Angalizo: Wanaoweka matangazo ya kutafuta Kazi

Angalizo: Wanaoweka matangazo ya kutafuta Kazi

Naitwa isaya mtewele natafuta kazi yeyote nina elimu ya kidato cha nne lakini pia nimefanya kazi ya usimamizi kwenye duka la vifaa vya ujenzi kwa miaka 5 nina uzoefu pia kama kuna kampuni la vifaa vya ujenzi au linalojihusisha na ujenzi pia naweza kuwa balozi wao kwa kutangaza bidhaa zao mikoani ahsante
 
Wasifu: Mimi ni kijana mkarimu na mchapakazi, mwenye umri wa miaka 27 ninayepatikana Ukonga Mombasa (karibu na Gongo la Mboto).

Elimu: Nina shahada ya Menejimenti ya Uhandisi wa Viwanda kutoka Chuo Kikuu Mzumbe; nime'base zaidi katika masuala ya utafiti, miradi, uvumbuzi na teknolojia, pamoja na menejimenti.

Uzoefu: Nina uzoefu wa miaka 3 katika kazi za mtandaoni, utafiti, usimamizi miradi na operesheni. Nimefanya kazi mtandaoni kama Data Entry and Research Volunteer katika kampuni mbili za kiteknolojia za Ulaya (Compaira, Deal Lite); Personal and Delivery Assistant wa CEO katika Hamashiach Bookshop; Organizing Team Leader wa Employability Africa program kutoka SC Konsult; Operations and Digital Platforms Manager katika kampuni ya usafirishaji (Afritrust Holdings Limited). Pia, nimefanya kazi kama Field Officer na Enumerator katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Nje na kazi, mimi ni mjasiriamali niliyepata mafunzo kutoka UDIEC GEP 2021 na Digify Tech 2021; Mwanaharakati wa masuala ya vijana niliyepata mafunzo maalum kuhusu elimu, kazi na afya ya akili kutoka katika mkutano wa kimataifa wa YOUNGA 2022; Msaidizi wa mtandaoni (Virtual Assistant) niliyeidhinishwa na ALX Africa baada ya kuhitimu vizuri mafunzo 2022.

Mapendeleo: Napendelea kufanya kazi kama Research Assistant, Project Assistant, Personal or Executive Assistant (wa mtu binafsi, shirika au kampuni), Tutorial Assistant, Training Assistant, Customer Service Officer, Digital Platforms Manager, Data Entry Specialist au Data Manager, katika maeneo yoyote (ikiwemo Posta, Mnazi mmoja, Makumbusho, Masaki, Tegeta, Bunju, Mbagala) ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Mimi ni mtu niliye'flexible hivyo naweza kufanya kazi katika mazingira ya aina yoyote (office, hybrid, work-from-home, fast-paced, collaborative, travel). Napendelea kufanya kazi ya part-time au kwa mkataba (lakini ikibidi, nipo tayari kufanya kazi full-time au hata kwa kujitolea).

NB: Kwa kuwa pia mimi ni Msaidizi wa Mtandaoni, naweza kufanya mbalimbali za uandishi (content writing, proofreading/grammar checking, English-Swahili translation) na za mtandaoni (account management, email management, documentation, online navigation, phone/computer backup, digital skills training, Windows and Office local activation). Huwa nafanya kazi kwa umakini, usiri na ubora.

Mawasiliano:
Simu - 0743744471
 
Natafuta kazi yeyote ,na elimu ya diploma ya pharmacy
Sina vyeti Wala experience
Niko Dar es salaam -kimara
Nashida sana natakiwa nijiinue
 
Habari wakuu Mimi Nina certificate ya laboratory technician pia Nina experience ya miaka 3 kuhusu laboratory technician, laboratory analysis, QC,QA pia blending oparetor au syrup oparetor pia naweza kufanya kazi popote pale penye maabara au panapozalishwa bidhaa .yeyote atakaye nisaidia kupata connection ya job nipo tayri kuingia naye mkataba awe anakata 10% ya mshahala wangu ndani ya miezi 12.asanteni
 
Wanajamii forums, na mimi natafuta kazi

sifa zangu ni kama zifuatazo

(1) nina bachelor degree masuala ya banking and finance

(2) nina cheti cha film and Tv production

(3) nina experience ya kazi ya marketing
(4) nina experience ya kutengeneza filamu na video ads

(5) nina skills za graphics design (both motion and still graphics)

ninafaa sana kwa masuala ya marketing
Kwann usijiajiri upande wa social media?
 
thumb20.jpg


Salaam!

Ni muda sasa humu Jukwaani kumekuwa na mabandiko ya watu mbalimbali wakiomba kazi, zile za ujuzi mahususi na zile za jumla.

Baadhi ya wanaoandika wamekuwa wakitaja sifa zao, wengine wakitaja kwa upana na wengine kwa ufupi sana na wakati mwingine bila taarifa zozote zitakazomwezesha mwajiri kupata fununu za mtu anayetaka kumuajiri.

Kama ambavyo wanaoweka matangazo ya kazi waliaswa hapa: ZINGATIA-Mnaoweka matangazo ya kazi humu nadhani ni wakati wa wanaoweka matangazo ya kusaka kazi pia tukazingatia vigezo kadha wa kadha.

Walau tangazo la kutafuta kazi liwe na vitu vifuatavyo:



  • Wasifu, kwa kuwa kanuni za JF zinalinda haki ya faragha, utambulisho uhusishe wasifu mwingine ISIPOKUWA majina. Mathalani, mwombaji anaweza kusema kuwa yeye ni kijana mwenye umri wa miaka XX anayepatikana eneo XY.
  • Elimu, hii inasaidia mtu ambaye anaomba kazi kuweka wazi elimu aliyonayo, iwe ya jumla au ya utaalamu mahususi. Waajiri au wenye kujua fursa za ajira wangependa kujua elimu aliyonayo mhitaji ili wamsaidie iwezekanavyo.
  • Uzoefu. Hiki ni kigezo kinachompa sifa za ziada mwombaji. Ni vema kusema kama umewahi kufanya kazi, semina ama kuhudhuria mafunzo fulani maalumu kwani itaongeza ushindani wa mwombaji.
  • Mapendeleo. Kutaja elimu na uzoefu pekee hakutoshi, ni vema muombaji/mhitaji akaweka wazi kazi, eneo, mazingira ya kazi ambayo anayapendelea pamoja na vitu vingine vya ziada. Kuandika kwa ujumla sana hupelekea wasio na nia njema kujibu kwa kejeli na dhihaka. Kuwa mahususi na kazi itakiwayo kutapunguza majibu mengi yasiyofaa kwa mwombaji.
  • Andiko lisiwe na nia ya kuvuta sana usikivu. Maandiko yenye uelekeo wa kulia-lia, kutangaza kuwa maisha ni magumu na hujui ufanyaje hakurahisishi harakati za kupata kazi. Watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia uhitaji huo uliopitiliza kwa manufaa yao kiuchumi (utapeli) na hata kingono (hasa kwa mabinti).

Nawatakieni kila lililo jema katika harakati za kusaka ajira!
Shukran
 
Back
Top Bottom