Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwanza Kabisa nachukua nafasi hii kutoa pole kwa Msiba wa Dkt Faustine Ndugulile, Lakini pole hii naitoa kwa familia yake tu, Sitoi Pole kwa Bunge wala kwa mwingine yeyote yule.
Baada ya Utangulizi huo naomba niingie moja kwa moja kwenye hoja yangu fupi sana, Ni hivi, Vyeo vya Kimataifa, kama vya WHO au UNICEF si vyeo vya kurithishana kama vyeo vya Tanzania, hivi ni vyeo vinavyogombewa baada ya Usaili mzito kutoka kwa Watu wenye akili nyingi, anayesailiwa ni mtu binafsi, Mtu huyo huchunguzwa mwenendo wake tangu huko kwao alikotoka kama yeye binafsi anao weledi.
Ndugulile alifukuzwa Uwaziri baada ya kumpinga Rais wa Tanzania, John Magufuli kuhusu namna ya kupambana na Korona, Magufuli aliamini katika Ushirikina wa Kupiga nyungu, Jambo ambalo Dr Faustine alilipinga, na likamgharimu Cheo chake na mambo mengine ambayo sitayataja, jambo hili ni miongoni mwa yaliyomfanya apigiwe kura na Watu wengi, Alichaguliwa Dr Ndugulile, haikuchaguliwa Tanzania
Vyeo vya WHO si kama Ubunge wa ccm, kwamba kwa vile Selina Kombani kafa basi Ubunge wake tumpe Mwanaye, mwanaye ambaye kazi yake kubwa bungeni ilikuwa kuorodhesha dawa za kuongeza nguvu za kiume likiwemo vumbi la Congo, Nani aliyesahau hili?
Hoja yangu ni kwamba Kifo cha Dr Faustine hakitaifanya Tanzania ionewe huruma ili Hata wakipeleka mgombea Duni basi achaguliwe tu.