Mama kaachia asali, mpaka July wengi mtakuwa mnasheherekea.
Nimekuwekea baadhi ya vidokezo vichache vinavyoweza kukunyima nafasi ya kuchaguliwa kwa ajili ya usaili (SHORTLISTED) kwa wanaopotia ajira portal.
- Kutosaini barua yako ya maombi, najua kabla ya kupakia barua yako ya maombi mfumo unakuambia hakikisha imesainiwa. Hii kuna wale wanaosaini pdf kwa kuinsert signature au online signature. Ukifanya hivi imekula kwako, print isaini kwa mwandiko wako na iscan tena.
- Scanning isiyo na viwango, wale wazee wa kumalizia kila kitu kwenye smartphone. Karatasi imejikunja na chafu Halafu unascan kwa simu yako inaacha water mark za "scanned by cam scanner". hauko serious mjuba.
- Vyeti vyako havijahakikiwa na advocate, na cha kuzaliwa hakijahakikiwa na rita. Hii najua kwenye maelekezo yao hawajasema ila nlikosa usaili kisa hiyo sababu. Nimeamabatanisha na screenshot ya ushahidi ili tomaso uamimi.
Wanaoomba ni wengi, kutakuwepo na vigezo vya ajabu vya kukutoa nje ya reli. Ni heri mkakutane Dodoma kwenye mnyukano ukose kuliko kuishia njiani.
Kama una vidokezo vingine ongezea hapa wadau wajue.