Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nao ni mtazamo wako.Hapa ndio dini zinakuja kuonekana takataka.
Yaani nchi zinamiliki Biomedical labs, wanatengeneza magonjwa halafu mnakuja kumsingizia Mungu?
Nao ni mtazamo wako.
Hapa ndio dini zinakuja kuonekana takataka.
Yaani nchi zinamiliki Biomedical labs, wanatengeneza magonjwa halafu mnakuja kumsingizia Mungu?
Well said mkuu, kinacho sikitisha na kukasirisha zaidi baadhi ya maabara hizo za Biomedical zimesambaa mpaka kwenye moja wapo ya Nchi ya Afrika mashariki, some former Soviet Republics, Continental Europe and UK, Latin America.
Dunia ilazimishe Taifa husika lifungilie mbali maabara hizi hatarishi - halafu wakumbuke kwamba what goes around comes around, tinkering around with Corona gnome ndio imetufikisha hapa tulipo, ujinga jinga wa wana sayansi wa Kijeshi wenye taaluma za virusi wasipo kuwa makini na tafiti zao hatarishi Dunia itakuja kuangamia na wao hawata salimika to tell the tale the mornig after, Corona virus should serve as a wakeup call.
Nchi gani hio ya E/Africa na malengo ya wao kua na hio Lab ni nini boss?
Dini na Mungu ni vitu viwili tofauti.Mtazamo wangu kivipi wakati vitu vipo vinaonekana?
Dini zimefanya watu wengi wamekuja wajinga. Hata hawawezi kureason tena.
Mimi sijazungumza habari za Mungu.Dini na Mungu ni vitu viwili tofauti.
Kuonesha na sio KUONYESHAmkuu next time kuwa makini unapokosoa wenzako, ushamba mzigo mkuu
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kuonesha na sio KUONYESHA
Senti bai yuzingi tecno T301
Kuonesha na sio KUONYESHA
Senti bai yuzingi tecno T301
Kuonesha na sio KUONYESHA
Senti bai yuzingi tecno T301
No its too earlyToo late. Lets face the consequences
Hata zilizokuwapo imeziuwa ili tulimie meno,sijui ni faidi IPI aipatayo mwanadamu kuwalimisha meno wenzakewatu wachape kazi. hizo kazi ni zipi wakati serikali yake imefulia haina uwezo wa kuzalisha ajira?
Hii ni chumvi imeongezwa. Ile hotuba nilisikiliza yote na hakuna sehemu aliyosema haya. Hii habari ambayo ni uongo na yenye lengo ovu ilishawekwa hapa siku nyingi na tukaidharau hivyo wewe unaokoteza makombo yaliyokwisha ozaThe president of Tanzania says that "he will not shut down churches because Jesus is bigger than the coronavirus the world is facing."
According to The President of Tanzania John Magufuli, "The Church is the body of Christ, so the COVID-19 can never overpower it."
While other countries are on Lockdown and have paused all social gatherings , The President of Tanzania said his Government will not be closing down churches and mosques because the diseases are of the Devil and cannot survive while in the "Body of Christ".
![]()
This now now brings us to a number of 20 out of 17 still continuing treatment in Tanzania and 2 have healed. Tanzanian president believes that as the country they can defeat the virus by connecting themselves with God and going to churches/Mosques to pray as the Bible says "For where there is two or more gathered together in my name, There am i with them [Mathew 18:20].
![]()
Andiko lako limekaa kiroho sana, madhara yake kama hili sio pigo la Mungu ni maambukizi ya kawaida tu kama ilivyo ya mafua, basi kwa ushauri wako wengi watateketea wakiendelea kukusanyika. Ila kama ni pigo la mungu ushauri wako ni mzuriNianze kwa kusema kwamba mimi siyo mshabiki wa CCM, maana najua wazi kuwa mambo mengi yameharibiwa na CCM katika nchi yetu.
Kwa kusema hivi sina maana kwamba nachukia kila kitu kinachofanywa na serikali ya CCM. Yapo mambo mengi mazuri yanayofanywa na Rais Magufuli, ila yapo mambo mengi mabaya yaliyofanywa na yanayofanywa na serikali inayoongozwa na serikali ya CCM.
Kuhusu hili la kuwaambia watu waendelee kuchapa kazi na kuonyesha udogo wa corona kuliko Mungu tunayemwabudu. Watu wazima na wale waliopevuka kiimani wanajua wazi Corona ni pigo kutoka kwa Mungu kwa ajili ya maovu yaliyokithiri duniani, hakuna namna ya kuweza kuondoa pigo kutoka kwa Mungu kwa kujikinga tu, bali kwa kuomba toba.
Kama ushauri wa wataalamu tu ndio unaohitajika, nchi zote zilizoendelea zingekuwa zimamaliza tatizo hili mapema, kinachowasumbua ni kuwa hawajapata ufahamu wa Kiroho kwamba janga hili limetokana na kuasi Mungu, na hivyo kusababisha maafa duniani.
Njia pekee yakuondoa hili janga ni makutano ya watakatifu wanao omba toba kwa Mungu na kumtaka rehema. Acheni utoto wa kumlaumu Rais, na kutaka ibada zizuiliwe, mtu anayewaza kuzuiliwa kwa ibada ni mpagani tu.
2Mambo ya nyakati 7:13-15
Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni;
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Kwa hiyo tujue kuwa solution ya pigo hili ni ibada na maombi ya toba. Mungu anataka watu wamrudie yeye
Wakuu,
Kwa taarifa nilizo nazo, ni kuwa muda si mrefu Rais Magufuli atalihutubia Taifa.
Kama hii itatokea, itakuwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani kuhutubia Taifa.
Tutarajie nini?
Stay tuned...
=======
LIVE:
View attachment 1395805
VIDEO:
Rais Magufuli anasema;
=> Baada ya kuibuka Ugonjwa wa Corona Serikali iliaanza kujipanga ikiwemo kutoa Elimu na kuwaandaa Wataalam.
=> Nashukuru Wizara na Vyombo vya habari kwa kushiriki kutoa Elimu kuhusu Ugonjwa huu wa Corona
=> Serikali iliandaa Madaktari kukabiliana na Ugonjwa huu
=> Tuliimarisha Sehemu za Viwanja vya ndege na Mipakani na kupeleka Vifaa vya kupima wale wanaoingia na kutoka.
=> Hadi sasa Nchi yetu imethibitika kuwa na Wagonjwa 12 huku wanne wakiwa kutoka nje ya nchi. Wagonjwa wote Wanaendelea Vizuri, Bado hatujapata habari ya kifo nchi kutokana na Ugonjwa huu
=> Hata Mgonjwa wetu wa kwanza leo ameonekana hana Virusi vya Corona na Wale wote walikuwa na maradhi haya, leo imeonekana negative.
=> Kufuatia kuingia kwa ugonjwa huu hapa nchini, Serikali imeendelea kuchukua hatua, mfano kuzuia mbio za Mwenge na bajeti yake kupelekwa Wizara ya afya ikatumike kusaidia kupambana na ugonjwa huu,
=> Tarehe 17 na 18 mwezi Machi kupitia Waziri Mkuu, Serikali ilitoa Maelekezo kuhusu uamuzi wa Serikali kuzifunga shule zote na vyuo vyote kwa mwezi mmoja ikiwemo kusitisha mikusanyiko ya ndani na nje, tumezuia michezo yote na mashindano mbali mbali.
=> Leo hatua nyingine tulizozichukua ni kama ifuatavyo:
=> Tumeunda Kamati ya kukabiliana na Ugonjwa huu na kamati hii itakuwa chini ya Ofisi ya Waziri mkuu.
=> Wasafiri wote wanaoingia nchini, Watalazimika kuwekwa Sehemu ya kujitenga [Karantini] kwa gharama zao wenyewe kwa siku 14 hata kama ni mwenyeji.
=> Wizara ya afya iboreshe maabara kuu na iboreshe vituo vya kuhudumia Wagonjwa ikiwemo kuongeza Vifaa.
=> Vyombo vya Usalama viimarishe USalama Mipakani kwa kuhakikisha watu hawaingii nchini hovyo hovyo.
=> Tumisitisha vibali vyote vya safari
=> Watu waendelee kufuata Maelekezo ya Wataaramu. nawasihi kuachana tabia ya kushikana mikono na kujishika pua na macho
=> Najua baadhi ya maeneo inawezekana mikusanyiko isiepukike kama sehemu za ibada, hospitali na makambini. Nawasihi watu wachukue tahadhari wanapokuwa maeneo hayo.
=> Nawasihi Watanzania kuacha kutoa utani na Mzaha juu ya ugonjwa huu ili kuzua taharuki na hofu. Watu watakao bainika wachukuliwe hatua.
=> Nawasihi watanzania tuepuke hofu zisizo na msingi. Kama tukifuata Uahsuri wa wataalam tutashinda adui huyu kama tulivyoshinda adui wengine
=> Nawahimiza tuendelee kuchapa kazi kwa bidii
=> Tuendelee kuchapa kazi kwa bidii kuijenga nchi yetu . Wakulima watumie mvua hizi kuchapa kazi ikiwemo Viwandani Wavuvi nk.
=> Napenda kutumia nafasi hii kutoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa kuliko wakati wowote. Hata Vitabu vya dini vinatufundisha kumuomba Mungu nyakati sura 7 mstari wa 14 pale wana wa Israel walipopatwa na Ugonjwa [2 Mambo ya Nyakati 7:14 inasema; Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.]
Quran Tukufu pia kitabu cha Al Baqara sura ya pili Mstari wa 155 [Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri ]
Waumini wote tusali na kuliombea taifa letu ili Corona isituvuruge.
Asanteni.