Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

Bebe uliyomba duhu Pasiko hemu fikiliaga shi abana bang'wa Lissu bena buchungu kiasi ki? Halafu unke ung'wa Ben Saanane alibalombela ki abatale ba si ise? Pyee abo nabataja lazima balilombela ache ug'winikile kaya.
 
Pascal kuna vitu vingine vinahitaji tu tafakuri ya kina.. Ni kweli kabisa corona ni janga na si jambo jema kuomba iingie nchini.. Lakini kwa hali tuliyonayo kuna tatizo kubwa mahali na wananchi wana fukuto vifuani mwao
Maombi haya ya kutaka corona ije ni namna ya kutoa ujumbe fulani kwenye jamii

Jr[emoji769]
 
Mkuu Mshana Jr , wewe ni miongoni mwa ma GT wetu humu katika mambo ya zile powers from within, pia unaijua nguvu ya kauli, ikitokea aliyeomba Corona ije na ikatokea kauli yake ikawa na nguvu kweli, na mjibu maombi akamjibu, ombi likatekelezwa Corona ikatua nchini Tanzania, jee itawashambulia wale wabaya wake tuu au hadi yeye, chama chake na familia yake?.
P
 
Mkuu Rutashubanyuma , huu pia ni unabii wa majanga, ni ramli chonganishi kutuchonganisha na Mungu.
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba! - JamiiForums

Ugonjwa wa Corona ni ugonjwa wa shetani na unaenezwa kishetani, Tanzania ni taifa la Mungu, sio kama Italy, hivyo Mungu ametukinga na ushetani wa Corona. Tuacheni kutishana, wananchi tuchape kazi.
P
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji40]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Zitto, hawa merchants of death ni sawa na hawa prophets of the doom nilio wazungumza humu?. Kama unasema wanashitakika, hivyo jee umewashitaki?, ili likitokea la kutokea, tumjue wa kulia nae kuhusu mtu wetu!.
P
 
Mungu siyo Pascal Mayalla useme atakuwa mnafiki.Naamini Pilato wa Chato atakufa kwa Corona, mark my words!
Duh...!. Mkuu Behaviourist,
Kumuombea mtu yoyote kifo chochote ni sawa na kumtabiria kifo, hivyo wewe ni nabii wa majanga!!, ila kwa vile Corona ni shetani, kumuombea mtu yoyote apate Corona ni ushetani!. Tuweni na utu wa kuliombea taifa hili janga la Corona lipitilizie mbali, tuwe binadamu jameni tusiwe mashetani!.

Wewe Mkuu Behaviourist , mbona umeyatamka maneno haya "Naamini Pilato wa Chato atakufa kwa Corona, mark my words" kwa uhakika sana as if wewe ndio Luciferi mwenyewe?. Siku likitokea la kutokea, wengine wetu tutamjua mtu wa kulia nae!
P
 
Naomba Mungu watu washuhudie wewe Mayalla P, ukifa ili waseme uongokuhusu kifo chako.Usipate nafasi ya kushuhudia ila watu wakushuhudie wewe
Duh...!, Mkuu Tsitingile, yamekuwa hayo!.
Kumuombea mtu yoyote kifo ni chochote ni sawa na kumtabiria kifo, hivyo wewe ni nabii wa majanga!!,
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba! - JamiiForums

ila kwa vile Corona ni shetani, kumuombea mtu yoyote apate Corona ni ushetani!. Tuweni na utu wa kuliombea taifa hili janga la Corona lipitilizie mbali, tuwe binadamu jameni tusiwe mashetani!.
Japo wewe ni binadamu, ila unaweza kujikuta umegeuka shetani bila wewe kujijua!.
Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums

P
 
Prophets of doom wa ajabu kabisa kweli wapo sana!.
Nkurunziza aligomea kupima COVID-19 Burundi na kudai hadharani kuwa Burundi hakuna Corona!.

1. Kwa kuanzia Corona ikabisha hodi nyumbani kwa rais Nkurunziza kwa kumpata mkewe, ndege ya rais ikatumika kumkimbiza Nairobi Hospital.

2. Wakati Wife akitibiwa huko Nairobi, Corona ikamrudia, akajaribu kukomaa nayo, lakini wapi, Corona ikala kichwa!.

3. Kitu cha ajabu kabisa, baada ya kifo cha rais Nkurunziza kuna watu, Watanzania wenzetu ni watu wa ajabu kweli kweli, eti wanamshangaa Mungu kwa kumuuliza kwanini Nkurunziza tuu, na kumuomba Mungu amalizie kazi eti kwa kuombea ampende zaidi.... nanii!. Hawa ni binadamu wenzetu kweli au ni mashetani?!. Badala ya kusikitikia kifo cha Nkurunziza, wao ndio kwanza wanaombea....

Huu sio utu!.
P
 
Wewe ni Bank?
 
Kwa hali ilivyo hata ukiwakuta waasi wa Msumbiji wanamshambulia mwa chama wa CCM unawapa baraka zote.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…