Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

:Nikuulize swali,hivi hitler angekuwa bado yupo hai ungemuombea azidi kuishi mkuu?

Hii dunia sio rahisi kama unavyoifikiria!

Ni hivi... Ukishindwa, you lose everything, including yale mema na mazuri ambayo dunia ingejivunia. Mshindi ndiye anayetoa definition ya utu na thamani ya utu wako kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.

Hitler angeshinda vile vita, hakika mambo yote ya ovyo tuliyosomeshwa na kuaminishwa juu yake yasingekuwepo, kwa sababu dunia ingelishwa kile ambacho kingemweka Hitler kwenye nuru njema!
 
Ni wapi malaika mtoa roho anaitwa Israel katika Biblia Mayala? Maana hilo neno ni la chuki na propaganda za watu wenye chuki na Israel mbona mi hukuona we mtu smart unaingiaje kwenye mtego wa chuki hivyo?

Wanabodi,

Huu ni wito wangu kwa wana jf wenzangu, Tuwaepuke "Manabii wa Majanga", Prophets of the doom" ambao kazi yao ni kuwanyooshea vidole wenzao na kuwahukumu pasipo uthibitisho, kila kunapotokea tukio baya, na kuwaombea wenzao majanga ikiwemo kuwatabiria kifo. Unapomuombea janga mwenzako, wewe bila kujua, kumbe ndio unajichumia janga kwako au kwa uwapendao as a karma reaction kwa mabaya uliomuombea au kumtabiria kifo mwenzako kwa kutumia kanuni ya tatu ya Newton law of motion isemayo "every force has equal and opposite reaction, pulling towards that force", yaani kila jema unalowaza, unalopanga, unalosema na unalotenda kwa wengine, litatengeneza karma nzuri ya mema (positive good karma power) ambayo mema hayo uliowaza, uliopanga, uliosema na uliotenda,yatakurudia wewe na kizazi chako, na kila janga,unalowaza, unalopanga, unalosema, unalotenda kwa wengine, linategeneza karma mbaya ya majanga (negative bad karma power) hivyo majanga hayo yatakurudia wewe na uzao wako!. Tusiwaombee wenzetu majanga, ili tusijichumie majanga!.

Wito huu ni kufuatia kuongezeka kwa threads ambazo haziliombei mema taifa letu na viongozi wake na nyingine kuwaombea hadi vifo wale tunaowahisi ni wabaya wetu. Kwa dini zote, amri kuu kuliko zote ni upendo, kwa jinsi ile Mungu alivyotupenda sisi hadi.... vivyo hivyo nasi tupendane, hata adui mpende, kama ni adhabu, adui yako ataadhibiwa na Mungu kupitia karma ya matendo yake!.

Kauli huumba, hivyo tusishabikie sana kauli zenye negativity na kujikuta kumbe ni sisi tuna sababisha hizo negatives kwa kuziumba kwa kauli zetu. Badala yake tuwe positive kwenye kila jambo, hata tukihisi jambo fulani sio jema, tutumie kitu kinachoitwa affirmatives kubadili negatives kuwa positives.

Miongoni mwa kauli hizi za hawa Prophets of the doom wa humu jf, ni pamoja na kuwatabiria vifo vya ajabu ajabu viongozi wetu!. Tusishangilie majanga yoyote kwa binadamu wenzetu, hata hawa viongozi wetu sio miungu watu hawa ni binadamu tuu kama sisi hivyo hata wakiwa ni watu wabaya kiasi gani, hata wakiwa na mioyo ya kishetani kiasi gani, hata watutendee maovu kiasi gani, sisi tuwaombee tuu mema, tuwaombee mafanikio na kuwaombea afya njema na waishi maisha marefu hapa duniani na sio kuwaombea kifo, halafu kama kuna maovu wameyatenda, sisi tusiwahukumu, tusije tukahukumiwa, kazi ya kuwahukumu kwa matendo yao, tumwachie Mungu mwenyewe ambaye ndiye Hakimu Mkuu, na hukumu yake ni kupitia kitu kinachoitwa karma, ambapo kila mmoja wetu atahukumiwa kwa matendo yake, ukitenda mema, utalipwa mema, ukitenda uovu au ubaya, utalipwa uovu au ubaya!.

Ila maisha yameumbwa na kifo pia kumeumbwa, kila mtu ni lazima atakufa siku yake ikifika tena atakufa kifo kile kile alichopangiwa na Mungu ile siku anazaliwa, hivyo tusimtabirie yoyote kifo, tusimuombee yoyote kifo, uhai na kifo ni chini ya mamlaka ya Mungu pekee na sio sisi binadamu.

Haijalishi mtu atakufaje, ila malaika mtoa roho Israel humpitia kila kiumbe humu duniani mara 7x 70 ( saba mara sabini) kila siku ili kuhakikisha saa yake ikifika, hazidishi hata nukta moja ya sekunde, kifo ni kazi ya Mungu hatuna haja kutabiriana vifo humu na wengine hadi kuombea vifo wengine, kwa kufanya hivyo wengine bila kujijua kuwa kumtabiria mwenzako kifo au mabaya ni kujiombea wewe mwenyewe kifo au mabaya hayo kwa kanuni ya karma ya what goes around, comes around kwa kufuata kanuni ya Newton ya every action, there is equal and opposite reaction.

Haijalishi mtu atakufaje, ila kwa yoyote na vyovyote atakavyokufa, kifo hicho ndicho alichoandikiwa na ndicho kilichopangwa ile siku anazaliwa, kwa sababu kuzaliwa na kifo ni mipango ya Mungu pekee. Hata shetani akipanga mipango miovu vipi, kama Mungu hajaridhia, hata wapange vipi, kamwe hawatafanikiwa, kila binadamu atakufa saa ile tuu aliyoandikiwa na kifo kile tuu alichopangiwa kwa mipango ya Mwenyezi Mungu pekee.

Tupendane, tuombeane mema hata maadui zetu, tuwaombee mema hivyo kutengeneza positive karma effects.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...

Wasalaam.
Paskali
 
Hata kwenye hii sintofahamu iliyojitokeza, manabii wa majanga, hawakosekani, baada ya kumshuhudia live ikulu, sura zao zimewashuka.
P
Pascal hii Nchi ina watu wa ajabu sana Kaka yangu. Mpaka Zitto Kabwe alikuwa kwenye mkumbo huo. Baada ya kupata za chini chini kuwa Mh. Anapiga mzigo kama kawaida akajifanya kanukuliwa vibaya. Ni hatari sana kuwa na watu wanaojidai kuusaka uongozi wenye akili kama Zitto. Ukweli nimefurahi sana kumuona Mkuu live. Ningekuwa mnywapombe ningekesha. Mungu ampe maisha marefu.
 
Pascal hii Nchi ina watu wa ajabu sana Kaka yangu. Mpaka Zitto Kabwe alikuwa kwenye mkumbo huo. Baada ya kupata za chini chini kuwa Mh. Anapiga mzigo kqmq kawaida akajifanya kanukuliwa vibaya. Ni hatari sana kuwa na watu wanaojidai kuusaka uongozi wenye akili kama Zitto. Ukweli nimefurahi sana kumuona Mkuu live. Ninvekuwa mnywapombe ningekesha. Mungu amoe maisha marefu.
Mkuu Nyangomboli , watu wanaomuombea mema Rais Magufuli ni wengi kuliko wanaomuombea mabaya, sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, Mungu atamlinda na kumpa maisha marefu, ila na yeye kama ana yake ya kustahili adhabu ya karma, muda wake ukifika karma itakula tuu kichwa, dawa ya kuepuka adhabu ya karma ni kutenda mema.
P
 
Ni wapi malaika mtoa roho anaitwa Israel katika Biblia Mayala? Maana hilo neno ni la chuki na propaganda za watu wenye chuki na Israel mbona mi hukuona we mtu smart unaingiaje kwenye mtego wa chuki hivyo?
Mkuu Chizi Maarifa, jee unayajua majina ya malaika wangapi waliotajwa kwenye bible na unazijua kazi zao?.
P
 
Wengi ndugu yangu. Akina mikael,gabriel n.k ntajie wewe israel ulimsoma kitabu gani katika biblia kuwa ndiye mtoa roho ili nami nafsi yangu ielimike...maana yawezekana nikawa maamuma katika hilo.

Mkuu Chizi Maarifa, jee unayajua majina ya malaika wangapi waliotajwa kwenye bible na unazijua kazi zao?.
P
 
Wengi ndugu yangu. Akina mikael,gabriel n.k ntajie wewe israel ulimsoma kitabu gani katika biblia kuwa ndiye mtoa roho ili nami nafsi yangu ielimike...maana yawezekana nikawa maamuma katika hilo.
Kwenye Bible, wametajwa kwa majina, malaika wanne tuu, Luciferi, Mikaeli, Gabriel na Rafael, jee kwa vile Bible imewataja hao wanne, ndio inamaanisha malaika wa Mungu wako wanne tuu?.
P
 
Umeanza kuogopa kifo mkuu? Nlikuona jana, naona kaumri kamesogea sogea!!

Anyway, muda na wakati wa sisi kurudi mavumbini ni Siri ya Mungu na watendaji wake. Kinachotokea hadi kuombeana mabaya ni chuki tu za kibinadamu. Uzuri mmoja, Mungu hashawishi au kuendeshwa na hisia za mwanadamu
Nani alikudanganya kifo kina umri?
 
Je kwa kuwa hawajatajwa wengine inamaanisha tunaweza watunga wengine? Maana kama neno malaika limetoka kwenye Biblia na ukasema wametajwa wanne. Nawe ukazungumzia biblia na characters wanaohusika na biblia.huyo israel mtoa roho umemtoa kwenye kitabu gani kinachohusiana na biblia.

Katika ukristo kuna malaika wengi. Nikutajie some names.
1. Gabriel
2. Rafael
3.abaddon
4. Ariel
5. Daniel
6. Azazel
7. Barachiel
8. Camael
9. Cassiel
Na wengine zaidi. Malaika hao wapo kwa mujibu wa Dini kuu tatu.
1. Kikristo
2. Kiyahudi
3. Kiislamu

Kwa upande wa Mashariki ya kati. Katika Ukristo hakuna malaika Israel/azrael. Huyo ni malaika kwa upande wa waislamu ambao nao wana dini yao na Mungu wao. So unapozungumzia uislamu ni sawa wana malaika wa kifo kwa jina la azrael. Kwa wakristo hayupo.

Kwenye Bible, wametajwa kwa majina, malaika wanne tuu, Luciferi, Mikaeli, Gabriel na Rafael, jee kwa vile Bible imewataja hao wanne, ndio inamaanisha malaika wa Mungu wako wanne tuu?.
P
 
My brother pascall, we were not happy coz of our plane being detained in south africa, no no no, we were happy coz this awamu ya tano thinks that they are clever than even God himself, i can tell you pascal my brother for free, lots of us will be more than happy if God sends this person(you know who i am talking abaut) to hell fire where he RIGHTFULLY BELONGS.
Mkuu THE SEAL, Hiyo wish inakuingiza kwenye kundi la prophets of the doom.
P
 
Hiyo wish inakuingiza kwenye kundi la prophets of the doom.
P
So you are oky with what this dictator is doing to our country that has known peace and such things since the time we got uhuru till 2015 when this hitlers brother took power?????? if you put me in the category of prophets of doom so be it, if you were azorys brother, tundu lissu cousin, ben saanane uncle, on and on, i doubt if you could call me a prophet of doom, but i respect your opinion, noting very well that OPINIONS are not TRUTHS,
 
Mkuu sikuionaga hii thread miaka yote!

Ulilenga kuhimiza upendo na kutendeana mema wakati huo ukijenga hoja fikirishi pia, saazingine wewe binafsi bila kujua.

Ulisema kuwa mtu atakufa siku ile ile, saa ileile, sekunde ile ile na aina ya kifo kilekile alichopangiwa na Mwenyezi Mungu.

Maelezo hayo tu ndiyo mimi nimeona ni kama maelezo tata!

Hivi kwa mfano, vifo vya kutisha vinavyosababishwa na binadamu wengine, kama vile kuuawa kikatili kunakotokana na uonevu au ujambazi, utasema aina hii ya vifo ni mapenzi ya Mungu na kwamba mtu yule kaandikiwa na Mungu afe kifo cha aina hiyo?

Iweje sasa wasababishaji waonekane kuishika masharubu serikali, pia iwe ni dhambi ya mauti katika amri za Mungu mwenyewe?

Embu jaribu kuliweka hili vizuri, ili twende pamoja mkuu.
 
Tumia ulimi wako vizuri. Unapomuombea Dua mbaya binadam mwenzio, kama si sitahiki kwake basi ujue Muumba wetu anaigeuza inakuja kwako mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mr.Mak , Naunga mkono hoja na hili nimelisema humu.

Wanabodi,
Unapomuombea janga mwenzako, wewe bila kujua, kumbe ndio unajichumia janga kwako au kwa uwapendao as a karma reaction kwa mabaya uliomuombea au kumtabiria kifo mwenzako kwa kutumia kanuni ya tatu ya Newton law of motion isemayo "every force has equal and opposite reaction, pulling towards that force", yaani kila jema unalowaza, unalopanga, unalosema na unalotenda kwa wengine, litatengeneza karma nzuri ya mema (positive good karma power) ambayo mema hayo uliowaza, uliopanga, uliosema na uliotenda,yatakurudia wewe na kizazi chako, na kila janga,unalowaza, unalopanga, unalosema, unalotenda kwa wengine, linategeneza karma mbaya ya majanga (negative bad karma power) hivyo majanga hayo yatakurudia wewe na uzao wako!. Tusiwaombee wenzetu majanga, ili tusijichumie majanga!.

Tupendane, tuombeane mema hata maadui zetu, tuwaombee mema hivyo kutengeneza positive karma effects.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...

Wasalaam.
Paskali
P
 
Back
Top Bottom