya maombi, najua kabla ya kupakia barua yako ya maombi mfumo unakuambia hakikisha imesainiwa. Hii kuna wale wanaosaini pdf kwa kuinsert signature au online signature. ukifanya hivi imekula kwako, print isaini kwa mwandiko wako na iscan tena.

2) Scanning isiyo na viwango, wale wazee wa kumalizia kila kitu kwenye smartphone. Karatasi imejikunja na chafu alafu unascan kwa simu yako inaacha water mark za "scanned by cam scanner". hauko serious mjuba.

3) Vyeti vyako havijahakikiwa na advocate, na cha kuzaliwa hakijahakikiwa na rita. Hii najua kwenye maelekezo yao hawajasema ila nlikosa usaili kisa hiyo sababu. Nimeamabatanisha na screenshot ya ushahidi ili tomaso uamimi.
Wanaoomba ni wengi, kutakuwepo na vigezo vya ajabu vya kukutoa nje ya reli. Ni heri mkakutane dodoma kwenye mnyukano ukose kuliko kuishia njiani.
Kama una vidokezo vingine ongezea hapa wadau wajue.
Sasa apo kwenye kusainiwa barua aisee
 
Mkuu, nimesoma vizuri maelezo yako na kweli uko sahihi kwani nami yaliwahi kunikuta haya mwezi wa MARCH KUTOITWA kwenye kwenye Usaili kwa kuwa sikucertify vyeti na niliweka Uzi wangu humu. Ila hiko kipengele Cha kucertify Rita mara nyingi tunajua ni kwa wale wahitaji wa mikopo ya elimu ya juu, Mwenyewe nakumbuka kipindi naomba chuo na mkopo wa chuo kikuu nilicertify cheti Rita kwa ajili ya kupewa mkopo.

Sasa mambo yasiwe mengi, naomba ushahidi kuwa ulinyimwa nafasi ya Usaili utumishi kisa hukucertify cheti Cha kuzaliwa Rita Hali ya kuwa kwa Hakimu Ulicertify, hapo umeweka sababu mbili tu! Tunataka tujiridhishe maana mambo ni mengi na utumishi Kila kukicha wanabadilika.
 
Kuhusu ushahidi wa kupigwa chini coz sikucertify birth certificate rita kwa kweli sina, ila nilipopigwa chini kwa sababu sikucertify kwa advocate imenifanya niwaze hivyo coz hakuna popote kwenye terms zao wamesema lazima mtu acertify vyeti na bado walinipiga chini kwa kigezo hicho. ni taadhari tu mkuu hawa jamaa hawaishiwi kukutafutia kigezo cha kukubutua
 
Mimi natatizo moja: Kwenye sehemu ya kuattach vyeti nikiweka kwenye PDF form inakataa japo iko chini ya 2mb naomba msaada
 
Sina jibu la uhakika, watu wengi wako wanaomba sasa kuna uwezekano mfumo umezidiwa na umeanza kumisbehave kama ilivyokuwa zile za TAMISEMI

Pili shrink file lako liwe chini ya mb 1, ukishindwa viscan tena viwe na kb chache za TAMISEMI wako ambao pdf zilikuwa zinagoma, nilipo shrink zilikubali kupakia
 
Msaada jamani jinsi ya kudelete info kwenye upande wa academic, kwenye ajira portal
Chagua institution, nenda sehemu ya edit, jaza upya afu apload na cheti husika alafu tuma. ukitaka kudhibitisha km imebadilika fungua institute afu view hapo utaona cheti ulichopakia
 
Vya kuzaliwa ni RITA mkuu, inafanyika online kwenye web ya RITA
 
huo ndo uvivu wa kufikiri kwenye mifumo yetu mkuu. uwezo wa kudhibitisha uhalali wa cheti ni tasisi inayotoa hicho cheti

Hili neno kudhibitisha ni nani kakudanganyeni? Naona wengi mnalitumia pahala palipostahili. Ni kuthibitisha na sio kudhibitisha.

Mambo madogo kama haya mimi ningekua HR nakula kichwa.
 
Back
Top Bottom