Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Nitoe tu ombi kwa kamati ya kudhibiti corona iliyo chini ya ofisi ya waziri mkuu kwamba ikiwapendeza wavifungie vilabu vya pombe za kienyeji.

Kwa mfano kwenye vilabu vya mbege, komoni au Ulanzi walevi hunywa kwa kuchangia bilauri ya kunywea na hivyo kupokezana mara kwa mara kwa kutumia mikono.

Nadhani DC Kasesela na Ole Sabaya mkifanya utafiti mdogo katika wilaya zenu mtakubaliana na mimi na hivyo kwa pamoja tuishauri kamati.

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka!
 
Hatimaye amekuwa serious... Alikwenda Lugalo akatoa jokes. Sasa mambo yaneenza kuwa moto naona mtu anakuwa mpole.Cheza na Corona wewe....!!
 
Hata kuisoma tu hotuba iliyoandikwa kwa mashine kwa "font size 24" Mzee Magufuli anashindwa kusoma kwa ufasaha!!

Tatizo ni nini??

Pamoja na kukosa "fluency", nimefurahishwa na jambo moja, kukwoti mstari wa Neno la Mungu kutoka Biblia Takatifu....

Hata hivyo naomba kumshauri ndg Magufuli kuwa, aanze yeye na Makonda wake " kuacha njia mbaya (maovu) yao" ili tunapomwomba Mungu kuponya nchi yetu, aone ukweli huo toka ndani ya moyo was kiongozi mkuu wa nchi.....

Na hii ikiwa ni pamoja na kukifuta mara moja kikosi kazi chao cha kuteka, kuumiza na kuua watu wanaowadhania kuwa wanatishia maslahi yao ya kisiasa....

Kusema tu kwa mdomo huku matendo yao yakisema kitu tofauti, ni unafiki na haina maana yoyote zaidi tu kwamba tunazidi kumdhihaki Mungu muumba wetu...!!
 
IMG_4719.JPG


KWA KWELI TANZANIA TUNA RAISI MUHIMU SANA ALIYE NA HOFU YA MUNGU

Haya yote yatapita, Tanzania itakuwa Bora zaidi na Mungu azidi kukubariki Mh Rais na Tanzania


Sent from Gnet Phone using JamiiForums
 
Kenya wamepata cases nane leo na katika hizo wageni nao ni wachache zaidi ya wenyeji. Wale tunaosema huu ugonjwa ni wa wageni tuendelee kupaza sauti.

Ila wenzetu wapo serious wanasema ole mtu akutwe sijui kanisani au wapi kwaajili tu ya kutafuta sadaka za waumini!
 
Ni swali fupi tu;

Je kamati ya kudhibiti virusi vya Corona iliyo chini ya Waziri Mkuu inahusisha pia wajumbe kutoka Zanzibar?

Maendeleo hayana vyama!
 
....Wasafiri wote wanaoingia nchini, Watalazimika kuwekwa Sehemu ya kujitenga [Karantini] kwa gharama zao wenyewe kwa siku 14 hata kama ni mwenyeji.

Mwenye taarifa zaidi atusaidie hapa maana mzee baba hajawa clear sana

Amesema hivi "wasafiri wote watakaoingia Nchini kutoka kwenye Mataifa YALIYOATHIRIKA ZAIDI na ugonjwa huu watalazimika kufikia kwenye sehemu ya kujitenga kwa 14 days kwa gharama zao".

Maswali kadhaa hapa

1) Does this mean wale wanaoingia kutoka kwenye Nchi zilizoreport wagonjwa wachache (less than 10, less than 30? less than 100? etc) hawatawekwa kwenye mandatory quarantine??

2) Utaratibu upoje? wameshaidentify hizo sehemu maalumu/hotels ambapo wasafiri watawekwa?

3) Does this apply to Zanzibar as well? maana inasemekana Zanzibar wanafanya mambo kivyao as far as the war against COVID-19 is concerned

Hili ni muhimu kuliweka sawa ili watu wajipange sawasawa.
 
Zanzibar wana kamati yao I guess. Walishapiga stop mdege kuleta watalii na kwa yule "mtalii" atakayekaidi na kuingia Zenji, atawekwa kwenye mandatory quarantine for 14 days kwa mfuko wake. Yaani unaweza kukuta wakapelekwa hotel za bei mbaya sana
 
Back
Top Bottom