Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 783
- 2,057
Hatutaki baadaye kuja na zile swaga za kushiba makande ya mchana na kuanza kuangalia upepo umelalia wapi ndio mnaibuka!
Inatakiwa tujue mapema hii timu ni ya aina gani ili kusudi tuweke kumbukumbu sawa.
Kuna wale vijana wa Mwenyekiti Rage washasema ndio mwisho wa Yanga, hawatoboi kutokana na ubora wa El Merekh lakini kuna wengine ni kama vile wanasita kutoa tamko; hawajui wawe upande upi wa shilingi, wanaogopa kusutwa mambo yakiwa ndivyo sivyo.
Tunawataka hao wachague upande tuwajue, hatutaki unafiki na uzandiki wa kusubiria matokeo ndio waanze kutujazia nyuzi hapa zisizokuwa na kichwa wala miguu!