Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Wataliano waliweka rehani afya za raia wao kwa kutanguliza uchumi badala ya afya sasa wanavuna walichopanda ni kuzikana tu hata Waziri Mkuu wao kabwaga manyanga...Kiburi cha mtaliano kimehamia hapa na sisi ndani ya wiki nne tutaufyata na kunyenyekea tu hakuna jinsi..
Sisi tunafuata nyayo za kiburi na dharau za mtaliano lakini tunamwomba Mwenyezi Mungu atufumbie macho tusiwe kama Wataliano yaani Mungu yupi huyo mwenye ubaguzi?
Kila mtu atavuna alichopanda: Tumethamini uchumi na kudharau afya zetu sasa tutegemee kupoteza uchumi na afya kwa mkupuo mmoja
Mwenyezi Mungu aliuliza maswali mawili muhimu sana:-
1) Hivi uhai wako siyo muhimu kweli zaidi ya mkate?
2) Hivi mwili wako siyo muhimu kweli zaidi ya mavazi?
Ndani ya wiki nne kuanzia leo tutapata majibu ya uhakika kama sala zetu za kubaguliwa zimejibiwa... Mwenyezi Mungu alituagiza magonjwa ya mlipuko na ya kuambukiza tunapaswa kujitenga kwa quarantine sisi tunasema business as usual... Sasa tunamkaidi khalafu tunategemea matokeo tofauti... Four weeks tutajua nini maana ya unyenyekevu
Sent using Jamii Forums mobile app