Kuna mtu ameshauri Serikali vibaya kimazoea!,bila kujali maslahi ya wapenda soka.
Raia wanapaswa kuwa huru kwenda watakapo,kusikiliza watakacho,kuona watakacho ili mradi hawavunji sheria.
Serikali imezoea kupora uhuru wa raia kuamua wakitakacho,sasa leo maelekezo ya Serikali kwenda chama cha mpira imeleta madhara(Mechi imeahirishwa huku washabiki wakipata hasara ya fedha waliotoa baada ya mechi kuvunjika).
Watendaji,wamezoea kutoa ushauri wa kujipendekeza bila kufanya tathimini yenye kujali maslahi ya wengi.
BORA RAIS AFANYE MABADILIKO ZAIDI KWA WATENDAJI,KUNA MAMBO WANAYOYAFANYA HAYAENDANI NA MTAZAMO WA SERIKALI YA AWAMU YA 6.