Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Yaani nilijua leo kutakua na strong statements lakini ndio kwanza mambo ni meusi tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wewe jilinde kama wewe na familia ukitegemea Magu umechemsha yeye siku zote iko 'offside' with the outside world yani kituko cha dunia.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeshauri vizuri, lakini tambua hili si jambo la kifamilia. Kumbuka hata WHO wametangaza ni "World Pandemic". Jambo la namna hii huwezi chukua hatua ya kifamilia ukawa "safe". Huko ni kujidanganya sana. Kama jamii inayokuzunguka inaishi maisha yasiyo "safe" wewe wawezaje kuchukua hatua ya kifamilia. Na tambua huwezi ifanya jamii ichuke tahadhari kwa kujidai unatoa tu elimu.

Binadamu hayuko hivyo. Wako ambao hata uwape elimu ya namna gani bado wataenenda sivyo. Ndiyo maana hakuna nchi duniani inayotoa elimu tu pasipo kuwa na sheria za kuongoza watu. Mambo ya namna hii ndiyo hufanya Serikali iwepo...Nirudie kusema "huwezi jilinda wewe na familia yako kama ulivyosema" kwenye hili bila kuwa na "strictly government intervention(s)"
 
Unatetea ujinga... Italy alichukua hatua gani baada ya Korona kuingia?
Sema unayojua usaidie watu kujua zaidi usikimbilie ujinga... navyojua pamoja na mengine Italy ni nchi yakwanza ulaya kuzuia ndege toka na kwenda china nk.
 
Unatetea ujinga... Italy alichukua hatua gani baada ya Korona kuingia?
Sema unayojua usaidie watu kujua zaidi usikimbilie ujinga... navyojua pamoja na mengine Italy ni nchi yakwanza ulaya kuzuia ndege toka na kwenda china nk.
 
Weka jambo unalolalamikia; jambo fulani alifaa atende hivi sio kutisha tisha watu.
 
Afrika kila kitu kilichelewa .
Utumwa
Ukoloni
Uhuru
Haki za Binadamu
Demokrasia
Utawala Bora.
Maendeleo

Sasa Korona imechelewa kuingia Afrika kwa nia njema kabisa na kwa msaada wa Mungu.
Yote ni ili tujifunze kwa wenzetu ili tusifanye makosa lakini tunafanya makosa Yale Yale mabaya kuliko waliotangulia.

Tumuombe Mungu atupe majawabu kwa Ugonjwa huu na pia tuchukue Tahadhari.
Mabasi yanajazana watu bila kuvaa maski watu wanapigiana Chafya na kukohoa kwenye mabasi.
Stand zinafurika watu bila kuvaa maski.

Eti watu wasivae mpaka waugue na wakivaa wazitoe kila baada ya masaa manne.
Sasa unajiuliza kama wanaona kuna sababu ya kuibadili inakuaje kwa ambaye hajavaa kabisa ?
Wanataka kumfurahisha nani?

Au ni ili watu wasihisi gharama ya maski. Kwa nini watu wasikate vipande vya mashati na khanga wakafunika midomo na pua zao ili wasipigiane Chafya?

Au hata wavae hijabu za kininja ? Lengo ni kupunguza maambukizi endapo yatakuja kwa wakati usiojulikana .

Afrika tubadilike kwa kujifunza kwa wenzetu. Kila kitu kimechelewa kwetu lakini hatujifunzi zaidi ya kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa faida ya madaraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Guus, Ni kweli hata Kondom kuna wakati serikali ilikua inatoa bure kwa baadhi ya taasisi.
Pia Chandarua serikali ilitoa kila kwa kila kaya ili kutokomeza malaria.

Serikali ilipaswa mpaka sasa ihamasishe watu wote wavae maski kabla ya ugonjwa kuingia .
Na pi namna rahisi ya kutumia maski za vitambaa kwa kufunika pua na mdomo bila kuasahau suala la usafi na kuzifua Mara kwa Mara kwa sabauni na maji ya moto na chumvi.

Kufunga mipaka yote ya nchi lilikua ni jambo la lazima na muhimu.
Uzuri Tanzania tuna chakula cha kutosha mana 80% ni wakulima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unatudanganya ili iweje? hadi sasa mi nawajua rafiki zangu watatu tayar wameshakufa huko Italy, ni waafrika kuna pia rafiki yangu mmoja mkenya hatujajua hatima yake, yupo mahtuti hatuna mawasiliano naye, mke wake anadai aliambiwa asipige simu maake ni kama kuwapotezea muda, wagonjwa ni eengi wa kuhudumia na wote wanahudumiwa sawa sawa.

kama kutajir na mauti watamwambia, na huyo mwanamke wao pis wapo quarantine na watoto, hawaruhusiwi kutoka wala kufanya chchte, wanaletewa chakula na mtu anakiweka nje akitoka wanakuja kukichukua kwa sababu walikuwa na mgonjwa hivyo wametengwa, ingawa anadai wako salama hadi sasa..hivyo tusiweke mzaha kws mambo kama hays, tuchukue tahadhari za ukweli tusidanganyane!
Corona haiui mtu mweusi, ya Italy hayatakaa yatokee bongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mikusanyiko anayohimiza Mkuu wa nchi iendelee bila wawiwasi misikitini na makanisani ina immunity na corona nchini kwetu? Hiyo si ndiyo iliyochangia kasi ya maambukizi Italy?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mkulu kaongea akiwa ikulu Dodoma na kasema haondoki tena hadi mwisho wa maisha yake. Sasa sijui ana maana atafia ikulu au!!!
 
Kila akiwaza madai ya tume huru anachanganyikiwa, maana hana uhakika atapata ushindi kiasi gani, kwani hajawahi kushindana zaidi ya kubebwa na hii Tume isiyo huru ya uchaguzi. Hivyo inabidi asake kura za waumini kwa kujifanya mnyenyekevu na mcha Mungu.
Tume huru kwake inamtisha kama korona
 
Hapa kiukweli nimeshindwa kuelewa sababu za kufunga Shule na Vyuo, Tanzania kuna dini kubwa mbili Waislamu na Wakristo, Waliofunga Shule na Vyuo wanaenda Miskitini na Makanisani, mi nafkiri Luna haja ya kutafakari zaidi, hatujafanya kitu hapo, Lakini naamini Watz Wa naona yanayotokea duniani,maamuzi ni yao, stay at home please

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom