Pascal Mayalla ni kweli chadema inahitaji fresh blood ila sio Mwambe,CHADEMA inahitaji fresh blood kama Tundu Lisu ila walichokifanya sio kibaya ni maandalizi ya Tundu lisu kuongoza jahazi
Pascal alichofanya ni akili ya juu mno katika kujaribu kuasa wapiga kura.
Jee wapiga kura watakuwa hawajitambui na kuona kuwa katika mitikisiko ya kukiua chama hakikufa? Nani alipambana kisife wakati huo hadi sasa?
Na jee huyu mgeni ndani ya chama wa chini ya miaka 4 iweje aje na kufikiria kuwa yeye anauwezo wa kukamata nafasi ya juu kabisa ili kukiponya chama chake kipya dhidi ya chama chske cha zamani ambacho majuzi mwenyekiti wake amesema Mwambe anakipenda sana na alifanyiwa mizengwe tuu akaondoka?
Ni sawa na unataka kuoa mke aliyemuacha mumewe sio kwa vile hampendi bali gubu la mawifi ndio limemuondoa huko. Akikutana na mumewe wa zamani chocho basi ni mahaba "kama yote"
Mkuu usipoteze muda wako na huyo Pascal bali kumbuka maneno ya Mbowe kuwa uchaguzi huu Rushwa imekuwa tatizo sana na moja wa hao waliokula anaweza kuwa yeye Pascal au huyo anayepigiwa debe Mr Mwambe...binafsi Mwambe ni very Jr kubeba mikoba ya Mwenyekiti Taifa kama sio kuua chama, huyo bwana hata alikotokea wanachama wengi hawamjui ila pesa ya kununua wanachama anayo kapata wapi pesa hiyo kama hajapewa na aliyemlipa Pascal? huyu Mayalla anadai eti Mbowe kakaa sana kwenye uongozi bila kuleta maendeleo na sasa basi panahitajika badiliko lakini mtu huyohuyo anashindwa kusema kuwa CCM imekaa sana kwenye uongozi mpaka sasa inashindwa kumlipa hata mkulima wa Korosho, kumbe kweli mchawi hana usiku wala mchana
Mkuu Mayala umegusa ninapo pataka naki kwenye mtizamo kuna Jambo nataka kuweka.
Lolote kati ya mawili haya litakiimarisha chama; mosi iwapo wajumbe kwa utashi wao tu pasi kushawishiwa wakamwambia iwa sauti ya kimya kimya Mfalme muda wa kupumzika umefika.
Na pili iwapo Mbowe, aliamua kufuata taratibu zote za kujaza na kurudisha fomu, ili ionekane namna demokrasia ilivyo tamalaki ndani ya chama na ndio maana wajumbe wakamchagua Mwambe na ulimwengu ukawaelewa hivyo itakua ni milage kubwa sana kwa chama.
CHAMA KITAIMARIKAJE?
Kwanza watakua wamefanikiwa kufanya demage control kwa yale aliyoyasema Prof. Safari na Mh. Waziri Mkuu mstaafu Tuluway Sumaye.
Pili chama rasmi kitaifikirisha upya jamii juu ya community pendwa ya wachagga, Jamii itafuta ule unadharia wa Kuuwawa kwa Chacha Wangwe na kutimuliwa mbali wale mapacha watatu ZITTO, SAMSON NA PROF. MKUMBO.
Muda ni rafiki adhimu hasa katika siasa za nchi hii.
Pascal watu wazima hawadanganyani mimi nakujua na wewe unanijua ila sema tu sivizuri kuanza kutambulishana, wewe umeamua kuwa verified user sawa ila tukikutana tunafahamiana vizuri tu.
Mkuu Mmawia, kiukweli wengi humu tunajuana kupitia jf tuu lakini hatujuani in reality, mimi ni very real, sijawahi kuwa CCM, hata wakati nikimpigia debe EL, sikuwahi kuwa CCM wala sijawahi kuwa Team Lowassa, na hata Lowassa alipohamia Chadema, sikuwahi kuwa Chadema, na sasa ni kweli poti wangu ndio yuko kunako, bado sijawahi kuwa CCM, ila tunanokwenda...
P
Pascal watu wazima hawadanganyani mimi nakujua na wewe unanijua ila sema tu sivizuri kuanza kutambulishana, wewe umeamua kuwa verified user sawa ila tukikutana tunafahamiana vizuri tu.
Mkuu Mmawia kwanza nakubaliana na wewe kuwa kuna wana jf tunajuana in real names na tunajuana kuwa wote ni wana jf lakini hatujuani nani anatumia pen name gani, mimi mwenyewe my two kids are jf members and I don't know the names they use, hivyo inawezekana kabisa mimi na wewe tunajuana in reality, hivyo ningekuomba kuwa mkweli na muwazi kuhusu mimi, jee unavyo nijua in reality mimi nina chama chochote?.
P
Mayalla nilikuwa nakuaminia Sana na kusoma makala zako, Ila kwa sasa unaangalia tumbo lako zaidi kuliko kusimamia haki. Endelea tu utaupata ukuu wa wilaya.
Wanabodi, Hili ni bandiko la swali tuu, Ili uchaguzi wa 2020 usiwe ni igizo tuu la uchaguzi, Je tumchagize na kushinikiza Tundu Lissu ndiye asimamishwe na upinzani kumkabili John P. Magufuli? kwa sababu mpaka sasa, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana...
Mkuu Mmawia kwanza nakubaliana na wewe kuwa kuna wana jf tunajuana in real names na tunajuana kuwa wote ni wana jf lakini hatujuani nani anatumia pen name gani, mimi mwenyewe my two kids are jf members and I don't know the names they use, hivyo inawezekana kabisa mimi na wewe tunajuana in reality, hivyo ningekuomba kuwa mkweli na muwazi kuhusu mimi, jee unavyo nijua in reality mimi nina chama chochote?.
P
Mkuu Ndumbayeye, binadamu tunatofautiana uwezo na uwezo, mwingine ni mzuri katika kupanga mikakati, mwingine ni mzuri kwa kusema sana, mwingine kwa kuhutubia, mwingine kwa ushawishi etc, na ili kufanikiwa lazima hawa watu wenye uwezo tofauti to work as a team. Chadema ilikuwa na team nzuri, mfano Zitto ana very big convincing power, JJ.Mnyika ni researcher mzuri kujimba data, Lissu ni very powerful speaker, Prof. Kitila Mkumbo ni good strategist, team ya Chadema ilikuwa ikikiwasha kinawaka kama ile list ya mafisadi ya Mwembe Yanga au Moto wa Buzwagi Bungeni. Baada ya kumtimua Zitto, JJ.Mnyika now is nothing, baada ya kumtimua Prof. Kitila Mkumbo, kwa upande wa strategies Chadema is zero kwasababu hamna mtu kama Zitto wala Kitila na Zitto kule kwake pia he is nothing kwasababu kuna viungo hana.
Usidharau mtu, mimi kwangu hadi mfagizi ni muhimu na home hadi beki tatu ni muhimu, tena ma beki tatu wanaokoaga majahazi usipime ila watu hawapendi tuu kufunguka kama ambayo jf tunavyo isaidia sana serikali hii ya Magufuli lakini hatutajwi na badala yake ni serikali kutufungulia mlolongo wa makesi, na sisi individual members tunaojulikana ni wana jf, cha moto tunakipata kwa vibano kwenye shughuli zetu
P
Pascal Mayalla,
We Paskali acha unafiki, wakati CDM inahujumiwa waziwazi huwa upo kimya, CHADEMA na wapinzani wamefungiwa kufanya siasa karibu mwaka wa 4 sasa wakati Katiba na Sheria ya nchi inaruhusu mbona kalamu yako hatujawahi kuisoma ikiandika uonevu huo.
Unajua kwamba CHADEMA ni taasisi inayojitambua, Kiongozi mkuu wa taasisi ndiyo mboni ya taasisi husika, kuna vetting lazima ifanyike before na pre-agreement nzito na bodi nzima ijiridhishe kwamba huyo anayetaka kuongoza taasisi kashiba nondo, viatu vinatosha na anaendana na philosophy ya taasisi husika.
Sasa huwezi kulala ukaibuka ati unataka kuongoza CRDB benki kisa una Masters ya Uchumi na CPA, hapana mambo huwa hayaendi hivyo.. unajua kila kitu ila kwa sababu unapenda kuandika kuhusu CHADEMA in negative well and good.
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavua, kiukweli sisi wazee hatuupendi kweli uzee due declining stage. Hata mimi mimi baada ya kukata 50+, nywele inapoanza kupiga bati wengi wetu ama wananyoa vipara au wanapiga black, wajukuu walipoanza kutokekelezea na kuitwa babu nikaanza kuona noma, nawambia bora mniite grandpa ni afadhali kidogo kuliko babu!. Rounds zilipoanza kupungua kutoka doze ya 3 kwa siku, daily siku zikaanza kupungua zikianzia 3 times a week, 2 times a week sasa only once a week tena round yenyewe moja, kiukweli unaanza kukosa amani na kuhusi kusaidiwa.
Uzee usikie hivyo hivyo, wakati wazee kwa wenzetu wanajipumzikia, huku kwetu wazee ndio they want more!.
Hakika nimefurahishwa sana na Mwandishi huyu Pascal Mayalla wa kipekee aliyemuuliza swali Rais lenye msingi na hata rais kajibu kwa ubabaishaji. Natafuta clip au mwenye nayo aiweke. Kwanza kaanza kwa kuitaja JamiiForums kwa kusema ni mwanachama mwandamizi wa JamiiForums. Hayo yameelezwa na...
Mkuu Mmawia, wewe usicheke bali funguka tuu kama Paskali humu jf anajifanya hana chama huku in reality huwa akionekana ku randa randa viunga vya Lumumba wewe sema tuu.
P
Pasco, ninakuiheshimu sana na wewe ni moja ya role model wangu, ila sasa umeanza kuwa mnafiki na muongo mkubwa. Kwanini?
CHADEMA kitakufa sio sababu ya uongozi mbovu ni kwa sababu hakuna FAIR GROUND.
CHADEMA ikifa ni hasara kubwa kwa Taifa sio Mbowe wala Lisu. Kumbuka wakati wa kudai katiba mpya kuna wana CCM walipinga ila sasa wanaugulia maumivu makali.
Wanabodi,
Kichwa cha habari cha bandiko hili kinajieleza wazi, hili likiwa ni bandiko la swali, kuwa Siku Zote Huwa Nailaumu Chadema Kuwa Hawajitambui na Hawajui Wanataka Nini!. Sasa Kesho Chadema Wanafanya Uchaguzi wa Mwenyekiti, Swali ni Jee Sasa Chadema Wanajitambua?, Jee Wanajua Wanataka Nini?...
Katika Uchaguzi wa Kesho wa Mwenyekiti wa Chadema, Kama Chadema Wanajitambua, Watachagua Kuishi, Lakini Kama Bado Hawajitambui Kama Kawaida Yao, Watachagua Kifo!.
Swali ni Jee Chadema Kuchagua Kifo au Kuishi?. Tusubiri Hiyo Kesho Tuone...
Naanza Bandiko Hili na Declaration, Kisha Naleta Justification
Naomba kuanza kwa declaration of interest, mimi Paskali wa Jeiefu, sio mshabiki, mfuasi, au mwanachama wa chama chochote cha siasa, lengo la declaration hii ni kwa ajili ya manazi wa Chadema waliotamalaki humu JF, ambao ukichangia jambo lolote ambalo hawalipendi, watakushukia kwa kukubeza, kwa vile wewe sio Chadema, mambo ya Chadema, yanakuhusu nini?!, hivyo maneno kama "pilipili usioila inakuwashia nini?" hayawezi kukosekana. Naamini kuna Watanzania wengi kama mimi ambao sio wanachama wa chama chochote cha siasa, na kuna wanachama wa vyama vya siasa ambao wako very objective kwa maslahi ya taifa wakiwemo wana CCM ambao wangependa kuona, nchi yetu inapata credible opposition, kwa huku Bara, Chadema ndicho chama pekee kilichoonyesha angalau kinaweza, ila baada ya kutokea huyu game changer aliyabadili the political game, Chadema imeporomoka na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kama Chadema hawatafanya the right thing now, they are going to be reduced to nothing. Chadema ikifa, sio hasara kwa Chadema na wanachama wa Chadema tuu, ni hasara kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla kwa nchi kurejea chini ya mfumo wa chama kimoja which is not good at all kwa majaaliwa ya mustakabali wa taifa letu.
Justification
Kuna justification kubwa moja kwa mtu ambaye sio Chadema kujadili mambo ya Chadema. Chadema kwa vile ni chama cha siasa na kina wanachama, kuna watu wanadhani Chadema ni private party, interms of usajili na kujiunga hivyo ni mali ya wanachama na viongozi wao pekee, no!, Chadema is a public party, nichama cha umma wa Watanzania, na kinaendeshwa kwa kugharimiwa na tax payers money, hivyo ni public party, kwenye kitu kinachoitwa "private property no right to trespass", hii maana yaye ni mali ya mtu binafsi ina kinga ya kisheria ya kutoingiliwa, na hata katika mienendo na maisha binafsi ya watu wakiwemo viongozi, kuna kinga ya kifaragha, "the right to privacy" ambayo haipaswi kuingiliwa, lakini mtu yoyote, au taasisi yoyote inayolipwa with tax payers money, inapoteza hizo kinga zote mbili za private propery na the right to privacy, the tax payers have all the rights to know the public as well as the private conduct of such entity maana nikodi zao!. Kwa vile Chadema kinaendeshwa kwa ruzuku, hiyo ruzuku ni fedha yako, fedha yangu na fedha yetu as public, hivyo we have all the rights, kujua kila kitu kuhusu Chadema na kutoa maoni yoyote kuhusu Chadema, na ndio maana hesabu za Chadema, zinakaguliwa na CAG.
Hoja za Bandiko hili
Japo Chadema wenyewe hawajikubali na kuukubali ukweli kuwa Chadema hapa kilipofika kama chama kikuu cha upinzani kiko stagnant na graph yake imeanza kushuka kwa kasi ambapo viongozi na wanachama wake wanaojitambua, they are doing the right thing, wengine wanasubiri tuu Bunge livunjwe nao waamue, hivyo wana Chadema kindakindaki wenye misimamo thabiti, walioamua kuifia Chadema, itawabidi wajitambue "Kama Chadema Sasa Wanajitambua, na Wanajua Wanataka Nini, Watamchagua Mwambe, Lakini Kwa Vile Siku Zote Chadema Huwa Hawajitambui, Sijui Sasa Kama Wanajitambua, Hebu na Tusubiri Tuone!".
Hitimisho
Kwanini Mwambe na Sio Mbowe?.
Nanalizia kwa kusisitiza, Mhe. Mbowe hana tatizo lolote bali amefikia point of his optimum, mwisho wa uwezo wake, he can not do anything more than what he can or what he did due to over staying na kuwa over saturated to the point of saturated solution that can take no more that it can, ila pia naelewa mapenzi ya Watanzania kwa viongozi wao, hata Nyerere asingengatuka mwenyewe ile 1985 hakuna mtu angethubutu kumwambia mzee pumzika, hivyo inawezekana wana Chadema bado wana mapenzi makubwa sana na Mhe. Mbowe, kwenye mustakabali wa uhai, survival na sustainability ya chama, wasiangalie mapenzi, waangalie uwezo, ability na capabilities.
Politics is science, inafuata principles of political science, Mbowe alipokea Chadema kikiwa ni chama cha kiharakati, alipaswa aki transform kugeuka chama tawala in waiting. Serikali Kivuli ni government in waiting, ilipaswa kila Waziri akifanya jambo fulani, waziri kivuli ana counters kwa kueleza how wrong the government is wangekuwa Chadema wangefanya nini tofauti but serikali kivuli ya Chadema utaisikia tuu Bungeni but its like it doesn't exist nje ya Bunge.
Namfahamu vizuri Mwambe, huyu sio mwanaharakati ni strategist, baada ya Chadema kumpoteza Prof. Kitila Mkumbo, na ZZK, kiukweli kabisa Chadema is totally empty in terms of strategists, hivyo Mwambe ata i transform Chadema kutoka chama cha kiharakati kukigeuza chama tawala in waiting. Japo umaarufu wa Chadema ni ule uanaharakati wake, chama cha kiharakati kazi yake ni harakati tuu, hakiwezi kwenda Ikulu unless na sisi tufanyie majaribio ikulu yetu!.
You can just imagine kama Chadema hii tunayoiona sasa ndio ingepewa nchi ile 2015, hali ingekuwaje?!, si ingekuwa disastrous, thanks God angalizo hili, limesaidia
Wanabodi, Preamble: Chadema ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa...
www.jamiiforums.com
Namalizia Kwa Lile Lile Swali la Msingi, Kama Chadema Sasa Wanajitambua, na Wanajua Wanataka Nini, Watamchagua Mwambe, Lakini Kwa Vile Siku Zote Chadema Huwa Hawajitambui!...Then Watamchagua Tena Mhe. Mbowe. Swali Jee Chadema Sasa Wanajitambua na Kujua Wanataka Nini?Au Bado Hawajimbui?,
Tusubiri Tuone!.
Nawatakia Wana Chadema, Uchaguzi Mwema wa Kuchagua Ama Kuendelea Kuishi Ama Kifo!.
Ndugu Paskali,
Baada ya kusoma bandiko lako hili, ndio umedhihirisha zaidi tuhuma dhidi yako kwamba kuna kitu unatafuta kutoka utawala wa awamu ya tano. niseme ukweli tu kwamba bandiko lako HALINA VIWANGO.
Aina ya hoja uliyojenga, kuwaambia CHADEMA wamchague fulani na fulani wamuache, ni hoja ya hatari ambayo inatakiwa mtu akanyage kwa tahadhari kubwa. kwa kawaida watu waungwana huwa hawatoi kabisa ushauri wa aina hiyo. hata kama wanataka kusema mchagueni fulani, hawatasema hivyo moja kwa moja, bali watajenga hoja zenye nguvu na madhubuti, ili kuwashawishi wapiga kura, kwa hoja. na hata mtu anaposoma hoja kama hizo, huweza kucheka hapa na pale, lakini hasa ataheshimu mchango wako.
Sasa basi, kwa kuwa umeamua kuandika hivyo ulivyoandika, kuna njia ambazo ungeweza kutumia angalau watu wakakuelewa. unasema Mbowe amefikia kikomo katika utendaji wake. kwa hoja zipi? unasema chama kinakufa, je ni kweli kinakufa au ni mazingira ya kisiasa ya sasa hivi yalivyo?
Ukiangalia kihistoria, CCM na serikali yake huwa wana-target chama kikuu cha upinzani. Ilikuwa hivyo kwa NCCR, ambayo baada ya Lyatonga Mrema kujiunga nacho, kiliibuka kuwa chama kikubwa sana cha upinzani, na kutoa wabunge machachari, kama akina Masumbuko Lamwai. NCCR ilipigwa vita hadi ikawa dhaifu kama ilivyo leo. ikaibuka CUF. Hii nayo ilitamba bara na visiwani, hapo zaidi visiwani. nayo ikawa targeted. utasikia oohh, chama cha waislamu, nk. hatimaye kwa kumtumia Lipumba, CUF imeondoka rasmi katika orodha ya vyama vikuu vya upinzani, na bila shaka uchaguzi wa 2020 utahitimisha rasmi safari yao. ikaja CHADEMA. kule mwanzo serikali za CCM wala hazikuwa na shida na CHADEMA, ambao kwa mwaka 1995 na 2000 hawakusimamisha mgombea wa urais, bali walikuwa wanaunga mkono wagombea wa NCCR. CHADEMA walianza kusimamisha wagombea urais mwaka 2005 kwa kumsimamisha Mbowe mwenyewe. ilikuwa hapo CHADEMA ndiyo ikaanza kupaa. kila uchaguzi CHADEMA kimejiongozea idadi ya wabunge, madiwani nk. na hatimaye kuibuka kuwa chama kikuu cha upinzani. hapo ndipo serikali ya CCM imei-target CHADEMA. sasa hivi kelele zote zinaelelekezwa CHADEMA.
Mara kadhaa viongozi mbalimbali wametangaza kifo cha CHADEMA. walikuwepo akina Steven Wasira, na hatimaye Rais Magufuli mwenyewe ambaye aliahidi kuua vyama vyote vya upinzani kufikia 2020. Na katika wote hao, Magufuli ametumia mamlaka yake kwa kiasi kikubwa ili kuvikandamiza vyama vya upinzani. Kwa hiyo kwa kuweza kuhakikisha CHADEMA iko hai na inaweza kufanya chaguzi zake, na hata akina Cecil Mwambe wakagombea katika mazingira kama haya, ni jambo kubwa.
Unasema unamfahamu Mwambe. unamfahamu vipi? yaani tukuamini tu wewe kwamba madhali unamfahamu kwamba ni strategist mzuri, basi? kafanya nini mpaka hivi sasa? Mbowe tunamfahamu, mazuri yake na madhaifu yake. Mwambe je? Ulitakiwa uorodheshe yapi kayafanya, ili kuwashawishi wajumbe wa CHADEMA.
Hivyo kwa kutamka tu ulivyotamka, hujajitendea haki wewe mwenyewe kama mwanahabari mkongwe.
Lakini kuna hili la UANAHARAKATI. Hizi ni Propaganda za CCM. wanachora ramani chama cha siasa kinatakiwa kiwe vipi. Ebo! Hivi kwanza CCM ni chama cha siasa? kilishakufa siku nyingi mbona? ni kikundi tu fulani kinachotumia dola kutawala. hata wanaCCM wenyewe washajichokea. na ndio maana CCM inaweza kuendesha vioja kama huo unaoitwa uchaguzi wa serikali za mitaa. Na mwenyekiti wao anajipongeza kabisa akiwaambia HONGERENI KWA USHINDI!!!
Chama cha upinzani kinatakiwa kupambana muda wote. lakini tukumbuke pia kwamba nguvu za vyama vya upinzani zinatokana na utayari wa watanzania kuvitetea vyama hivi na kuvilinda. wakiwaachia viongozi tu siyo haki. CHADEMA hawana dola ya kuegemea, kama wanavyofanya CCM. wao wana support ya wananchi tu basi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.