Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Hakuna mahali nimelinganisha kati ya yeye na mimi, nilichozungumza ni ile hali ya ninyi kumwona kama yeye ni authority.

Kwamba anachokisema mnaona kama hakitakiwi kukosewa.

Sijawahi kumpenda wala kumchukia, namchukulia kama member wengine tu humu, na ninachokisoma kwake lazima nikithibitishe mahali kama inawezekana.
learn to appreciate someone IQ and talent, thats all
 
Ataongea yale aliyoyasema kanisani kuwa Corona ni nyepesi kuliko ajali
Kwa ufupi huyu mtu ni janga la Taifa
He is not serious
Anadiriki kusema hajafa mtu bado mpaka afe mtu ndio atachukua precautions
Nchi ziko kwenye lockdown uchumi umeyumba big time yeye anazungumza matani

Tanzania Tufanye yafuatayo:
Funga mipaka
Wachina au Wageni wote wawekwe kwa quarantine ( muda wa kutambua pia uhalali wa kuwepo nchini)
Office na biashara zifungwe (restraunts mama ntilie masoko)
Watu wasisafiri ovyo
Watu wakae majumbani (14days)
Daladala zipunguze abiria
Jeshi la wananchi sio polisi lisimamie zoezi
 
Igweeeee wandugu.Leo katika jamhuri ya hapa kisiwa cha Sumatra Indonesia,marais wawili wamehutubia taifa pendwa,mmoja kaongelea ugonjwa tishio duniani Corona akiwa kanisani na kuwataka wananchi wa hapa Sumatra waache kuogopa na wasitishwe kabisa na Corona.

Baadaye rais mwingine wa hapa hapa kisiwani akalihutubia taifa kwa vyombo vya habari,cha ajabu rais huyu ameongea vizuri kuhusu ugonjwa wa Corona na hatua zilizochukuliwa na serikali kuukabili ugonjwa na akaeeleza mikakati mipya ikiwemo kila mgeni anayeingia nchini atawekwa karantini kwa siku 14 kwa gharama zake.Huyu rais japo amechelewa kuchukua hatua lakini wananchi wamefurahishwa na hotuba yake kiasi tofauti na rais aliyeongea akiwa kanisani.

Wananchi wa hapa kisiwani wanashangaa utafauti mkubwa wa hizi hotuba za marais,sasa wamenituma niwaulize wasomi wa hapa jukwaani maoni yao na mustakbali wa kisiwa chetu.Karibuni wadau watu makini wa hapa jamii forum.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JipuKubwa, Kiongozi mbona tahadhari inatolewa kwa vitu minor cases

Je, unapovua viatu ambayo umevivaa na kupita maeneo mbalimbali hamuongelei?

Je, mavazi tunayovaa tunapulizia dawa za kuua vijidudu vya corona

Kumbuka hivi virusi vina uwezo kuishi kwa masaa zaidi ya kumi mpaka siku tatu

Tumekomaa na kuosha mikono tu na kusahau yatupasa kupuliza madawa majumbani na maofisini

Kikubwa Jaribu kuwa na akiba ya maneno, Pale ni kanisani anaongea na watu wake, Huku mtaani corona haina kanisa
 
Wa kanisani tumeambiwa kiboko ya huu ugonjwa ni maombi, maana ugonjwa huu tumeambiwa umeletwa na shetani
 
Kwa ufupi huyu mtu ni janga la Taifa
He is not serious
Anadiriki kusema hajafa mtu bado mpaka afe mtu ndio atachukua precautions
Nchi ziko kwenye lockdown uchumi umeyumba big time yeye anazungumza matani

Tanzania Tufanye yafuatayo:
Funga mipaka
Wachina au Wageni wote wawekwe kwa quarantine ( muda wa kutambua pia uhalali wa kuwepo nchini)
Office na biashara zifungwe (restraunts mama ntilie masoko)
Watu wasisafiri ovyo
Watu wakae majumbani (14days)
Daladala zipunguze abiria
Jeshi la wananchi sio polisi lisimamie zoezi
Hizo precautions alizosema hujazisikia?
 
Rais wa kanisani alijawa na Roho Mtakatifu wakati Rais wa Ikulu aliandikiwa hotuba lakini hata hivyo alishindwa kuisoma kiufasaha.
 
Back
Top Bottom