Wakuuu Leo rais amehutubia, taifa ambapo ameeleza mipango ya serikali katika kupambana na corona, na changamoto zinazoikumba nchi katika kipindi kigumu hiki na ametoa maelekezo kadhaa, kiujumla mheshimiwa rais ameeleza vizuri Sana na Mimi nimemuuunga mkono kwa hotuba yake Nzuri Sana
Ila Nimeshangaa watu wanamponda na kumshambulia na kukosoa hotuba yake wengi wakisema afunge mipaka na wengi wanapinga kauli yake kuwa watu wachape kazi, wakuuu Mimi nampingaga Rais kwa mambo mengi Lakini Kwa hotuba yake ya Leo nampongeza na kumuunga mkono kwa asilimia Mia.
Nawashauli wakuuu kuwa tusisite kumkosoa rais katika mambo ambayo hayaendi sawa pasipo kuogopa mtu yoyote tupase Sauti, Lakini tusipinge hata yaliyomazuri anayofanya rais tumuunge mkono kwa mazuri na tujizuie kumkosoa kwa kila japo
Wakuuu ujue heli nusu Shari kuliko Shari kamili, heli tupate tatizo moja tutapambana nalo kuliko kupambana na matatizo mawili kwa Wakati mmoja, hatuwezi kupoteza watu Kwa ugonjwa na tukapoteze wengne kwa njaaa, jamani hivi tukifunga mipaka watanzania wanategemea Kutoka ndio wale weng hupata vitu toka nchi za jirani kila Siku ndio wale, je wewe hao watu utaweza kuwalisha? Hivi watu wasiende kazini kuchapa Kazi utaweza kuwalisha? Dar watu wengi zaid ya nusu ni vibarua wanaotegemea kutoka wakafanye Kazi ili walipwe kwa Siku warudi nyumbani watoto wale, mama ntilie hivyo hivyo, wakuuu acha Kabisa kuhangaika ili watu wasiende kazini, mipanga ifungwe watu watakufa na njaaa kwa wingi kuliko kufa na corona tumuuunge Mkono rais tuache hao wanao pinga kila kitu na kulazimisha eti mipaka ifungwe hao hawajui Tanzania ilivyo
Rais katoa hotuba Nzuri Sana tumuunge mkono
Sent using
Jamii Forums mobile app