Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

KENZY,
Yeye ameona kulima kwa jembe la mkono na ma? Kwanza korosho hajawalipa....je pesa za kununua mazao anazo au anaendelea kutudanganya tu? Ningemuona amefanya vizuri kama amesema tufanye vizuri kwenye kazi za technology ili wataalamu wetu wapate mahali pa kupeleka kazi zao au angesema wajitahidi kutengeneza vifaa ambavyo havipo kama masks, sanitizer, gowns nk ili tukabiliane na upungufu uliokumba duniani na tutengeneza profit lakini anawaambia watu wakalime?

Je kuna mpango gani wa wataalamu wetu kujaribu kufanya utafiti wa kutengeneza dawa za kutibu au kinga? Si tunavyo vyuo vya madaktari hapa nchini? Hadi tuwategemee hao wa huko magharibi anaowasema vibaya kila siku? Je dawa na kinga zisipofika mapema au zikiwa ghali, nchi yetu maskini itafanya nini?
 
Ahsante Mhe Rais JPM!! Mungu akulinde na magonjwa , hasa Corona!! [emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazazi wako na ndugu zako umewaombea? RAIS anayejali uchumi wa wachache kuliko afya ukimuombea roho haikusuti? WAzungu na ubeberu wao na kupenda chumi lakini wamefunga kila kitu na leo wanaFUNGA NDEGE ZOTE ZA EMIRATES,

WAMAREKANI WOTE DUNIANI WAMEAMRIWA KURUDI KWAO ila JIWE aliyekimbilia dodoma akiwatumia wahujumu maisha ya watu kama ISABELA NA MWANA FATUMA [FA] kuhadaa kuwa huu ugonjwa ni mafua ya kutibu na panadol
 
Kwa hili watanzania tuepuke misongamano sio tu kanisani na masjid.kwa jinsi tunavyokaribuana kwenye hayo majengo ya ibada hatari.viongozi wa dini ni wajibu wenu kuwalinda waumini wetu na ninyi wenyewe sijui ni kwanini viongozi wetu wanaamini kupitia mikono ndio kisambazaji kikuu na sio njia ya hewa.mapadre 29 wamekufa italia.
KUMBUKA DUNIA MZIMA MASK NA KUNAWA MIKONO Vinaenda pamoja.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar wana kamati yao I guess. Walishapiga stop mdege kuleta watalii na kwa yule "mtalii" atakayekaidi na kuingia Zenji, atawekwa kwenye mandatory quarantine for 14 days kwa mfuko wake. Yaani unaweza kukuta wakapelekwa hotel za bei mbaya sana
Tofautisha quarantine na self isolation.
 
Corona haiui mtu mweusi, ya Italy hayatakaa yatokee bongo G4rpolitics,
Wewe ndio unatudanganya, mimi ndio nakwambia corona haiui mtu mweusi. Hao rafiki zako wana maradhi yao tu mengine.
Kaulize wachina Wuhan ngozi nyeusi zilivyowaonyesha maajabu.
 
Ndani ya wiki nne kuanzia leo tutapata majibu ya uhakika kama sala zetu za kubaguliwa zimejibiwa... Mwenyezi Mungu alituagiza magonjwa ya mlipuko na ya kuambukiza tunapaswa kujitenga kwa quarantine sisi tunasema business as usual... Sasa tunamkaidi khalafu tunategemea matokeo tofauti... Four weeks tutajua nini maana ya unyenyekevu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Ruta Shuba Nyuma, huu pia ni unabii wa majanga, ni ramli chonganishi kutuchonganisha na Mungu.
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba! - JamiiForums

Ugonjwa wa Corona ni ugonjwa wa shetani na unaenezwa kishetani, Tanzania ni taifa la Mungu, sio kama Italy, hivyo Mungu ametukinga na ushetani wa Corona. Tuacheni kutishana, wananchi tuchape kazi.
P
 
Kila mtu anathawabu yake na adhabu yake, huwezi ukajua ni kwanini raia wa Italia wanakufa kama kuku,kuliko wachina ambao ndio chanzo cha korona, huwezi kujua makusudi ya Mungu kwa Italia,Mungu mwenyewe ndiye anayejua kwanini karuhusu kipigo cha namna hii kiwapate raia wa Italia, cha msingi ni kufuata masharti na kuendelea kumuomba Mungu atuepushe na baraa hili.
Mungu ndo ameruhusu haya yatokee Italia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
field marshall1,
Ile ilikua sio hotuba. Kwanza hajasema hao wagonjwa wako tanzania sehemu/mikoa gani. Pili hajasema wameambukizwa nje ya nchi au ndani ya nchi ilikujua kama tumeshaanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe na kujua ukubwa wa tatizo.

Tafiti na technolojia hajagusia kabisa. Kazungumzia mambo ya dini, shetani corona, na tuendelee na kazi. Unaweza ona kabisa mhutubiaji ana mtazamo finyu juu ya hili tatizo.
 
binafsi sijawahi kufikiri kumuombea huyu rais na sitegemei,nawakumbukaga yatima,vilema,walotingwa na mzigo wa maisha wakasahau kuomba na kumshukuru Mungu.
 
Ile ilikua sio hotuba. Kwanza hajasema hao wagonjwa wako tanzania sehemu/mikoa gani. Pili hajasema wameambukizwa nje ya nchi au ndani ya nchi ilikujua kama tumeshaanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe na kujua ukubwa wa tatizo. Tafiti na technolojia hajagusia kabisa. Kazungumzia mambo ya dini, shetani corona, na tuendelee na kazi. Unaweza ona kabisa mhutubiaji ana mtazamo finyu juu ya hili tatizo.
Ila jamaa angefaa pia kuwa mchungaji...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuwezi kujua labda wanataka ugonjwa usambae ili wapate kisingizio cha kuahirisha uchaguzi. Who knows.
 
Muhimu ni kuchukua hizi tahadhari serious binafsi nina mafua wiki sasa, koo linakauka, jana imeanza homa, kwenye kupenga mafua na kwenye kubanja damu ikatoka nimeushambulia mwili na dawa kidogo leo nina nguvu.

Na huku kijijini kwetu Corona imetapakaa awataki watu kama sisi kufika hospitali mpaka upate kikohozi kinachoweza kudumu kwa masaa matatu mfulilizo na hiyo hali iwe inajirudia thanks god mpaka sasa kifua sina.

Guys take this precaution measures serious
This is where we will fail! Hii bureaucracy ya kufanya vipimo ikiendelea, tutakuwa na low numbers in the books ila kiuhalisia watu watakuwa nao wengi zaidi. Ninakushauri ukae mbali na watu as much as possible na kila baada ya lisaa au hata nusu saa nawa mikono kwa maji na sabuni. Pole sana mkuu.

Jana nimepiga zile namba zao, zaidi ya mara tatu unawekwa waiting zaidi ya dakika tano mpaka nikakata tamaa,

Serikali ingekubali private sector na innovation hubs zichangie kwenye kukabili huu ugonjwa, hasa kwenye kutoa taarifa, kufanya vipimo hata vile vya awali, kusanitize maeneo ya uma, namna ya kupunguza mikusanyiko kwa kutoa huduma kidijitali, nk. Halafu wasisitize self isolation kwa watu.
 
Jiwe ni muoga wa uchaguzi wa vyama vingi, anataka corona ishike kasi kidogo ili apate sababu ya kuahirisha uchaguzi.
 
Jana Rais Magufuli alihutubia Taifa kuhusu hali halisi ya ugonjwa wa corona hapa Tanzania.

Katika mambo aliyosisitiza ni kutoa elimu kwa umma badala ya hofu na vitisho.


Lakini hali halisi Ikoje?

Jana ilikuwa jumapili ya kwanza baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika Tanzania.

Watu tulikusanyika kwenye makanisa yetu.

Mambo niliyogundua ambayo ni hatari kwa Taifa.

Wakristo wengi wanapuuza na hawajui madhara ya ugonjwa huu.

Pili, Hawajui kama ugonjwa ila wanajua ni mapepo au nguv za giza au kitu flani kimetoka kwa shetani.

Tatu, 90% Wanatumia sanitizer kwa wingi " japo wataalamu wengi wanasema Sanitizer inaua bacteria na sio virusi" Dawa ni kunawa maji kwa sek.40 kwa kutumia sabuni au kutumia detro ya maji ni nzuri zaidi.

Nnne. Amini Usiamini bado Wakristo wengi wanaamini Watu weusi hawapati virus hivi na wanafananisha na mafua makali.


Ushauri Kwa wenye mamlaka , Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Afya.

Fungeni mikusanyiko ya ibada makanisani na misikitini.

Nchi ya Marekani imenyoosha mikono dhidi ya ugonjwa huu kwa kuufunga kabisa jimbo la Calfonia, sio jambo dogo na ni jambo kubwa.

Napenda muwakumbushe watanzania Virusi hivi ni kama vile vya dengue, Sars, Homa ya riftvalley ambavyo vilisumbua sana Watanzania na hata tuka ogopa kula nyama, kwa hiyo virusi hivi ni hatari sana wawe na taadhali kubwa.

Pia Serikali isikae kimya. Kutoa up to date ya ugonjwa huu unawafanya wananchi kuwa na taadhari zaidi, hasa kujua sehemu gani kuna shida kubwa kama mtu amepanga kwenda asiendi na hii inasaidia sana kama serikali itakuwa imeweka ka a karantini ya mkoa gani na wilaya gani kuna shida kubwa. na watu wachukue taadhali zipi.

Msiwalaumu wananchi hata mara moja msipo wajulisha watajijulisha wenye.


CHUKUA TAADHALI CORONA NI UGONJWA HATARI SANA. NAWA MIKONO MARA KWA MARA, BAKI NYUMBANI KAMA HAKUNA ULAZIMA WA KWENDA POPOTE, TUWATUNZE WATOTO, NA WAZEE WETU WABAKI NYUMBANI WASIENDE KWENYE MIKUSANYIKO YA WATU WENGI.
 
Back
Top Bottom