Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

:Nikuulize swali,hivi hitler angekuwa bado yupo hai ungemuombea azidi kuishi mkuu?

Hii dunia sio rahisi kama unavyoifikiria!

Ni hivi... Ukishindwa, you lose everything, including yale mema na mazuri ambayo dunia ingejivunia. Mshindi ndiye anayetoa definition ya utu na thamani ya utu wako kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.

Hitler angeshinda vile vita, hakika mambo yote ya ovyo tuliyosomeshwa na kuaminishwa juu yake yasingekuwepo, kwa sababu dunia ingelishwa kile ambacho kingemweka Hitler kwenye nuru njema!
 
Ni wapi malaika mtoa roho anaitwa Israel katika Biblia Mayala? Maana hilo neno ni la chuki na propaganda za watu wenye chuki na Israel mbona mi hukuona we mtu smart unaingiaje kwenye mtego wa chuki hivyo?

 
Hata kwenye hii sintofahamu iliyojitokeza, manabii wa majanga, hawakosekani, baada ya kumshuhudia live ikulu, sura zao zimewashuka.
P
Pascal hii Nchi ina watu wa ajabu sana Kaka yangu. Mpaka Zitto Kabwe alikuwa kwenye mkumbo huo. Baada ya kupata za chini chini kuwa Mh. Anapiga mzigo kama kawaida akajifanya kanukuliwa vibaya. Ni hatari sana kuwa na watu wanaojidai kuusaka uongozi wenye akili kama Zitto. Ukweli nimefurahi sana kumuona Mkuu live. Ningekuwa mnywapombe ningekesha. Mungu ampe maisha marefu.
 
Mkuu Nyangomboli , watu wanaomuombea mema Rais Magufuli ni wengi kuliko wanaomuombea mabaya, sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, Mungu atamlinda na kumpa maisha marefu, ila na yeye kama ana yake ya kustahili adhabu ya karma, muda wake ukifika karma itakula tuu kichwa, dawa ya kuepuka adhabu ya karma ni kutenda mema.
P
 
Ni wapi malaika mtoa roho anaitwa Israel katika Biblia Mayala? Maana hilo neno ni la chuki na propaganda za watu wenye chuki na Israel mbona mi hukuona we mtu smart unaingiaje kwenye mtego wa chuki hivyo?
Mkuu Chizi Maarifa, jee unayajua majina ya malaika wangapi waliotajwa kwenye bible na unazijua kazi zao?.
P
 
Wengi ndugu yangu. Akina mikael,gabriel n.k ntajie wewe israel ulimsoma kitabu gani katika biblia kuwa ndiye mtoa roho ili nami nafsi yangu ielimike...maana yawezekana nikawa maamuma katika hilo.

Mkuu Chizi Maarifa, jee unayajua majina ya malaika wangapi waliotajwa kwenye bible na unazijua kazi zao?.
P
 
Wengi ndugu yangu. Akina mikael,gabriel n.k ntajie wewe israel ulimsoma kitabu gani katika biblia kuwa ndiye mtoa roho ili nami nafsi yangu ielimike...maana yawezekana nikawa maamuma katika hilo.
Kwenye Bible, wametajwa kwa majina, malaika wanne tuu, Luciferi, Mikaeli, Gabriel na Rafael, jee kwa vile Bible imewataja hao wanne, ndio inamaanisha malaika wa Mungu wako wanne tuu?.
P
 
Nani alikudanganya kifo kina umri?
 
Je kwa kuwa hawajatajwa wengine inamaanisha tunaweza watunga wengine? Maana kama neno malaika limetoka kwenye Biblia na ukasema wametajwa wanne. Nawe ukazungumzia biblia na characters wanaohusika na biblia.huyo israel mtoa roho umemtoa kwenye kitabu gani kinachohusiana na biblia.

Katika ukristo kuna malaika wengi. Nikutajie some names.
1. Gabriel
2. Rafael
3.abaddon
4. Ariel
5. Daniel
6. Azazel
7. Barachiel
8. Camael
9. Cassiel
Na wengine zaidi. Malaika hao wapo kwa mujibu wa Dini kuu tatu.
1. Kikristo
2. Kiyahudi
3. Kiislamu

Kwa upande wa Mashariki ya kati. Katika Ukristo hakuna malaika Israel/azrael. Huyo ni malaika kwa upande wa waislamu ambao nao wana dini yao na Mungu wao. So unapozungumzia uislamu ni sawa wana malaika wa kifo kwa jina la azrael. Kwa wakristo hayupo.

Kwenye Bible, wametajwa kwa majina, malaika wanne tuu, Luciferi, Mikaeli, Gabriel na Rafael, jee kwa vile Bible imewataja hao wanne, ndio inamaanisha malaika wa Mungu wako wanne tuu?.
P
 
Mkuu THE SEAL, Hiyo wish inakuingiza kwenye kundi la prophets of the doom.
P
 
Hiyo wish inakuingiza kwenye kundi la prophets of the doom.
P
So you are oky with what this dictator is doing to our country that has known peace and such things since the time we got uhuru till 2015 when this hitlers brother took power?????? if you put me in the category of prophets of doom so be it, if you were azorys brother, tundu lissu cousin, ben saanane uncle, on and on, i doubt if you could call me a prophet of doom, but i respect your opinion, noting very well that OPINIONS are not TRUTHS,
 
Mkuu sikuionaga hii thread miaka yote!

Ulilenga kuhimiza upendo na kutendeana mema wakati huo ukijenga hoja fikirishi pia, saazingine wewe binafsi bila kujua.

Ulisema kuwa mtu atakufa siku ile ile, saa ileile, sekunde ile ile na aina ya kifo kilekile alichopangiwa na Mwenyezi Mungu.

Maelezo hayo tu ndiyo mimi nimeona ni kama maelezo tata!

Hivi kwa mfano, vifo vya kutisha vinavyosababishwa na binadamu wengine, kama vile kuuawa kikatili kunakotokana na uonevu au ujambazi, utasema aina hii ya vifo ni mapenzi ya Mungu na kwamba mtu yule kaandikiwa na Mungu afe kifo cha aina hiyo?

Iweje sasa wasababishaji waonekane kuishika masharubu serikali, pia iwe ni dhambi ya mauti katika amri za Mungu mwenyewe?

Embu jaribu kuliweka hili vizuri, ili twende pamoja mkuu.
 
Tumia ulimi wako vizuri. Unapomuombea Dua mbaya binadam mwenzio, kama si sitahiki kwake basi ujue Muumba wetu anaigeuza inakuja kwako mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mr.Mak , Naunga mkono hoja na hili nimelisema humu.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…