Badala ya kujibu unakimbilia kutoa lugha za ovyo...
Binafsi nishasema sana hapa kwamba JPM Administration ilijaa UONGO lakini tukaonekana tuna chuki!!
Ripoti ya CAG (Development Projects) ambayo ilitolewa wakati JPM akiwa hai ilieleza mengi kuhusu Bwawa la Nyerere! Na wakati huku mitaani mkidanganywa mambo ni bam bam, ukweli ni pamoja na ufuatao:-
View attachment 2143150
Wakati wewe ukiamini mipesa ipo tu kwa sababu ndivyo mlivyokuwa mnaambiwa, CAG alishindwa kuona bajeti for 2 consecutive financial years.
Bajeti ambayo CAG alithibitisha kuwepo ni kwa 2019/20 and 2020/2021 ambayo unaona hapo TOTAL ni takribani TZS 3 Trillion, wakati Project Cost ni takribani TZS 7 Trillion!
Now endelea kuamini JPM alishatenga matrilions za kumalizia huo mradi!!
Je, baada ya kazi kuanza... mambo yalienda mserereko kama mlivyokuwa mnaambiwa huku mitaani?!
Setback ya kwanza ilikuja baada ya TANESCO kumruhusu Contractor kujenga 1 Diversion Tunnel badala ya 2 kama ambavyo mkataba ulikuwa unase,a. Matokeo yake, iliponyesha mvua, na kutokea mafuriko maji yakapanda juu!
View attachment 2143174
Outcome: Project ika-delay kwa miezi 5
View attachment 2143173
Again, endelea kuamini kwamba angewepo JPM basi mradi ungekamilika by June 2022 wakati tayari setbacks zilishatokea tangu wakati akiwa hai huku mkiambiwa "mambo kama kawa"!!
Je, baada ya ku-delay for 5 months, ina maana mambo ndo yakaanza kwenda kwa mserereko?! CAG mnoko ambae solution yake ilikuwa kuto-renew mkataba wake anaendelea hapa chini"-
View attachment 2143181
E bhana eh!
Kumbe wakati watu wanasubiria kusherehekea Mwaka 2021, mradi ndo kwanza ulikuwa umefikia 28.61%... ikiwa ni delay ya takribani 7 months.
Hapa nakukumbusha tu kwamba, hadi JPM anakutwa umauti, kuna kila dalili mradi ulikuwa hujafikia hata 35% completion rate!!
Je, shughuli zingine zilikuwa zinaenda kwa kasi?!
Summary ya project implantation ni kama inavyoonekana hapa chini:-
View attachment 2143187
Kumbe hadi CAG anaingia mitamboni, kulikuwa na major project components kibao ambazo zilikuwa hata hazijaanza huku zikiwa zime-delay kwa miezi kadhaa! Kuanza kwa ujenzi wa Permanent Bridge kwa mfano, ilikuwa ime-delay kwa zaidi ya Siku 500... sasa yale ma-crane yanayotakiwa kuwekwa kwenye tunnels sijui yatapitia wapi!!
All in all, yote hayo huenda yasingekuwa big issue kama kungekuwa na pesa ya kutosha!! Na hata mwanzoni mambo yalianza kwenda fasta baada ya kuchukua syndicated loans from Trade Development Bank ($ 1 Billion) na Credit Suisse ($0.5 Billion)!
Na hii mikopo inakuja wakati tuna 2 major projects, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa ikawa pesa inayopatikana inakuwa distributed kwenye hizo projects 2.
Mikopo mingine ambayo JPM alifanikiwa kuipata kabla hajafariki ni pamoja na mkopo wa
$400 Million kutoka UBA.
Hapo ndipo tunarejea swali uliloulizwa na
JokaKuu ambalo umejibu kirahisi mno... "mbona kipande cha SGR kutoka Dar to Moro tu, alishindwa kumaliza"?
Sasa endelea kusingizia Wakandarasi na akina Makamba wakati uhalisi ni kwamba, hata wakati JPM anaaga dunia, bado sehemu kubwa ilikuwa haijafanyika!!