Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

Hahaha paskali nashukuru kwa maoni yako. Lakini kumbuka na hawa watawala wanasahau dhana ya uongozi na kuwa watawala. Na hiyo tu haitoshi hujifanya miungu watu. Kumbuka sisi wananchi huwa tuna matamanio/wishes zetu. Tukimpata kiongozi na kweli akatenda tuliyotarajia na ni mazuri na impact yake ikawa positive na kuonekana, basi huwa tunasifu. Lakini tukipata watawala badala ya viongozi na wakatufanyia tusiyoyapenda kwa manufaa yao, basi sisi huwa tunalaani,tunalalamika na as a result tunaomba mabaya yawakute. Lakini kumbuka tunaomba hatuhukumu; mtoa hukumu ni mungu labda na mamlaka zake. Hivyo unapotuonya sisi siku zingine uwe unawaonya au kuwakumbusha watawala wawe viongozi na waonyeshe leadership sio utwana.
Nakubaliana nawe tusi hukumu wengine lakini kumbuka we act that way baada ya kuona hatutendewi haki au watawala hawatendi haki. We always act out of anger not in our normal sense. Tuhurumie na endelea kutuombea tupate busara tunapoonyesha reaction zetu. Andiko lako ni zuri kwetu, naomba hao watawala uwatafutie lao pia. Uungu mtu, kutudharau beada ya kukabidhiwa ofisi zetu. Na kutuona maadui ili hali sisi ndio tuliwapigia kura.Hata kama huwa hawapendi demokrasia ya kuchaguana lakini ndio mfumo halali uliopo. Hata wakiteuliwa waheshimu wananchi. Pongezi kwa onyo na maoni yako kwa wanajamii forum.
 

1 Kings 22:8
The king of Israel answered Jehoshaphat, "There is still one prophet through whom we can inquire of the LORD, but I hate him because he never prophesies anything good about me, but always bad. He is Micaiah son of Imlah." "The king should not say such a thing," Jehoshaphat replied.

Nadhani unajua nini kilimkuta mfalme Ahabu mwishoni ??
 
Hili bandiko linakuhusu
P

Anachotufanyia huyu mtu yaani dua mbaya zangu kwake.

Tunachanga hela kwa ajili ya kujenga barabara, shule, kituo cha afya wakati tunalipa kodi alafu anatuambia tusubirie apeleke maendeleo kwingine huoni hiyo ni hujuma kwetu walipa kodi
 
Mtu aliyefirisika kimawazo ndiyo awezaye kumtabiria mtu kifo, ili aogopwe. Kifo huja kwa njia mbalimbali hivyo, kifo siyo kitu cha kutishia mtu. Labda mambo mengine, kama mikosi na laana.
 
Mtu aliyefirisika kimawazo ndiyo awezaye kumtabiria mtu kifo, ili aogopwe. Kifo huja kwa njia mbalimbali hivyo, kifo siyo kitu cha kutishia mtu. Labda mambo mengine, kama mikosi na laana.
Kwa kuwa sii kitu cha utishia basi semeni anakufa lini tuandae sherehe!?
 
Sidhani kufa ni adhabu.
Km unajua kufa inamaanisha nn basi huwezi ogopa kufa.

Anayeogopa kufa ni mwovu.
Ingawa si vema kutabiria Mtu atakufa

Kifo ni adhabu maana kuna wanaokufa kifo cha mateso makubwa na kuna wale wanakufa wanatabasamu na kumsifu Mungu huku jamaa wakivuta roho.

Kuna vifo ni adhabu kubwa maana wale malaika watoa roho huja kwa kasi ya ajabu na kufanya vurumai kugombania roho yako.

Malaika watoa roho wengine hukuuliza kabisa wapi unataka waanzie kuvuta roho iwe miguuni au sehemu nyingine za mwili wako.

Ndo maana kuna watu wanakufa kifo cha taratibu na kisicho vurumani kutokana na kukumbuka kufanya maombi kusamehewa ubaya wake alotenda duniani.

Na kuna watu wanakufa kifo kibaya sana maana kinakwenda taratibu mno kutokana na ukatili na roho mbaya wa mkata roho.

Hivyo kifo ni adhabu kama vile viboko kama wachapwa fimbo mbili kwa upole au watandikwa khasa bakora 6 lakini usije kaa wiki mbili.

Mimi nimepata habari hii kutoka kwa washauri wangu wa masuala ya dini au walihi na makasisi walobobea.
 
Kumbe umepata mafundisho ya dini?

Basi hatuwezi elewana
 

Well said, mkuu; mwenye sikio na asikie.

Katika maisha yangu ya miongo kadhaa, sijawahi kukutana na mtu mwenye mafanikio makubwa ambaye brain yake imejaa negativity!
 
Hata kwenye hii sintofahamu iliyojitokeza, manabii wa majanga, hawakosekani, baada ya kumshuhudia live ikulu, sura zao zimewashuka.
P
 
Ilikuwa lazima hili litokee kwa sababu kuna watu wanaishi bila kujulikana lakini taarifa zao zinaishi na zinaaminiwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…