mtu m-bayaaaa
New Member
- Dec 20, 2021
- 4
- 3
habar....... nlikua naulizia kuhusu vyuo vinavyotoa diploma ya ualimu wa shule ya msingi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Good luck kijana wa NsumbaHABARI.
Naitwa HAMIS I JUMANNE, nina degree ya MEDICAL LABORATORY Katika chuo cha Muhimbili. Ninauzoefu wa kazi hii, nimefanya kazi kama mtarajali(Intern)katika hospitali ya rufaa ya SEKOUTOURE November 2020_november 2021.
Ninavyeti vyote Pia nina usajili uliokamilika kutoka board ya Maabara Tanzania.
Natafuta kazi.
Contacts: 0742567912/0626333059
Email:hamis4831@gmail.com
Unaumri gani ?Habari zenu wapendwa! Kwa majina naitwa Mary nipo mkoa wa dare salaam nina elimu ya kidato cha nne natafuta kaz yyte na nipo tayar kwenda mkoa wwt ule mwenye connection naomba anisaidie
ahsante saaan kwa kutujuza,MUNGU awabariki![]()
Salaam!
Ni muda sasa humu Jukwaani kumekuwa na mabandiko ya watu mbalimbali wakiomba kazi, zile za ujuzi mahususi na zile za jumla.
Baadhi ya wanaoandika wamekuwa wakitaja sifa zao, wengine wakitaja kwa upana na wengine kwa ufupi sana na wakati mwingine bila taarifa zozote zitakazomwezesha mwajiri kupata fununu za mtu anayetaka kumuajiri.
Kama ambavyo wanaoweka matangazo ya kazi waliaswa hapa: ZINGATIA-Mnaoweka matangazo ya kazi humu nadhani ni wakati wa wanaoweka matangazo ya kusaka kazi pia tukazingatia vigezo kadha wa kadha.
Walau tangazo la kutafuta kazi liwe na vitu vifuatavyo:
- Wasifu, kwa kuwa kanuni za JF zinalinda haki ya faragha, utambulisho uhusishe wasifu mwingine ISIPOKUWA majina. Mathalani, mwombaji anaweza kusema kuwa yeye ni kijana mwenye umri wa miaka XX anayepatikana eneo XY.
- Elimu, hii inasaidia mtu ambaye anaomba kazi kuweka wazi elimu aliyonayo, iwe ya jumla au ya utaalamu mahususi. Waajiri au wenye kujua fursa za ajira wangependa kujua elimu aliyonayo mhitaji ili wamsaidie iwezekanavyo.
- Uzoefu. Hiki ni kigezo kinachompa sifa za ziada mwombaji. Ni vema kusema kama umewahi kufanya kazi, semina ama kuhudhuria mafunzo fulani maalumu kwani itaongeza ushindani wa mwombaji.
- Mapendeleo. Kutaja elimu na uzoefu pekee hakutoshi, ni vema muombaji/mhitaji akaweka wazi kazi, eneo, mazingira ya kazi ambayo anayapendelea pamoja na vitu vingine vya ziada. Kuandika kwa ujumla sana hupelekea wasio na nia njema kujibu kwa kejeli na dhihaka. Kuwa mahususi na kazi itakiwayo kutapunguza majibu mengi yasiyofaa kwa mwombaji.
- Andiko lisiwe na nia ya kuvuta sana usikivu. Maandiko yenye uelekeo wa kulia-lia, kutangaza kuwa maisha ni magumu na hujui ufanyaje hakurahisishi harakati za kupata kazi. Watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia uhitaji huo uliopitiliza kwa manufaa yao kiuchumi (utapeli) na hata kingono (hasa kwa mabinti).
Nawatakieni kila lililo jema katika harakati za kusaka ajira!
Asante Sana![]()

Sawa kbxasante sana kwa kutukimbusha aisee wengi wetu tunajisahau sana