Angalizo kwa BOT baada ya riba za mikopo kuanza kushuka

Angalizo kwa BOT baada ya riba za mikopo kuanza kushuka

Mimi binafsi nampongeza RAIS lakini kwa kiwango kidogo sana, naona bado punguzo lake halijaathiri wananchi wengi wa nchi hii. Kwasababu kukopa siyo jambo la lazima, mtu anaweza kukopa na mtu akiamua anaweza hasikope. In short ni jambo la kujitakia mwenyewe.

Mimi nitampongeza RAIS moja kwa moja kama ataamua kupunguza makato ya wafanyakazi, kwa kweli hayo makato yanaturudisha sana nyuma wafanyakazi, inafika mpaka asilimia arobaini (40%) ya makato ya mshahara wetu, kwa kweli hiki kitu kinaumiza sana na kinarudisha sana nyuma. Ishu ya mkopo ni ishu ya kujitakia siyo jambo la lazima, afanye hili la lazima ambalo hatuwezi kuliepuka kuliko huo mkopo.
 
Hata mimi kwa hili namuunga mkono Raisi wetu...
 
Kwaiyo kupunguza riba kwa mkopaji kwa nchi masikini kama yetu haiwezekani?
sio kwamba haiwezekani ila ni ngumu maana uwezo wa watu kuweka akiba ni mdogo na akiba ndo inakopeshwa. kama benki zinapata pesa za kukopesha kwa riba kubwa jumlisha gharama za uendeshaji biashara zilivyojuu unadhani kukopesha kwa riba ndogo ni rahisi. Riba ni bei ya bidhaa kama bei ya chungwa tu huwezi nunua chungwa shilingi tano uuze shilingi tano lazima uweke kiwango cha faida na gharama za biashara.
 
MTAZAMO asante kwa kuja na hii thread.

Kipindi cha Kikwete, biashara zilishamiri sana, wafanyabiashara wengi walikuwa wanakopa na kurudisha inavyotakiwa, Magufuli alipoingia akaanza kuwabana wafanyabiashara, sekta binafsi ikaonekana ni adui wa maendeleo ya taifa kuelekea uchumi wa viwanda, TRA wamehusika kuua biashara nyingi sana, naamini wengi ni mashahidi wa hili.

Benki zilianza kutangaza NPL (Non Performing Loans) kwa rate za ajabu, tumeona benki kadhaa zimeshindwa kujiendesha na zimeondoka sokoni, benki nyingi faida zinashuka kila kukicha, wafanyabiashara hawakopi tena kwa kiwango kile, hawana uhakika wa kurudisha.

Securities zimeshuka thamani, nyumba iliyowekwa bond (security) ambayo back then ungepata 150Mil sasa hivi unaweza usipate hata 100M, je kama huyo mtu alikopa 120 Mil, si ni hasara kwa benki?

Baada ya benki kuona wafanyabiashara hawakopi, hawakopesheki, wamehamia kwa wafanyakazi (sekta waliyokuwa wanaidharau kipindi kile), sasa kila benki inakimbilia kupunguza rate kwa wafanyakazi, CRDB wamechochea zaidi kwa kufanya Public Announcement, benki nyingi zilianza kutuma taarifa kwa makampuni kimya kimya.

Kwangu sioni kama kuna la kumpongeza Mkuu.

Angalizo kwa mabenki: Hii mikopo ya wafanyakazi haina dhamana, dhamana ni sahihi ya mwajiri tu. Kadri siku zinavyoenda makampuni mengi yanafanya retrenchment, na kuna wafanyakazi wengi watakuwa wamechukua mikopo ambao watakuwa laid off, hivyo benki zitegemee NPL zingine.

Angalizo kwa Wakopaji: Kuna watu wengi wataingia kwenye mkumbo wa kukopa kwa vile tu riba zimeshushwa, unapokopa bila plan ya nini ukafanyie hela itaisha na utabaki na maumivu ya makato kwa kipindi chote cha miaka ya makato, pia wengi tutasema ngoja nikope nikafanyie biashara, biashara ni ngumu sana kitaa, biashara zinakufa, bomoa bomoa zimekuwa nyingi, unajenga duka Magu anapita na Greda.
 
hakuna tofauti unlesa kama unamuhama anayetumia formula ya FLAT RATE kama WAHUNI BENKI YA DAR ES SALAAM - DCB eti wanajeshi wanawapa REDUCING, raia tunapewa FLAT RATE! tunabaguana wenyewe kwa wenyewe , hata wazungu wanatucheka
Hao ni wabinafsi, double standard ya wenyewe kwa wenyewe ni ubaguzi wa kikaburu! Walaaniwe na wateja waikimbie bank hiyo!
 
Safi sana mleta hoja ana hoja nzuri...hongera Mheshmiwa Rais Dr. JPM na serikali ya awamu ya tano kwa kuliona ili tatizo la riba kubwa kwa mikopo hususani kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa kipato cha chini
Wakati anaingia makampuni /taasisi nyingi interest ilikuwa kati ya 15% hadi 20%, yeye akafanya ya kufanya ikapanda hadi kufika 25%, hivyo kushuka kufikia 17% haihitajiki pongezi kwake. Kwani ameturudisha tulipo kuwa. Labda tumlaumu kwa kukutesa kwa kipindi takribani miezi 36
 
Mimi binafsi nampongeza RAIS lakini kwa kiwango kidogo sana, naona bado punguzo lake halijaathiri wananchi wengi wa nchi hii. Kwasababu kukopa siyo jambo la lazima, mtu anaweza kukopa na mtu akiamua anaweza hasikope. In short ni jambo la kujitakia mwenyewe.

Mimi nitampongeza RAIS moja kwa moja kama ataamua kupunguza makato ya wafanyakazi, kwa kweli hayo makato yanaturudisha sana nyuma wafanyakazi, inafika mpaka asilimia arobaini (40%) ya makato ya mshahara wetu, kwa kweli hiki kitu kinaumiza sana na kinarudisha sana nyuma. Ishu ya mkopo ni ishu ya kujitakia siyo jambo la lazima, afanye hili la lazima ambalo hatuwezi kuliepuka kuliko huo mkopo.
Pambana na hali yako au acha kazi
 
Wavifunge speed gavana hivi vi micro finance
Wamama wa uswahilini watauana na izo Microfinance.
Walikuwa wanakopa, ikifika kipindi cha marejesho wanaenda kujiuza kwy baa na mahotel ili kupata iyo pesa
 
Wamama wa uswahilini watauana na izo Microfinance.
Walikuwa wanakopa, ikifika kipindi cha marejesho wanaenda kujiuza kwy baa na mahotel ili kupata iyo pesa
Kujiuza ni tabia tu, km ulikopa ili uanzishe business inayolipa in time huna haja ya kujiuza, ila kukopa kwa mkumbo ndo watu wanauziwa vitu vyao, kopa fanya business, shilingi itakayotumika kutofanya kazi iliyokopewa lazima ije ikupe mzigo mwishoni, kwan hatuoni mtu anakopea hela ya kibiashara afu anatumia kidooogo kifamilia au hata kibinafsi
 
Back
Top Bottom